Marekani yalaani vita nchini Libya
26 Agosti, 2014
Maafisa nchini Marekani wanasema
Misri na umoja wa falme za kiarabu zilihusika na mashambulio nchini
Libya katika wiki iliyopita kuwalenga wanamgambo wa kiislamu
wanaokabiliana na vikosi vya serikali.
Afisa mmoja mkuu wa Marekani ameiambia BBC kwamba Marekani haikushirikishwa katika mashambulio hayo na ilishangazwa.Misiri imekana tuhuma hizo na hapajakuwa na tamko lolote kutoka kwa Umoja wa falme za kiarabu.
Marekani na washirika wake wanne wa Ulaya zimeshutumu wanachokitaja kama usumbufu wa kutoka nje nchini Libya. Ufaransa, Ujerumani, Italia, Uingereza na Marekani zimelaani vikali mpigano na ghasia nchini Libya.
Nchi hizo zimesema zinarudia wito wao, zikiungana na ule wa serikali ya muda ya Libya, Baraza la Wawakilishi na wananchi wa Libya, kwamba pande zote nchini Libya zikubaliane na usitishaji wa vita mara moja na kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kisiasa, kujizuia na mipango inayoweza kudhoofisha hatua hiyo.
No comments:
Post a Comment