Stori: Mwandishi Wetu
IMEFICHUKA!
Madai ya Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Geita, Vicky Paschal
Kamata kuwatumia meseji za kashfa wabunge wenzake, Lucy Thomas Mayenga
(CCM) na Catherine Valentine Magige (UVCCM)Mkoa wa Arusha sasa mambo
hadharani.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, wabunge hao warembo wako katika vita
baridi ikiendeshwa chini kwa chini kwa Cathy (pichani) na Lucy kudai
kwamba wamekuwa wakitumiwa meseji zenye kejeli na kashfa nzito kutoka
kwa mheshimiwa Vicky.
KUNA SABABU?
Kwa mujibu wa chanzo chetu, licha
ya sababu kutokuwa wazi sana, lakini madai ni kwamba wana bifu
linalokimbilia mwezi wa nne sasa.
“Unajua si rahisi wao kuweka wazi
bifu lao, lakini wenyewe watakuwa wanajua nini kiini, ukifuatilia
utagundua kuwa maisha yao yamekuwa ni ya vikundivikundi, akina Lucy wana
kundi lao na Vicky ana la kwake,” kilisema chanzo hicho.
KWA NINI VICKY?
Chanzo kiliendelea kuanika
kwamba, baada ya meseji zinazodaiwa kukosa staha kutumwa na
asiyejulikana kwenda kwenye simu za mkononi za Cathy na Lucy,
waheshimiwa hao hawakupembua sana mchele, moja kwa moja wanadaiwa
kumtaja hasimu wao kwenye vyombo vya dola kuwa huenda anahusika na
‘utundu’ huo.
POLISI WAFUATILIA MINARA YA SIMU
Duru za
kipolisi zinadai kuwa kufuatia waheshimiwa hao kumlalamikia Vicky, wana
usalama hao walianza kuchunguza mawasiliano yake ambapo walibaini mambo
makuu mawili.
KWANZA, baadhi ya meseji hizo zilionesha kutumwa kwa
kupitia mnara wa simu uliopo maeneo ya bunge. PILI, kuna meseji
iliwezeshwa kusafiri kwa nguvu ya mnara uliopo eneo linaloitwa Uwanja wa
Ndege ambapo inadaiwa Mheshimiwa Vicky ndiko anakoishi.
SERIAL NUMBER
Pia yapo madai kwamba, polisi hao
walikwenda kitaalam zaidi na kubaini kwa kutumika namba zilizomo ndani
ya simu eneo la kuwekea betri (serial number) ambazo zilionesha kuwa,
laini iliyokuwa ikituma meseji za kuudhi kwa waheshimiwa hao pia imekuwa
ikutumia na laini ambayo polisi walimjua mhusika, ingawa wasemaji wake
wamesita kuthibitisha.
POLISI NYUMBANI KWA VICKY
Habari zaidi zinadai
kuwa, Jumanne iliyopita, polisi mkoani Dodoma walifika nyumbani kwa
mheshimiwa Vicky na kufanya uchunguzi kama wanaweza kupata simu yenye
laini iliyoripotiwa na akina Mayenga (pichani) kwamba imekuwa
ikiwakashifu kwa meseji lakini hawakufanikiwa kukuta chochote.
Alipotafutwa Vicky ili kujua undani wa meseji hiyo juzi, simu yake
haikuwa hewani. Kwa upande wake Lucy ambaye alidai kutumiwa meseji za
matusi katika gazeti moja (siyo la Global), naye simu yake iliita bila
majibu, huku Cathy akishindwa kupatikana na kulifanya gazeti hili kuzidi
kuchimba kwa kina sakata hili ili kupata mbivu na mbichi na kuzianika
bila kusitasita.
No comments:
Post a Comment