Mtandao
wa Watezi wa Haki za Binadamu (THRDC) umefuatilia kwa karibu mchakato wa kupata
katiba mpya unaondelea Bungeni, mjini
Dodoma na kuona ya kwamba mchakato huu
umegubikwa na mambo mengi yenye kuashiria ukiukwaji wa haki za wajumbe
wa Bunge hilo. Mchakato wa kupiga kura
ya NDIO au HAPANA kwenye rasimu ya katiba inayopendekezwa umezua vitisho na ‘sintofahamu’ nyingi dhidi ya wajumbe walio
piga kura ya HAPANA.
Mtandao
wa Watetezi kama Sauti ya watetezi wote nchini Tanzania imepokea taarifa
zenye kusikitisha kutoka kwa baadhi ya wajumbe wanaounda Bunge Maalumu la
Katiba kuwa wabunge waliopiga kura za HAPANA
zenye kuashiria kukataa katiba
inayopendekezwa wamelalamika na kukiri kuwa maisha yao yapo hatarini Mjini
Dodoma. Mtandao unalaani vitendo hivyo pamoja na wote wanaohusika na vitisho
hivyo dhidi ya wajumbe hao wa Bunge la Katiba.
Mtandao
baada ya kuwasililina na wajumbe hao umebaini kuwa wanaotishwa ni
miongoni mwa wajumbe watokanao na kundi la 201 hasa upande wa Zanzibar ambao
wamesisitiza kwamba maisha yao yapo hatarini na wanaishi kwa wasiwasi huku
wengine wakifanya mipango ya kuondoka upesi katika Mkoa huo ambao bunge
linaendeshwa.
Kwa
mujibu wa maelezo yao, inaonekana kuwa toka
walipo piga kura za wazi za HAPANA baadhi ya wabunge na hata mawaziri wamekuwa wakiwatishia maisha
kwa kuwa wametekeleza haki yao ya kupiga kura ambazo hazikuwafurahisha
watawala. Miongoni mwa wajumbe waliopiga
kura za hapana na waliopokea vitisho
hivyo baada ya kupiga kura ya ‘HAPANA’ ni:
1.
Salma
Said- Asasi zisizo za Kiraia (AZAKI)
2.
Ali
Omary
3.
Adil
Mohammed- Chama cha Walemavu Zanzibar
4.
Fatma
Mohamed- Taasisi za Kidini
5.
Jamila
Abeid- Vyama vya Siasa
6.
Dr
Alley Nasor- Vyuo Vikuu Zanzibar
7.
Mwanaid
Othman
Vitisho
vivyo vilianza baada ya Mwenyekiti kuhofu kutopata idadi ya theluthi mbili
kutoka Zanzibar. Wajumbe hawa kwa sasa wanahishi kwa ofu kubwa na mashinikizo
makubwa toka kwa baadhi ya watawala na
wajumbe waliopo katika Bunge hilo la
kuwataka wabadili msimamo wao. Mashinikizo hayo ni pamoja na tendo la kura za
hapana kuundiwa kamati ya kuzijadli bila kujulikana lengo lake ni nini hasa,
kwani kura ikishapigwa hairudiwi tena.
WITO WETU
Tunapenda
kuwakumbusha Wajumbe na Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba kuwa Katiba Bora inatokana na maridhiano na kwa kuheshimu
mchakato na si kwa mabavu au nguvu ya dola.
1. Kila
mtu anahaki ya kutoa maoni yake binafsi na kupiga kura bila kulazimishwa
achague nini.
2. Sheria
ya mabadiliko ya katiba inatakiwa kufuatwa
ili kuepusha nchi kuingia kwenye machafuko.
3. Tuna
msihi kiongozi wa Bunge Maalumu la Katiba kufuata misingi ya utawala bora, haki
za binadamu, na demokrasia anapoliendesha Bunge hilo.
4. Mtandao
unawasihi wajumbe wote wa Bunge Maalum la Katiba kuacha kuwadhalisha na
kuwanyanyapaa wale ambao wataonekana wakipiga kura za HAPANA, kwani lengo la kuwepo kwa zoezi la
upigaji kura lilikuwa linatambua uwepo wa kura za NDIYO na HAPANA.
5. Tunalisihi
jeshi la polisi kutimiza dhamana yake ya kulinda raia na mali zao kwa kuhakikisha
hatua muhimu zinachukuliwa kutokana na vitisho walivyopokea baadhi ya Wajube Maalumu wa Bunge la Katiba.
6. Tunawasihi
wajumbe wote waliopo mjini Dodoma kwenda kuripoti katika vyombo vya usalama
pamoja na kutoa taarifa kwa THRDC endapo wataona mazingira yoyote ya
kuhatarisha maisha yao.
No comments:
Post a Comment