Sunday 17 August 2014

HILI NDO DONGO LA MASANJA kwa DIAMOND NA WEMA

Soma alichoandika Masanja Mkandamizaji kuhusu uhusiano wa Wema na Diamond
WEMA
Masanja mkandamizaji mchekeshaji kutoka kundi la Komedi Orijino kupitia ukurasa wake wa instagram ameandika mawazo yake juu ya uhusiano wa Wema Sepetu na Diamond.
Hiki ndicho alichoandika,”Hili swala la diamond na wema nadhani mungu amemuhurumia mmoja wapo kati ya hao wawili. Kama wangekuwa watu wa kuoana wangesha oana uchumba gani mrefu kama wanasomea udokta????
Rafiki yangu nasib, kama kweli mlipendana kwa dhati hizo kasoro zinarekebishika, maana hakuna mwanadamu aliye sahihi kwan hata ww nasib unamapungufu yako. Na wewe dada yangu wema lazima ujue mme ndio kichwa cha nyumba kwa maelezo hayo inaonyesha haumsikilizagi mwenzio omba msamaha tenaaa na tena na ukubali kubadilika.
Mi sipendi mkiwa mnaongozana wote kwenye ma show ya usiku mme kafanye kazi mke abaki home ukirudi mwili umepoa hata ujauzito unaingiaa!! Sasa woote stejini mkirudi miili ya moto si mtazaa popompoo jamaniii!! Nitafurahi kusikia tofauti zenu mmezimaliza kwa amani ili mashabiki wenu wasijisikie vibaya.