Yafuatayo ni baadhi ya mambo unayoweza kuyafanya ili kuwa na afya
bora katika mwaka huu wa 2011.Lakini kabla sijaendelea mbele sana,naomba
niweke wazi kwamba afya bora haihusu kula vizuri na mazoezi peke yake
bali pia fikra chanya(positive attitude). Kuna umuhimu wa kuhakikisha
kwamba siku zote unakuwa na mawazo chanya na pia kuwa karibu zaidi na
watu wenye mawazo chanya.
1.Kunywa Maji kwa wingi- Bila shaka unakumbuka msemo
“Maji ni Uhai”.Hiyo ni kweli kabisa.Maji ni uhai sio tu kwa mazingira
yetu na dunia kwa ujumla bali pia kwa afya au miili yetu.Maji ni kitu
muhimu sana kwa afya zetu.Asilimia 60% ya miili yetu imetengenezwa au
imesheheni maji. Maji yanahitajika kwa ajili ya kuondoa takataka au vitu
visivyofaa kutoka mwilini.Maji ndio hubeba virutubisho na oxygen.
Kiasi cha maji anachohitaji mtu kinategemea na mambo kadhaa kama vile unyevu(humidity) wa mahali ulipo,shughuli zinazohusisha mwili anazozifanya mtu na pia uzito wa mwili.Pamoja na hayo,kwa wastani miili yetu inahitaji lita 2 na nusu mpaka 3 za maji.Vyakula tunavyokula huchangia kama asimilia 20% za maji katika miili yetu.Kwa hiyo tunahitaji kunywa maji kiasi cha lita 2 mpaka lita 2.4 au glasi 8-9 za maji kwa siku.

Njia rahisi ya kujua kama mwili wako una maji ya kutosha ni katika
kuangalia mkojo. Mkojo wako unatakiwa kutokuwa na rangi(colorless) au
kuwa wa njano kidoogo.Kinyume cha hapo ni ishara kwamba hauna maji ya
kutosha mwilini.Njia nyingine kutambua ni pamoja na kukaukwa na
midomo(lips) na hata ulimi na pia kupata kiasi kiduchu cha mkojo.
Pata Usingizi wa Kutosha: Unakumbuka tulipokuwa
wadogo wazazi wetu walisisitiza sana kwamba twende tukalale mapema ili
tukue? Bila shaka walikuwa wanajua kwamba usingizi ni sehemu muhimu sana
katika afya. Ukiachilia mbali faida za usingizi kwa ajili ya afya za
akili/ubongo wetu,usingizi au mapumziko ya kutosha ni muhimu kwa
miili.Afya njema huenda sambamba na mapumziko.Ni wakati wa kuupa mwili
nafasi ya kujijenga,kujiongezea nguvu na muhimu zaidi kuhakikisha kwamba
tunakuwa na akili timamu. Pia ukosefu wa usingizi ni chanzo cha kuzeeka
mapema.
Fanya Mazoezi- Hili linaweza kupita bila maelezo ya
ziada.Mazoezi ni muhimu sana kwa afya bora. Fanya mazoezi angalau mara
tatu katika wiki.Jipatie muda wa kutembea japo kwa dakika 30. Kama
inawezekana nenda Gym.Badala ya kupanda lifti pale kazini kwako au
mitaani,tumia ngazi za kawaida.Egesha gari lako mbali kidogo na
unapokwenda ili upate nafasi ya kutembea nk. Muhimu zaidi ni kuchagua
aina ya mazoezi unayoipendelea. Mazoezi hayatakiwi kuwa adhabu.
Faida za mazoezi ni pamoja na kujiepusha na magonjwa mbalimbali,kupunguza unene(bila shaka unajua kwamba unene kupindukia sio afya bali ni ugonjwa na sababu kubwa ya maradhi mengine)
Faida za mazoezi ni pamoja na kujiepusha na magonjwa mbalimbali,kupunguza unene(bila shaka unajua kwamba unene kupindukia sio afya bali ni ugonjwa na sababu kubwa ya maradhi mengine)
Kula Matunda Kwa Wingi-Matunda ni chanzo kizuri sana
cha madini na vitamins ambazo miili yetu inahitaji sana kwa ajili ya
afya bora. Unajua kwamba machungwa,kwa mfano, yana faida kubwa zaidi
kiafya kuliko vidonge vya Vitamin C unavyobugia kila leo? Aina
mbalimbali za matunda ambayo yana virutubishi vingi zaidi kiafya ni
Parachichi(Avocado),apple,matikiti
maji(cantaloupe),Zabibu(Grapefruit),Kiwi,Guava,mapapai,machungwa,
strawberries nk.
Kula mboga za majani- Kama ilivyo kwa matunda,mboga za
majani(vegetables) ni muhimu sana kwa afya zetu. Wataalamu wa afya
wanashauri kwamba tule aina 5 mpaka 9 za mboga za majani na
matunda.Jitahidi kupata angalau zaidi ya aina 5 za mboga za majani na
matunda.
Punguza Kula Vyakula vya Makopo- Kutokana na jinsi
dunia inavyozidi kwenda mbio,watu wengi huwa tunakosa muda wa
kupika.Matokeo yake tunakimbilia kwenye vyakula vya kwenye makopo
ambavyo ndivyo vimejaa katika maduka na ma-supermarket. Jitahidi
kuviepuka vyakula hivyo kwa kadri unavyoweza.Mara nyingi vyakula vya
makopo huwa na ingredients ambazo hazifai kwa afya zetu.Kwa mfano,vingi
miongoni mwa vyakula hivyo huwa na chumvi nyingi kitu ambacho ni chanzo
cha High Blood Pressure na maradhi ya moyo. Unaposhindwa kabisa kujizuia
kununua vyakula hivyo vya makopo jaribu kuangalia ambavyo havina sukari
au chumvi.
Jipende- Kama nilivyodokeza hapo mwanzo,afya bora
huenda sambamba na afya ya akili/ubongo.Njia mojawapo ya kupata afya
hiyo ni pamoja na kujipenda.Pengine unajiuliza,kuna mtu ambaye
hajipendi? Ukweli ni kwamba pengine ni kweli kwamba hakuna mtu ambaye
hajipendi.Tofauti inakuja pale mtu anapofanya vitu ambavyo ni kinyume
kabisa na mapenzi ya mwili.
Mfano,uvutaji sigara,unywaji pombe kupindukia,kutojisafisha mwili wako kwa mfano kuoga,kupiga mswaki na pia kupumzika nk.Hizo zote ni tabia ambazo zinaweza kuonyesha jinsi ambavyo hujipendi au huupendi mwili wako.Kama unaupenda utautumia vibaya au kuuharibu?

No comments:
Post a Comment