Mwenyekiti wa CWT Manispaa ya Iringa Zawadi Mgongolwa akisisitiza jambo wakati akitoa salamu zake kwa walimu leo uwanja wa samora |
Mgongolwa akiwataka walimu kuendelea kufanya kazi kwa moyo japo mishahara yao haitoshi |
Walimu wakiwa katika maandamano hayo leo |
Maandamano ya walimu Iringa |
Walimu katika maandamano yao leo
Ujumbe unasomeka wadau
Mgeni rasmi katika siku ya walimu
Manispaa ya Iringa Bw Adam Swai wa tatu kulia ambae amemwakilisha
naibu waziri wa TAMISEMI Kasimu Majaliwa akipokea maandamano ya
walimu
Walimu wakiingia katika uwanja wa Samora kwa maandamano leo
Ulinzi ukiwa kamili gado
Walimu Manispaa ya Iringa wakiimba wimbo maalum wa walimu wakati wa maadhimisho ya siku ya mwalimu duniani
JESHI la Polisi
wilaya ya Iringa mkoani Iringa leo limeweka ulinzi mkali kwa kuweka
askari wa FFU wakati wa maandamano ya siku ya mwalimu Duniani ili
kuthibiti wafuasi wa vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi
(UKAWA)kujichomeka katika maandamano hayo.
Askari hao wa FFU na wale wa kawaida walionekana katika maeneo
mbali mbali ya mji wa Iringa huku baadhi yao wakiwa katika uwanja
wa Samora ili kuhakikisha wanaoshiriki maandamano hayo ya siku ya
mwalimu ni walimu na si vinginevyo .
Mtandao
wa www.matukiodaima.co.tz umeshuhudia askari wa FFU wakiwa
wamejiandaa kikamilifu kwa kuwa na mabomu ya machozi huku walimu
hao wakithibiti vikali wasio walimu kushiriki katika maandamano hayo
kwa kuweka uzio mango la kitambaa nyuma ya maandamano hayo na
viongozi wake kuwa nyuma ya uzio huo na polisi na mbele viongozi
wengine wakiwa wametangulia na polisi.
Mmoja
kati ya walimu walioshiriki maandamano hayo alisema kuwa
wamelazimika kuweka uzio huo ili kuwawezesha walimu kushiriki
maandamano hayo bila watu wengine kujipenyeza kwa malengo hayo ili
kuvuruga siku hiyo ya mwalimu.
Kwani
alisema tetesi za chini kwa chini walisikia kuwepo kwa watu wa
UKAWA kutaka kushiriki maandamano hayo kwa malengo yao ya kupinga
katiba jambo ambalo wao kama walimu baada ya kulipata waliamua kuwa
makini zaidi ili kuepusha siku yao kuingizwa mambo ambayo si
malengo haswa ya mwalimu.
Hata hivyo
hakukuwa na vurugu zozote zilizopata kujitokeza katika maandamano
hayo kutokana na waandamanaji hao kufanya maandamano ya amani chini
ya ulinzi wa polisi ambao walikuwa nyuma zaidi ya waandamanaji ili
kuthibiti wale wasiopenda amani kujipenyeza .
Akitoa
salamu za walimu katika maadhimisho hayo ya siku ya mwalimu Duniani
mwenyekiti wa chama cha walimu (CWT) manispaa ya Iringa Zawadi
Mgongolwa alisema kuwa mbali ya mwalimu kufanya kazi kwa kujituma
ila bado mwalimu ameendelea kuishi maisha ya shida kutokana na
serikali kushindwa kuwathimini walimu nchini.
" Sherehe hizi za mwalimu duniani
hufanyika kila mwaka Octoba 5 ila kwa Manispaa ya Iringa tumeamua
kuifanya leo ili kuwapa nafasi walimu wanaokwenda mkoani Kagera
katika sherehe za kitaifa .....ndugu mgeni rasmi huwa tunapenda
kukutana mara kwa mara ila tunashindwa kuthiminiwa na serikali
yetu"
Alisema kuwa ofisi ya chama cha
walimu Manispaa ya Iringa iliweka utaratibu wa kukutana na walimu
ila ofisi ya mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imekuwa
ni tatizo kuwa katika kuwaunganisha walimu pamoja na hata katika
maadhimisho hayo ni walimu chini ya 10000 ndio wameshiriki kati ya
walimu zaidi ya 2000 waliopo mjini Iringa.
Hivyo alisema kuwa wameamua kufanya
sherehe hizo wenyewe ili kuuganisha umoja wa walimu mbali ya
Manispaa ya Iringa kuwatenga walimu hao na kuwa itafika siku
watafikisha malalamiko yao rasmi katika ofisi ya TAMISEMI ili chama
hicho kiweze kuwa chama rafiki na serikali .
Mwenyekiti huyo aliwataka walimu hao
mbali ya kuendelea kutothaminiwa na Manispaa ya Iringa ila bado
wanapaswa kuendelea kuifanya kazi hiyo kwa moyo ili kuliendeleza
Taifa na kuwa kazi hiyo ya ualimu ni wito na kuwa wanapigana kwa
ajili ya vizazi vijavyo na si vinginevyo na kuwa kauli mbiu yao ya
Taifa lisilo jali walimu halina mipango ya kimaendeleo iwe
chachu kwa pande zote mbili walimu na serikali.
CHANZO MZEE WA MATUKIO DAIMA.
No comments:
Post a Comment