ampa dakika za kutosha kumshambulia na kumtukana na kujitangaza kua yeye ni msafi na kutangaza kuwa atagombea wa urais wa Zanzibar.
Ninajiuliza ni sawa kwa mheshimiwa spika kufanya haya?
Kwa nini asiache hayo masuali ya Hamad Rashid wamalizane kwenye vyombo vya habari kama Maalim alivyofanya?
Mtanzania Wameandika Hivi Kuhusu Hilo:
MJUMBE wa Bunge Maalumu la Katiba ambaye pia ni Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF), amemshambulia kwa maneno Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Maalim Seif Sharif Hamad, huku akimfananisha na popo.
Mbunge huyo alisema hayo baada ya kupewa nafasi na Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta, akisema lengo ni kujibu mashambulizi yaliyoelezwa kwake na Maalim Seif kupitia kituo kimoja cha televisheni.
Baada ya kupewa fursa hiyo, Hamad alisema Maalim Seif hafai kuwa kiongozi kwa kuwa hana msimamo kisiasa jambo ambalo linamfanya awe kama popo ambaye hajulikani kama ni ndege au mnyama.
No comments:
Post a Comment