Reyhaneh Jabbari
mwenye umri wa miaka 26 amehukumiwa kunyongwa baada ya kukutwa na hatia
ya kumuua mtu mmoja ambaye alifanya jaribio la kumbaka.
Taarifa iliyoripotiwa na CNN inasema
mwanamke huyo amenyongwa katika gereza la Tehrain, Iran ambapo alikuwa
amefungwa baada ya kutenda kosa hilo mwaka 2007 wakati huo akiwa na umri
wa miaka 19.
Mwanamke huyo
amekutwa na hatia hiyo kutokana na kosa la kumuua aliyekuwa mfanyakazi
wa wizara ya ulinzi na usalama nchini Iran, Morteza Abdolali.
Shirika la kimataifa la haki za binadamu Amnesty International limelaani
kitendo cha Iran kutoa hukumu hiyo, ambapo mbali na jitihada ya kampeni
mbali mbali zilizofanywa ikiwemo zile za kwenye mitandao ya kijamii
katika kuipinga hukumu hiyo kuonekana kutozaa matunda.
Taarifa kutoka
nchini humo zinasema mahakama ilitoa hukumu hiyo baada ya kutojiridhisha
na utetezi alioutoa mahakamani kwamba alitenda kosa hilo akiwa
anajilinda.
Utafiti wa Umoja
wa Mataifa wa mwaka 2011 unaonesha Iran ni moja ya nchi zinazoongoza
kwa ukiukwaji wa haki za binadamu ambapo nchi hiyo ina wastani wa kutoa
hukumu ya kunyongwa mtu 1 kila baada ya masaa 8.
No comments:
Post a Comment