Afisa mahusiano wa chuo cha Kikuu cha Iringa, Agness Kitundu akimpaa maelekezo mlinzi wakati wa mahafali ya chuo hicho.
WAHITIMU |
WAHITIMU |
WAHITIMU |
WAHITIMU |
WAHITIUMU |
WAHITIMU |
WAHITIMU |
WAHITIMU |
WAHITIMU |
WAHITIMU |
WAHITIMU |
HOTUBA YA MAKAMU
MKUU WA CHUO PROF. NICHOLAS T. A. BANGU KWENYE MAHAFALI YA KWANZA
YA
CHUO KIKUU CHA
IRINGA
TAREHE 25 OKTOBA
2014
1.
UFUNGUZI
Mheshimiwa Mkuu wa
Chuo, Mh. Judge Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani,
Mwenyekiti wa Baraza
la Chuo Kikuu cha Iringa, Bishop Dr. O. Mdegela,
Wakuu wa Serikali na Taasisi mbalimbali,
Wafanyakazi wa Chuo,
Wanafunzi mliohitimu,
Wanafunzi mnaoendelea,
Wageni Waalikwa,
Mabibi na Mabwana.
2.
KUKARIBISHA WAGENI:
Awali
ya yote kwa heshima na taadhima naungana na Mwenyekiti wa Baraza kuwakaribisha
katika mahafali haya ya kwanza ya Chuo Kikuu cha Iringa kuwashukuru kwa
kuhudhuria.
3.
PONGEZI:
Natoa
pongezi kwa wanakamati ya maandalizi walioongozwa na Bwana Aloyce Suleiman na
wengine waliohusika kwa namna mbalimbali kukamilisha maandalizi.
Nawapongeza
wafanyakazi wote (wanataaluma na waendeshaji) kwa ujumla na kwa mmoja mmoja kwa
kazi nzuri waliyoifanya katika kipindi cha mwaka 2013/14 na kutufikisha kuwa na
mahafali ya kwanza.
Nawapongeza
wahitimu wote kwa kufikia hatua hiyo. Ni
dhahiri kuwepo kwenu hapa chuoni kumechangia kuwajenga kielimu, na ninaamini
kumechangia kuwajenga kiroho na kimaadili na kuwa mtatumia nyenzo hizo zote
kuchangia katika juhudi za kitaifa za kuboresha hali ya maisha ya Watanzania na
walimwengu wote kwa ujumla.
4.
SHUKURANI
Katika kipindi cha
mafunzo 2013/2014 wafuatao ni baadhi ya waliotufadhili kwa hali na/au mali:
·
Wazazi/walezi wa wanafunzi,
·
Serikali ya Tanzania
kupitia taasisi yake ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB),
·
Serikali ya Umoja wa Ulaya,
·
Serikali ya Finland,
·
Serikali ya Uholanzi kupitia Shirika lake la NUFFIC,
·
Chuo Kikuu cha Nelson Mandela,
·
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kupitia
LMC,
·
Shirikisho la Kilutheri la Amerika (ELCA): kupitia Synod ya Eneo la Mt. Paul (St. Paul ares Synod),
·
Uongozi wa ngazi mbali mbali za Mkoa wa Iringa
5. MATUKIO-
KIPEKEE MWAKA WA MASOMO 2013/2014
5.1.
Mradi wa Hifadhi ya Utamaduni, Utalii na Maendeleo endelevu
Kanda ya Kusini mwa Tanzania
(Cultural Heritage conservation, Tourism and Sustainable Development in
Southern Highlands of Tanzania.
5.1.1
Mradi huu unafadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya (EU)
5.1.2
Katika Utekelezaji tuna washirika 8 na baadhi yao ni Chuo Kikuu cha
Cottingen Ujerumani, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ofisi ya Manispaa ya
Iringa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Iringa.
5.1.3
Shughuli zilizofanyika mwaka huu zimo katika makundi
matano:
5.1.3.1
Utafiti na uchoraji ramani.
5.1.3.2
Maandalizi ya upatikanaji Boma la Kijerumani toka
Serikalini na mipango ya ukarabati.
5.1.3.3
Maandalizi ya kibiashara utamaduni na promotion
5.1.3.4
Kuhusisha wananchi katika biashara ya utalii wa utamaduni
5.1.3.5
Kwa kushirikiana na vyuo vya Ujerumani, Finland
kujenga uwezo wa kitaaluma: vijana 9 wamepata ufadhili kwa ngazi ya Masters
(M.A) na 1 kwa digrii ya falsafa (Ph.D) lengo ni kufanya utafiti wa utalii wa
utamaduni kuwa moja ya agenda ya Chuo cha Iringa.
5.2.
Kuelekea kuwa Chuo Kikuu cha Kizazi cha Tatu (SGU) kizazi hiki
kinatofautina na vizazi viwili vya awali kwa kufanya ujasiliamali kuwa sehemu
ya taaluma. Tendo la kuingiza ujasiliamali linaenda kwa hatua:
5.2.1.
Kuelimisha waalimu na wanafunzi nafasi ya ujasiliamali
katika taaluma.
5.2.2.
Kubadili mfumo wa ufundishaji kuwa mwanafunzi ndio kitovu
cha kujenga elimu na pili kuhamasisha tambuzi zote sita za ubongo; kukumbuka
(remembering), kuelewa (understanding), kuchambua (analyzing), kuchanganya
(synthesizing), kutumia (Application) na kubuni (Creating)
5.3.
Kuwahamasisha wanafunzi kuanzisha makapuni ya kuzalisha mali wakingali
choni kwa maana hiyo kuelekeza mafunzo wanayoyapata kwenye kampuni wanaoijenga.
Hadi sasa shughuli kadhaa zimeanzishwa na zinaendelezwa na wanafunzi
waliohitimu. Kwa mfano SAMIS inafanya shughuli za supermarkets na PESSI
inayoshughulika na kuzungusha plastics na kadhalika.
Hatua ya nne
ambayo imeanza mwaka huu ni kuimarisha uundaji wa kampuni kutumia nadhania
inayoitwa Team Academy. Mwaka huu wa masomo tuna
wanafunzi 40 ambao watafanya masomo yao kwa
utaratibu huo sambamba na mafunzo ya kawaida na kuanzia mwakani mfumo wa masomo
yao utakuwa
unaelekea kwenye kampuni ambazo wameamua kuziunda na kuziendeleza.
Mafunzo ya namna
hii yalizinduliwa huko Finland.
Mwaka 1993 na hivi sasa umesambaa katika nchi kadhaa duniani Netherlands
Hungary Argentina hususani Finland, France, UK, Spain, China, Brazil,
Austelia). Kwa Africa chuo chetu kitakuwa cha kwanza. Juzi nilipata fursa ya
kuelezea mfumo huu kwenye Mkutano wa NEPAD. Wajumbe wengi walifurahia na chuo
cha Africa Zimbabwe na Jomo Kenyata wametukarisha tukawaeleze zaidi.
5.4.
Kitengo cha Kilimo (Institution of Agriculture) na kitengo
cha mitaji midogo (Inst. Of Microfinance) vimepata ufadhili wa Kitengo cha America
kinachoitwa Iringa Hope USA ufadhili wa Jengo litakalokuwa na vyumba vya ofisi
na vyumba vya mijadala ya wakulima kuhusu stadi za kilimo na fedha.
5.5.
Kitengo cha Marekani cha ubadilishaji wa elimu kimefungua
tawi katika Chuo cha Iringa. Kwa mwaka huu tawi lilipokea wanafunzi 5 mwezi wa
Januari na mwezi huu hivi sasa wameongezeka hadi 20. Kila kundi limekuwa hapa
kwa miezi mitatu na wanajifunza mambo mbali mbali. Matumaini yetu ni kwamba
wanafunzi wetu wataweza kwenda katika vyuo huko Marekani.
6. WAHITIMU:
Mheshimiwa Kaimu Mkuu
wa Chuo,
Katika mwaka 2013/2014
jumla ya wanafunzi 2228 wanahitimu kwa mchanganuo ufuatao:
1.
|
Astashahada ya Theolojia (Certificate in
Theology)
|
20
|
2.
|
Stashahada ya Theolojia (Diploma in
Theology)
|
12
|
3.
|
Shahada ya Kwanza
ya Tauhidi (Degree of Bachelor of Divinity –
(BD)
|
5
|
4.
|
Astashahada ya Ushauri Nasihi
(Certificate in Counseling Psychology)
|
7
|
5.
|
Stashahada ya Ushauri Nasihi (Diploma in
Counseling Psychology)
|
40
|
6.
|
Shahada ya Kwanza
ya Ushauri Nasihi (Degree of Bachelor of Counselling (BCOUNS)
|
37
|
7.
|
Astashahada ya Utawala na Biashara
(Certificate in Business Administration – CBA)
|
125
|
8.
|
Astashada ya Ununuzi na Usimaminzi wa Mali
(Certificate in Procurement and Material Management)
|
24
|
9.
|
Stashahada ya Utawala na Biashara
(Diploma in Business Administration)
|
353
|
10.
|
Stashahada ya Sayansi katika Uhasibu na
Fedha (Diploma in Accounting and Finance)
|
23
|
11.
|
Stashahada ya Ununuzi na Usimaminzi wa Mali (Diploma
in Procurement and Material Management)
|
40
|
12.
|
Shahada ya Kwanza
ya Sayansi katika Uhasibu na Fedha (Bachelor of Science in Accounting and
Finance - BAF )
|
39
|
13.
|
Shahada ya Kwanza
ya Uchumi na Fedha (Degree of Bachelor of Science in Economics and Finance)
|
34
|
14.
|
Shahada ya Kwanza
ya Utawala wa Biashara (Degree of Bachelor of Business Administration)
|
88
|
15.
|
Astashahada ya Sheria (Certificate in
Law)
|
52
|
16.
|
Stashahada ya Sheria (Diploma in Law)
|
33
|
17.
|
Shahada ya Kwanza
ya Sheria (Bachelor in Law
|
166
|
18.
|
Astashahada ya Sanaa ya Maendeleo ya
Jamii (Certificate in Community Development
|
65
|
19.
|
Stashahada ya Sanaa ya Maendeleo ya
Jamii (Diploma in Community Development)
|
48
|
20.
|
Shahada ya Kwanza
ya Sanaa ya Maendeleo ya Jamii (Bachelor of Arts in Community Development)
|
198
|
21.
|
Shahada ya Kwanza
ya Anthropolojia ya Utamaduni na Utalii (Bachelor of Arts in Cultural
Anthropology and Tourism)
|
94
|
22.
|
Astashahada ya Sanaa ya Uwanahabari
(Certificate in Arts in Journalism)
|
7
|
23.
|
Stashahada ya Sanaa ya Uwanahabari
(Diploma in Arts in Journalism)
|
6
|
24.
|
Shahada ya Kwanza
ya Sanaa ya Uwanahabari (Bachelor of Arts in Journalism)
|
68
|
25.
|
Astashahada ya Sayansi na Teknolojia ya
Habari (Certificate in Information Technology)
|
62
|
26.
|
Stashahada ya Sayansi na Teknolojia ya
Habari (Diploma in Information Technology)
|
36
|
27.
|
Shahada ya Kwanza
ya Sayansi katika Teknolojia ya Habari (Degree of Bachelor of Science in
Information Technology)
|
43
|
28.
|
Shahada ya Kwanza
ya Elimu katika Hisabati (Bachelor of Education Mathematics)
|
58
|
29.
|
Shahada ya Kwanza
ya Elimu katika ….. (Bachelor of Education – Arts)
|
274
|
30.
|
Stashahada ya Uzamili ya Elimu Ualimu
(Postgraduate Diploma in Education – Teaching)
|
26
|
31.
|
Shahada ya Uzamili ya Sanaa ya Maendeleo
ya Jamii na Usimamizi wa Miradi (Master of Arts in Community Development and
Project Management)
|
38
|
32.
|
Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika
Saikolojia (Master of Science in Counseling Psychology)
|
2
|
33.
|
Shahada ya Uzamili ya Elimu – Sanaa
(Master of Education – Arts)
|
3
|
34.
|
Shahada ya Uzamili ya Sheria katika
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Master of Law in Information and
Communication Technology Law
|
15
|
35.
|
Shahada ya Uzamili katika Mfumo wa
Sheria za Jinai za Kimataifa na Haki za Binadamu (Master of Laws in
International Criminal Justice and Human Rights (LLM-ICJ-HR)
|
9
|
36.
|
Shahada ya Uzamili ya Anthropolojia ya
Utamaduni na Utalii (Master of Arts in Tourism, Culture and Society)
|
6
|
37.
|
Shahada ya Uzamili ya Utawala na
Biashara (Master in Business Administration)
|
72
|
JUMLA
|
2228
|
Prof. NICHOLAUS . T. A. Bangu
VICE CHANCELLOR
No comments:
Post a Comment