Na Mwandishi wetu
MKURUGENZI
wa Kampuni ya Lino International Agency, Hashim Lundenga, amekanusha
uvumi uliosambaa kwenye mitandao ya kijamii mapema leo, kuwa Sitti Abbas
Mtemvu (pichani katikati) amelazimika kuvua taji la Uremo la Tanzania
(Redd’s Miss Tanzania 2014).Uvumi
wa Sitti kuvua taji hilo umetokana na taarifa zilizotolewa kupitia
akaunti ya Facebook mrembo huyo anayelalamikiwa kughushi vyeti vya
kuzaliwa, akisema kutokana na vidole vya lawama anavyooshewa kiasi cha
kuosa amani, amelazimika kuvua taji ili awe huru.
“Habari
za jioni Watanzania wenzangu, kutokana na kuwa nimekuwa nikisemwa sana,
maneno mengi yasio na tija juu ya hili taji la U-Miss anzania
2014,,mpaka kupelekea nisiwe na amani na uhuru ndani ya nchi yangu
Tanzania, kwa roho safi nimeamua mwenyewe kujivua taji hilo na kuacha
wanaye ona anastahili taji hili apewe ili niendelee na maisha yangu kwa
amani ,isiwe shida sana kwani sitegemei taji hili ili kuishi!!”
imeandikwa katika ukurasa huo.
Akizungumzia
uvumi huo, Lundenga alisema hakuna ukweli juu ya taarifa hiyo, na
kwamba kama lingekuwa na ukweli ni wazi kwamba Sitti angeiarifu kampuni
yake, inayoratibu kinyang’anyiro hicho kilichotimiza miaka 20 mwaka huu.
“Hakuna
taarifa iliyotufikia hadi sasa kuhusiana na taarifa hizo. Sitti anajua
anapaswa kufanya nini kama anaamua kulitema taji, ambapo anapaswa
kutuarifu sisi kabla ya kuripoti hilo mahali popote. Kwa kuwa hajafanya
hivyo, tunaamini hilo halipo nab ado tunamtambua kuwa mrembo wetu,”
alisema Lundenga.
Kwa
upande wa mama wa mrembo huyo, alisema ameshtushwa na taarifa za mwanaye
kujiuzulu na kusema si za kweli, kwani kama angepanga kufanya hivyo
asingefanya kwa kificho, badala yake angeitisha mkutao na wanahabari:
“Hawezi kujiuzulu kienyeji hivyo na hata mimi mama yake sina taarifa
hizo, hayo ni matumizi mabaya ya mitandao.
No comments:
Post a Comment