Miss
Nasreem Abdul akiwa pamoja na wasichana waliofanyiwa ukatili na
kutelekezwa na sasa wanalelewa na Taasisi ya wanawake katikaa Jitihada
Kimaendele 'WAJIKI' Kilichopo Mwananyamala Kinondoni Jijini Dar.
Miss Ilala
namba mbili Nasreem Adbul ameonesha mfano wa kuigwa kwa warembo wengine
baada ya kuwapatia zawadi watoto yatima wenye uhitaji na wanaoishi
mazingira magumu.
Kwa mujibu wa meneja wa mrembo huyo
Livingstone Mkoi alisema kuwa" Katika kile kinachoonekana kuguswa na
matatizo ya kijamii na ni siku chache tu tangu achukukue ushindi wa
pili katika kinyang'anyilo cha kumtafuta Miss Ilala mrembo wetu
ametembelea vituo kadhaa vya watoto yatima pamoja na TAASISI YA WANAWAKE
KATIKA JITIHADA KIMAENDELEO "WAJIKI" Iliyopo Mwananyamala Jijini Dar na
kutoa kile alichokuwa nacho" Alisema Mkoi
Aidha kituo kingine alichotembelea mrembo huyo ni cha AL- HIDAYA
ORPHANS CENTER Kilichopo Buguruni ambacho kina watoto zaidi ya 70 huku
kila siku wanaongezeka.
Hata hivyo kwa upande wa mrembo huyo
alisema" Namshukuru Mungu kwa kunisaidia kuwa mshindi wa pili na wiki
hii tunaingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya shindano la Taifa la
Urembo hivyo nimeguswa na matatizo wanayoyapata watoto yatima na ndiyo
maana nimetoa zawadi yako kwako kama msaada na Mungu akinijalia baadae
tena nikishinda taji la Taifa nitaendelea mikoani kwani watoto wako
wengi wanaoitaji msaada" Alisema Nasreen
No comments:
Post a Comment