Friday, August 29, 2014
KERO ZA BARABARA: MBEYA YETU YAMULIKIA BARABARA YA VETA , AMBAPO KUNA VIONGOZI WA KUBWA WA SERIKALI WANAISHI HUKO PAMOJA NA CHUO CHA MAFUNZO YA UFUNDI STADI VETA.
Hii
ni moja ya Kero ya kakipande kadogo sana na korofi ambako wananchi
wanaoishi eneo hili wamelalamika sana na kudai kuwa hakuna anayesaidia
kwa njia zozote..
Mbeya
yetu baada ya kupata taarifa hizo iliona ni vema na haki kutembelea
eneo hilo na kujionea wenyewe ambapo mpaka sasa wenye magari
wamelazimika kuikimbia barabara hiyo kutokana na kuchakaa vibaya kwa
njia hiyo
hata
hivyo baadhi ya wakazi wamelalamika sana kuwa njia hiyo hasa hako
kakipande kadogo kamekuwa kero kubwa na kusababisha hata mataili yao ya
magari kuharibika, kuisha na kuyabadilisha kila wakati
Pia
Mbeya yetu ilibaini wazi kuwa kuna Chuo cha ufundi stadi cha veta na
hii ikiwa ni moja ya njia kuu na ambapo katika Chuo hicho kuna zaidi ya
wanafunzi Elfu mbili sasa swali likaja je hawa wanafunzi hakuna
waliosomea Fani ya ukandarasi hata waje kumwaga kifusi na kuziba mashimo
hayo?
Na
kubwa zaidi katika eneo la barabara hiyo kuna viongozi wakubwa wa
Serikali wanaishi huko akiwemo Mkuu wa Majeshi Tanzania, Waziri Asiye na
Wizara Maalum, Aliyekuwa naibu Waziri wa Elimu, Viongozi wa wa Mkoa,
Pamoja na Watu wenye uwezo na Baadhi yao pia wameikimbia barabara hii.
Zifuatazo ni picha za Baadhi ya maeneo ambayo Tochi yetu imemulikia kwa umakini.
Hiki
ndicho kipande cha barabara hiyo ambapo ndipo inapoanzia kwa kutazama
unaweza ukasema ni salama lakini ukiangalia kulia kwako utagundua kama
kuna shimo lililofunikwa na udongo, Eneo hilo ni mashimo ukipita vibaya
unaweza acha tairi zako za Gari
Haya
ni Mawe yaliyochongoka , wengi wamepatwa na pancha katika eneo hili na
kusababisha wahame njia hiyo hata kama wanaishi jirani na maeneo hayo.
Eneo hili ni kucheza Sindimba tuu
Hakuna Unafuu hata kidogo
Kwanza kabisa kwa vumbi hili hapa ni hatari sana pia barabara kipande hiki inazidi kuwa mbaya zaidi
Hapa huwezi hata kwepa ni lazima utapita tuu na kupita kwake lazima utasababisha majanga na chombo chako cha usafiri
SWALI ... JIJI MPO? JE MMEKUONA NA HUKO.. KAMA BADO PITIENI MTAZAME
No comments:
Post a Comment