Sehemu ya watu waliojitokeza katika mkutano huo |
Wakionesha ishara ya chama chao |
CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimelitaka jeshi la Polisi
kudhibiti misafara mirefu ya magari na pikipiki, na aina yoyote ya
maandamano wakati wa mapokezi ya katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi
(CCM) Abdulahman Kinana wakati wa ziara yake mkoani Iringa .
Kauli
ya Chadema imekuja ikiwa ni siku takriba tatu kabla ya kuwasili
Kinana Oktoba 6-11 mwaka huu kuanzia ziara yake mkoani Iringa
Kwa
mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari zilizotolewa na CCM mkoa
Kinana ataambatana na Katibu Itikadi na Uenezi wa chama hicho Nnape
Nauye wanatarajia kufanya ziara ya kukijenga chama hicho na kukagua
utekelezaji wa Ilani ya CCM katika wilaya zote za mkoa wa Iringa wakati
wa ziara hiyo.
Akiwahutubia
juzi wananchi wa kata ya Kihesa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la
Chadema (BAVICHA) Patrick Ole Sosopi alisema wamesikitishwa na jeshi
la polisi kuzuia mapokezi yake mkoani Iringa huku wakitambua wazi kuwa
ni haki ya wanachama kumpokea kiongozi wao ila polisi waligoma
kutoa kibali zaidi ya kuruhusu mkutano wa hadhara pekee.
Akiwa na Makamu Mwenyekiti Bavicha, Patrick Ole Sosopi |
Alisema
wakati wakijiandaa kuchukua Dola wanataka kuona wanashindana katika
uwanja sawa wa kisiasa kwahiyo hawatakubali kuona jashi la Polisi
linaruhusu maandamano katika misafara ya Kinana wakati kwao linakataa.
Sosopi
aliyekuwa na Mchungaji Peter Msigwa wakitokea jijini Dar es Salaam
kulikofanyika chaguzi mbalimbali za kitaifa za chama hicho, walipokelewa
katika eneo la Igumbilo na viongozi wachache wa chama hicho baada ya
Polisi kudaiwa kuwazuia wafuasi wao kuwapokea kwa misafara ya magari,
bodaboda na maandamano.
“Tumetii
maelekezo ya Polisi, vijana wetu wa bodaboda wamezuiwa kutupokea; ili
haki itendekea tunataka Kinana na timu yake watakapoingia mjini Iringa,
misafara yao isiwe na maandamano ya watu, pikipiki wala magari,” alisema
Mchungaji Msigwa katika mkutano wao mkubwa uliofanyika katika kata ya
Kihesa mjini Iringa.
Mchungaji
Msigwa alisema watashangaa na kuchukua hatua endapo Polisi itairuhusu
CCM kuwa na maandamano na misafara ya magari na pikipiki.
No comments:
Post a Comment