Ofisi ya Bunge yatoa ufafanuzi kuhusu malipo ya posho za Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba.
Mkurugenzi
wa Habari na Itifaki, Bw. Jossey Mwakasyuka (kushoto) akitoa
ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na
malipo ya posho za Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba leo katika
ukumbi wa mikutano ofisi ya Bunge mjini Dodoma.
Baadhi ya
waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wakisikiliza kjwa
makini maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Habari na Itifaki, Bw. Jossey
Mwakasyuka wakati alipofanya mkutano na waandishi hao kwa lengo la
kutolea ufafanuzi kuhusiana na malipo ya posho za Wajumbe wa Bunge
Maalum la Katiba leo katika ukumbi wa mikutano ofisi ya Bunge mjini
Dodoma.
OFISI
ya Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma, imetoa
ufafanuzi juu ya taarifa zilizotolewa kwenye vyombo vya habari kuhusu
kuchelewa
kwa malipo ya posho za Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba.
Ufafanuzi
huo umetolewa leo na Mkurugenzi wa Habari na
Itifaki Bw. Jossey Mwakasiyuka wakati alopokutana na waandishi wa habari
kwa
lengo la kutolea ufafanuzi kuhusiana na taarifa hizo zilizoikera ofisi
hiyo ya
Bunge Maalum.
Mwakasyuka
amevieleza vyombo vya habari kuwa, ofisi ya Bunge
Maalum imekerwa na kuchapishwa kwa taarifa hizo na baadhi ya vyombo vya
habari
kwani taarifa hizo ni za upotoshaji na zina lengo la kuwadhalilisha
Waheshimiwa
Wajumbe na kuwafanya waonekane wenye kuishi na kufanya kazi kwa
kutegemea posho
wanazolipwa.
“Ni
vema ikaeleweka kwamba Wajumbe wa Bunge Maalum wote ni
watu wenye nafasi zao katika jamii na ni wenye kazi au shughuli zao
mahususi
zinazowaingizia kipato na kwamba Ujumbe wa Bunge Maalum ni nafasi ya
muda tu ya
kutimiza jukumu la kuliandalia taifa Katiba Mpya”. Alisema Mwakasyuka.
Mwakasyuka
ameongeza kuwa, si vema kwa vyombo vya habari
kuwadhalilisha Wajumbe hao kwa njia yoyote ile kwani kwa kufanya hivyo
kunawavunja moyo na kuwafanya washindwe kuifanya kazi ya Bunge Maalum
vizuri
kama ilivyotarajiwa na wananchi.
Akifafanua
kuhusiana na malipo ya posho hizo, Mkurugenzi
Mwakasyuka ameviambia vyombo vya habari kuwa, Wajumbe wote wa Bunge
Maalum
ambao wanahudhuria vikao vinavyoendelea wamekwishalipwa posho zao zote
kama
wanavyostahili.
“Ni
vyema ikaeleweka kwamba malipo ya posho yanafuata
taratibu za fedha za umma na yanapita kwenye mchakato maalum
unaojumuisha
kupata orodha za mahudhurio ya Wajumbe kwenye kikao, upatikanaji wa
fedha toka
Hazina, na upatikanaji wa fedha toka Benki, hivyo wakati mwingine
huchukua siku
kadhaa hadi kukamilika.” Alifafanua Mwakasyuka.
Aidha,
Mwakasyuka amevitahadharisha vyombo vya habari vinavyondika habari za Bunge
Maalum
kuzingatia maadili na kanuni za Uandishi wa habari zinazotolewa katika
vikao
vya Bunge Maalum ili taarifa kama hizo za upotoshaji zisijirudie tena.
“Kumbukeni
kuwa wajibu wenu ni kuhabarisha umma na sio
kupotosha umma na hata kuleta usumbufu kwa jamii kutokana na uandishi
usio
makini”. Alionya Mwakasyuka.
Katika
kanuni za Bunge Maalum, kanuni ya 77 inawataka
waaandishi wa habari kuandika habari za Bunge Maalum kwa weledi mkubwa
kwa
kuzingatia maadili ya uandishi wa Habari ili kuondoa uandishi wenye
kuleta
chuki kati ya Serikali na Wananchi wake kwani kinyume na kanuni hiyo,
Katibu
anaweza wakati wowote kuondoa ruhusa aliyotoa kwa mwakilishi wa chombo
chochote
cha habari iwapo chombo hicho kitatoa taarifa yoyote kuhusu shughuli za
Bunge
Maalum ambayo kwa maoni ya Bunge Maalum inapotosha ukweli au vinginevyo
inakiuka kanuni, taratibu au haki za Bunge Maalum.
na fredy mgunda
No comments:
Post a Comment