Tuesday, 26 August 2014

NA WAPIGWE TU:Baada ya Pinda Kutangaza Nia ya Urais, Wanzazibari Wasema Hawamtaki Kwani Alisema Zanzibar Sio Nchi

Baada ya Pinda Kutangaza Nia ya Urais, Wanzazibari Wasema Hawamtaki Kwani Alisema Zanzibar Sio Nchi

Tuesday, August 26, 2014
Zanzibar. Madai ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuingia katika kinyang’anyiro cha urais yameibua mjadala mkali kutoka kwa baadhi ya wanasiasa, wasomi na wananchi wa Zanzibar ambao wamesema hafai kutokana na kauli yake kuwa ‘Zanzibar si nchi’.

Wakizungumzia uamuzi huo ulioripotiwa na vyombo vya habari juzi, baadhi ya wananchi hao wamempinga na wengine kumuunga mkono.

Aliyekuwa mgombea mwenza wa TLP katika Uchaguzi Mkuu 2010, Abdallah Othman Mgaza alisema Pinda anaponzwa na kauli yake kuwa Zanzibar si nchi... “Zanzibar ni nchi kamili ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kutojua kwake akasema si nchi na kuwakera Wazanzibari. Anapoteza muda wake bure kwa kufikiria urais wa Muungano, sehemu moja ya dola hawana imani naye.”
.

Mkurugenzi wa Uenezi, Habari na Mawasiliano kwa Umma wa CUF, Salum Abdallah Bimani alisema chama hicho kimepata mshangao kusikia Pinda akitaka kuwamo katika orodha ya wanaojitaja kuwania urais wa Muungano wakati upande mmoja wa Muungano bado una kinyongo naye kwa matamshi yake yaliyodai Zanzibar si nchi.

“Ndugu zetu CCM Zanzibar wana kawaida ya kutotusikiliza na kutubeza, kwa hili tunawaomba chondechonde wafungue masikio yao, akiwa waziri mkuu alisema Zanzibar si nchi, akipata urais ataitangaza nchi yetu mkoa na kutuletea gavana mkaazi,” alisema Bimani.

No comments:

Post a Comment