Katika kuenzi Nyerere Day kwa vitendo Mbunge wa Jimbo la Musoma
Mjini (CHADEMA) Vicent Nyerere, amejenga choo chenye matundu 8 katika
kijiji cha Bumangi, ambapo anataraji kukabidhi kwa serikali ya kijiji
mara baada ya kukamilika kwa ujenzi huo.
Kijiji hicho ambacho
kipo kata ya Muriaza Wilaya ya Butiama mkoa Wa Mara, wananchi wamekuwa
wakijisaidia porini kwa muda mrefu sasa.
Nyerere alisema kuwa gharama kubwa ilitarajiwa kutumika katika ujenzi
wa choo hicho lakini hadi hivi sasa, gharama inayotarajiwa kutumika ni
shilingi millioni 3 kwa kuwa wanachama wa Chama Demokrasia na
Maendeleo(CHADEMA) wamejitolea kufanya kibarua bila malipo.
"Tumejenga Choo kijiji jirani cha Bumangi soko ili wananchi wapate kujisaidia kuliko kwenda porini" Alisema Nyerere
Hata hivyo alisema kuwa Choo hicho kitakabidhiwa kwenye serikali ya kijiji mara baada ya kukamilika ujenzi kwa ajili ya utunzaji.
Aliongeza kuwa soko la bumangi hufanyika Mara moja kwa wiki na linahudumia zaidi ya vijijini 37 hivyo wananchi hukumbana na adha kubwa kwa kujisaisaidia porini kutokana na kutokuwa na choo.
Nyerere ametoa wito kwa wakazi wa maeneo ya Bumangi kutumia choo hicho kwa usafi na kukitunza ili kiweze kudumu kwa muda mrefu.
Alisema Maliwato/choo ni sehemu muhimu sana katika eneo lolote linalotumiwa na binadamu na ni sehemu inayohitaji usafi wa hali ya juu sana ili kuepukana na magonjwa ya milipuko.

No comments:
Post a Comment