Mabaki
ya mwili yaliyokutwa katika eneo la kijiji cha Lupapila wilaya
ya songea mkoani Ruvuma yakikusanywa na wataalamu kutoka hospital ya
mkoa
wa Ruvuma.
MIFUPA ya masalia ya
binadamu wa jinsia ya kiume ambaye hakuweza kufahamika jina na
kukadiriwa kuwa na miaka (30) yamegundulika na Zaujia Pilly (70) mkazi
wa kijiji cha Lupapila wilaya ya songea mkoani Ruvuma
Ruvuma wakati akienda kuchimba dawa za kienyeji baada ya kuwaona mbwa wakishambulia sehemu za mabaki hayo.
Ruvuma wakati akienda kuchimba dawa za kienyeji baada ya kuwaona mbwa wakishambulia sehemu za mabaki hayo.
Kamanda wa polisi mkoa wa
Ruvuma Mihayo Msikhela alisema kuwa tukio hilo limetokea oktoba 26 mwaka
huu majira ya saa 9:45 alasiri huko katika kijiji cha Lupapilamtaa wa
Mahinya kata ya Subira nje kidogo ya manispaa ya Songea.
Alisema kuwa inadaiwa siku
hiyo ya tukio kwenye msitu wa uwanja wandege ilikutwa mifupa ya binadamu
wa jinsia ya kiume ikiwemo fuvu la Kichwa, Mbavu, Mikono na Miguu
wakati sehemu ya kiuno na mapaja ikiwa imeharibika vibaya.
Alifafanua kuwa mabaki ya
mwili huo yaligunduliwa na Zaujia Pilly wakati akienda kuchimba dawa za
kienyeji kwenye msitu huo ghafla aliwaona Mbwa wakifukuzana kugombania
mabaki ya mwili wa binadamu.
Alieleza zaidi kuwa Zaujia
baada ya kugundua tukio hilo alitoa taarifa katika uongozi wa serikali
ya Mtaa na kisha taarifa zilipelekwa katika kituo kikuu cha polisi cha
songea mjini ambako baadaye polisi walifika eneo la tukio wakiwa
wameongozana na Daktari kutoka hospitgali ya Mkoa wa Ruvuma ambaye
aliyafanyia uchunguzi mabaki ya mwili huo na kubaini kuwa marehemu
alikuwa amepigwa na kitu kizito kichwani kwenye eneo la kisogo
kilichopelekea kifo chake.
Kamanda Msikhela alisema kuwa kufuatia tukio hilo hakuna mtu yeyote anayehusishwa na jeshi la polisi mkoani Ruvuma linaendelea kufanya chunguzi wa kina juu ya kifo hicho.
Na Amon Mtega -Songea
No comments:
Post a Comment