Monday, 13 October 2014

MBEYA::NDENJELA AZINDUA MABASI MAPYA YA KISASA NDENJELA JET.


MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akikata utepe kuzindua mabasi ya kisasa ya kampuni ya Mwaji Group  jijini Mbeya


Ndani ya mabasi ya Ndenjela jet


MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro pamoja na Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Ahamed Msangi wakifurahia maelezo mafupi toka kwa Mkurugenzi mtendaji    wa Mwaji Group Allan Mwaigaga

MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akiongea na wananchi waliohudhuria sherehe hizo za uzinduzi wa mabasi ya kisasa

 Mkurugenzi mtendaji    wa Mwaji Group Allan Mwaigaga
akiwashukuru wageni waalikwa kwa kuhudhuri sherehe ya uzinduzi wa mabasi yake ya kisasa

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Ahamed Msangi akitoa neno la shukrani na kusisitiza madereva kuwa makini barabarani na kuzingatia alama zote za barabarani

Moja ya wafanyabiashara wakubwa mkoani mbeya anaejulikana kwa jina la TUGHIMBE akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wafanyabiashara wa mkoa wa Mbeya kuwa kumuunga mkono wenzao kwa kusafiri na mabasi ya Ndenjela jet

Kaimu meya wa jiji la Mbeya Fungo akimshukuru mkuu wa mkoa mbeya kwa hotuba yake nzuri aliyoitoa katika uzinduzi wa mabasi hayo

Baadhi ya wananchi waliohudhuria sherehe hiyo ya uzinduzi wa mabasi hayo


Awilo akitumbuiza katika uzinduzi wa mabasi hayo


Dereva wa kike Nusura akionyesha umahili wake wauendeshaji wa Basi hilo la Ndenjela Jet huku pembeni Mwandishi wa Mbeya yetu Joseph Mwaisango akishangaa
MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akimpongeza Dereva wa kike Nusura Maguliko mara baada ya kumwona akiendesha moja ya mabasi aliyoyazindua

Kondakta wa basi la  Ndenjela jet akisoma risala mbeya ya mgeni rasmi

Mtaalamu wa mitambo ya magari hayo, Joshua Mshanga, alisema vifaa vilivyofungwa kwenye magari hayo vinasaidia kupunguza ajali zinazotokana na ulevi, mwendokasi na kuyapita magari mengine sehemu za hatari.






MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, amewataka vijana kutokuchagua aina ya kazi bali kufanya kila jambo ili mradi wanaisaidia serikali katika kupambana na upungufu wa ajira nchini.
Kandoro alisema Serikali inatengeneza mazingira wezeshi kwa kila mtu kupata ajira na sio kumpa ajira kila mtu hivyo kwa anayetoa ajira kwa mtanzania mwenzake anachangia kutekeleza malengo ya serikalio ya kuhakikisha ajira zinapatikana.
Hayo aliyasema wakati akizindua magari ya kisasa ya Kampuni ya   Mabasi yafanyayo safari zake kati ya Mikao ya Mbeya, Rukwa na Dar Es salaam ya Ndenjela Jet katika hafla iliyofanyika Uyole kwenye ofisi ya kampuni hiyo jijini Mbeya.
Kandoro alizungumza hayo kufuatia mmiliki wa mabasi hayo, Allan Mwaigaga kuajiri zaidi ya watu 50 huku akizingatia haki sawa kwa kuwa na wanawake sawa na wanaume katika ofisi yake na kuwa na dereva wa kike anayeendesha moja ya mabasi yake.
Alisema kuna umuhimu wa watu hususani vijana wa kike kutokubagua aina ya kazi na ajira jambo litakalosaidia Serikali kuondokana na wimbi la upungufu wa ajira kwa wananchi unaolikabili taifa.
Alisema Ndenjela ni mfano wa kuigwa kwa kuwa ameweza kuajiri vijana bila kubagua jinsia ikiwa ni pamoja na kutekeleza maazimio ya Raisi ya kuhakikisha na toa ajira sawa kwa wanawake na wanaume yaani 50 kwa 50.
“ ndugu zangu tuige mfano wa huyu mmiliki wa haya mabasi kutoa ajira kwa watanzania wenzetu kwani kazi ya serikali sio kuajiri kila mtu bali ni kutengeneza mazingira wezeshi kama alivyofanya Mwaigaga kwa kuajiri watanzania zaidi ya 50 bila kubagua” alisema Kandoro.
Kwa upande wake mmiliki wa mabasi hayo, Allani Mwaigaga, ambaye pia ni Mkurugenzi mtendaji wa Mwaji group workshop, alisema amelazimika kubuni magari ya kisasa kulingana na mahitaji ya watanzania yenye lengo kubwa la kyupunguza ajali nchini.
Alisema magari yake yataweza kuwa mfano hapa nchini kwa kupungiuza ajali kwa kiwango kikubwa kutokana na kufungiwa kifaa maalumu ambacho kitakuwa kikiyaongoza magari hayo pamoja na dereva anayeendesha na kutoa taarifa kama atakiuka sheria za usalama barabarani.
Alisema magari hayo yamefungiwa mtandao wa WIFI ambapo kila gari litakuwa likiongozwa na watu wanne akiwemo Dereva hivyo watuwengine watakuwa wakibaki Mbeya katika chumba maalumu wakifuatilia mwenendo wa gari kila hatua linapokuwa likisafiri.
Naye mtaalamu wa mitambo ya magari hayo, Joshua Mshanga, alisema vifaa vilivyofungwa kwenye magari hayo vinasaidia kupunguza ajali zinazotokana na ulevi, mwendokasi na kuyapita magari mengine sehemu za hatari.
Alisema kifaa cha GPS kilichofungwa kwenye magari hayo kinawezesha aliyekuwa kwenye chumba cha kuongozea magari kujua gari lilipo, kama dereva anayeendesha ni mlevi, spidi ambayo gari linatembea au dereva akienda tofauti na alikopangiwa ambapo kifaa hicho hutuma taarifa haraka na kutoa hatua ambazo zinapaswa kuchukuliwa kwa wakati huo.
Mwisho.

                            Na Mbeya yetu

No comments:

Post a Comment