KATIBU
wa itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) Taifa Nape
Nnauye ambana mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa
amfananisha na mpangaji na kuwa kodi yake ya kuendelea kudumu katika
jimbo hilo imekwisha hivyo ajiandae kufungasha vilago ili uchaguzi
mkuu 2015 akabidhi jimbo hilo CCM.
Nnauye alitoa kauli hiyo leo mara
baada ya kuwasili katika jimbo la Iringa mjini kwa ajili ya ziara
siku 6 mkoani Iringa na katibu mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana
Alisema kuwa CCM imekusudia
kuyarejesha majimbo yote yaliyochukuliwa na wapinzani mwaka 2010
likiwemo jimbo la Iringa mjini linaloongozwa na mbunge wake mchungaji
Msigwa na kuwa uwezo na nia ya kulikomboa jimbo hilo upo hivyo ni
lazima wapangaji wote kuanza kukaa mkao wa kuondoka .
" Tutakuwa na ziara mkoa wa Iringa kwa
muda wa siku 6 na hadi tukimaliza ziara yetu hapa Iringa chama
chetu kitakua juu zaidi hivyo nawaombeni fikisheni salam kwa
wapangaji kuwa kodi yao imekwisha na hivyo tunahitaji watuajie
jimbo letu na kwa sasa hatuna mpango wa kupangisha tena" alisema
Nnauye huku akishangiliwa na umati wa wananchi wa jimbo la Iringa
mjini waliokuwepo katika mapokezi hayo.
Akizungumza na wanachama hao kabla
ya kuzindua ofisi ya CCM wilaya ya Iringa vijijini Iliyofanyiwa
ukarabati upya katibu mkuu ,Abdulrahman Kinana
alisema kuwa CCM imeendelea kukamilisha utekelezaji wa ahadi zake
ambazo ziliahidiwa mwaka 2010 na kuwa hadi sasa sehemu kubwa ya
ahadi hizo imetekelezwa na kilichobaki ni kuwaomba watanzania
kuendelea kuwa na imani na CCM ili mwakani 2015 kuendelea kuchagua
chama hicho.
Kinana
alisema kuwa kazi kubwa imeendelea kufanywa na viongozi wa CCM
na serikali yake chini ya Rais Jakaya Kikwete katika kuona
watanzania wanaendelea kunufaika na matunda ya serikali yao kwa
kusogezewa maendeleo karibu zaidi na kutaja miradi mkubwa ambayo
imetekelezwa kuwa ni pamoja na ujenzi wa barabara za lami kila kona
ya nchi hii.
"
Tunazunguka kuendelea kukijenga zaidi chama lengo ni kuona
watanzania wanaendeleo kukiamini chama na kuhamasisha zaidi wananchi
kujitokeza kwa wingi katika chaguzi za serikali za mitaa mwaka huu
ili kuchagua viongozi wanaotokana na CCM kwani ndicho chama chenye
mapenzi ya kweli ya kuliongoza Taifa hivyo hakuna sababu ya
watanzania kutokiamini chama cha mapinduzi"
Pia
alisema kuwa mbali ya CCM kuendelea kukamilisha utekelezaji wa ilani
yake ya uchaguzi bado chama hicho kina mpango mzuri wa watanzania
ili kuona mwakani 2015 chama kinashinda na hapa watanzania wategemee
ahadi nyingi na kubwa zaidi ya zile za mwaka 2010.
Awali Kinana alimpongeza aliyekuwa
mjumbe wa bunge la katibu na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca
Msambatavangu kwa jinsi alivyowawakilisha vema wakazi wa mkoa wa
Iringa na watanzania kwa ujumla katika bunge la katiba na kuwa
alikuwa akimfuatilia na kufurahishwa na uwezo wake mkubwa wa kujenga
hoja.
Kwa upande wake Msambatavangu
akimkaribisha katibu mkuu huyo alisema kuwa mbali ya kuwa ziara
hiyo inaanzia jimbo la Kalenga kwa upande wa wilaya ya Iringa vijijini
ila mbunge wake Bw Godfrey Mgimwa hatafanikiwa kushiriki kutokana na
heshima kubwa ambayo spika wa bunge Anne Makinda amempa mbunge huyo
kwa kumteua kuwa miongoni mwa wabunge wachache vijana kwenda nje ya
Tanzania kushiriki mkutano mkuu wa dunia wa wabunge vijana.
|
No comments:
Post a Comment