WATU wasiofahamika wamevamia tawi la
CCM eneo la stendi ya Taxi nyuma ya posta mjini Iringa na kushusha
bendera mbili zilizokuwa zimetundikwa eneo hilo na kuzichana
chana .
Tukio hilo limetokea usiku wa
kuamkia jana kwa watu hao kufika katika eneo hilo kufanya
hujuma hiyo dhidi ya bendera za CCM eneo hilo .
Mwenyekiti wa eneo hilo James Mpete
alimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa bendera hizo
waliziweka kwa ajili ya kuhamasisha uhai wa CCM na kushawishi
vijana zaidi kubadilika na kujiunga na CCM baada ya kuwepo dalili
za ubabaishaji ndani ya Chadema.
Hivyo alisema kuwa mbali ya awali eneo
hilo kuwa na bendera za CCM na Chadema kutokana na muda ulivyozidi
kwenda ndipo vijana wa eneo hilo walipoamua kugeuka na wale wa
Chadema kuungana na wenzao wa CCM katika kuhamasisha uhai wa chama
na kupinga uwajibikaji hafifu wa mbunge wa jimbo hilo mchungaji
Peter Msigwa .
Mpete alisema kuwa katika hali ya
kushangaza ni baada ya watu hao kuvamia eneo hilo na kushusha
bendera za CCM na kuzichana kitendo ambacho wao wanakiona kama ni
hujuma kubwa na wapo katika harakati za kuwasaka waliofanya
hivyo.
" Kila mmoja ana chama chake na
siasa si ugomvi sasa tunashangaa kuona watu wanatuchania bendera
zetu .....kweli tupo katika uchunguzi mzito wa kuwasaka
wanaoendesha siasa za vurugu hivi" alisema mwenyekiti huyo .
Kuwa wanaimani kubwa kuwa waliofanya
hivyo ni wafuasi wa UKAWA na wamefanya hujuma hiyo baada ya
kuzuiliwa kufanya maandamano na wameona hasira zao wazimalizie
katika bendera za CCM jambo ambalo halina mahusiano na wao kuzuiwa
maandamano yao.
Hali ya kisiasa katika jimbo hilo la
Iringa mjini bado si njema kwa vyama vikuu viwili Chadema na CCM
kutokana na mvutano uliopo ndani ya vyama hivi vikuu katika jimbo
hilo la Iringa mjini .
Kwa upande wa CCM wapo katika mkakati
wa kumwondoa mbunge Msigwa kupitia oparesheni inayoendeshwa chini ya
katibu wa mkoa wa CCM Hasan Mtenga oparesheni iliyopewa jina la ondoa
Msigwa Iringa hivyo kutokana na hali hiyo vita ya kushindana kushushiana bendera ndio ambayo imeendelea katika jimbo hilo .
|
No comments:
Post a Comment