Stori: Gladness Mallya
MSANII wa muziki na filamu Bongo, Baby Madaha ambaye
anadaiwa kuishi kinyumba na meneja wake Mkenya, Joe Kariuki wa Kampuni
ya Candy n Candy Records, ametoa mpya baada ya kudai kuwa kutokana na
kusubiri kwa muda mrefu ili apate mwanaume anayefaa kwa ajili ya kumuoa
bila mafanikio, sasa ameamua kuwapanga foleni bila kujali idadi yao.
Akipiga stori na gazeti hili juzikati, Baby Madaha alisema amesubiri
sana kuolewa lakini hajamuona mwanaume anayefaa, hivyo ameamua kuwapanga
kama mafungu ya nyanya kama wao wanavyowapanga wanawake na ikitokea
mmoja ‘akamzingua’ anaachana naye na kumchukua mwingine.
“Mimi sasa hivi nawapanga tu wanaume maana sioni anayenioa ndiyo
maana nimechukua uamuzi huu, wanaume wamezoea kutupanga sisi wanawake
sasa mimi ndiyo nimewageuzia kibao nao waone utamu wake na ikitokea huyu
amenizingua namuacha nahamia kwa mwingine,”alisema Baby Madaha.
No comments:
Post a Comment