Sunday 17 August 2014

JE,HII NDO NGUVU YA MWANAMKE KATIKA NDOA...?

Ndoa Nyingi za Kizazi Hiki Zinavunjika Kwa Sababu za Kijinga, Nguvu ya Mwanamke Katika Ndoa

Written By Udaku Specially on Sunday, August 17, 2014 
POWER OF A WOMAN IN MAKING THE MARRIAGE WORK!

1st Lesson SOMETIMES A WOMAN WINS BY LOOSING! Unaweza mwanamke ukajiona umepoteza kitu ila in reality umeshinda! Na unaweza kuona umeshinda ila in reality umepoteza. Usiendekeze hisia za moyo zinavokuongoza na wapambe! Tumia akili na busara zaidi! Mfano unapewa data mumeo yuko guest kafumanie, kuliko kwenda na kumuita shigongo kuvunja utu wako na wa mumeo na kutia doa maisha yenu shukuru tu taarifaa, mpe mumeo benefit of the doubt sali kwa Mungu wako. Kuchapiwa ni siri ya ndani indeed! Usimchunguze mumeo kama CIA au KGB sababu ukitafuta sanaa kitu utakipataaa! Manake wanawake kuna tabia unamfatilia una withold eveidence hiku unaikusanya hadi uhakikishe siku ukimsomea mashtaka hana pakutokea ushahidi unatosha kuconvict. Hahahaaaaaa!

2nd Lesson! BY NATURE MARRIAGE IS SELF DESTRUCTORY, LOOK FOR SOLN TO MAKE IT WORK! Yaani nature yenyewe mambo ya kumkinai mwenzio, kutamani vipya, ni natural tu, hayahitaki hata sababu, sasa baada ya kuwa mtu wa lawama, kulaani kwanini mambo kama hayo yawatokee, kumuona mwenzio hana shukrani, spend more time kudeal na situation kuliko mwenzio. Kama uzazi umekubongesha work out, acha kula hivo. Kuliko kudemand the impossible kuwa sababu umemzalia akupende hivo hivo kwenye jimwili jipya sio rahisi. Shirikiana kutafuta soln.

3rd Lesson USISAHAU HATA SIKU MOJA AT A POINT LIFE YOU WERE HIS NUMBER ONE NDO MAANA AKAKUOA! Hata kama anakunyanyasa saivi, heshima haipo, anachepuka, labda wewe upo number 100 saivi not even once dont let you forget once upon a time you were his number 1, he married you, yes you na mapungufu yote yako, not Lily the cutest, mima the big as.s, Rose the beauty queen etc, wote aliwaona yet still akakuona wewe ugly betty or whatever! Tatizo ni kujisahau, wakati anakuoa you might have been ugly still lakini una heshima, upo humble, etc sasa umo ndani ndo unajifanya king kong atakwambia nini si ushindani hamna! Ukiona mambo magumu rudi back in the days ujiulize ulimloga vipi wakati ule umloge tena!

4th Lesson UTAMALIZA MABUCHA NYAMA NI ILE ILE! Unakuta mtu unamuacha mumeo kisa muhuni ana michepuko? Mwanaume gani asie na michepuko? Hahahaaa! Utamuacha wa kwanza utatafuta 2, wembe ule ule, utahangaika mpaka basi! Kabla hujamuacha mumeo kisa michepuko jiulize nani hachepuki utaempata? Au mimeo hela hana! Hata unaemkuta nazo zaweza kusiha vile vile. Tulia vumilia unyolewe. Wenzio wote wametulia wewe unajilegeza! Ifike mahala fumba macho uombe Mungu siku ziende maana hata ukisema uende kwingine mwendo ule ule! Unamuacha mumeo unaanza kuiba wa wenzio! Akili matope hayo?

5th Lesson KABLA HUJAPANIC KWA JAMBO MOJA KUMBUKA MEMA YAKE ELFU MOJA NDO UAMUE KUHUSU HIKO KIMOJA! Mtu kakuoa miaka 5, anakupa yote utakayo, anakiabudu malkia wake, hakuna unachokosa, shabash kateleza kidogo shetani kampitia sisi wote binadamu kakusoea kachepuka one time! Basi wewe. Unasahau mema yoooooote ya 5 years huko kumshika ndo unafunga mabegi na kutokomea! Khaaaaa! Au mmeishi vizuri miak 7, mwaka huu ndo kabadilika, japo uvumilie na kuomba atambue makosa na kujirudi miaka yote 7 watia kwenye dustbin, unashupalia matendo yake mwaka huu na kudai talaka! Sasa na mwanaume mda mwengine nae anakereka anaona kama wema wake wa miaka 7 sio issue basi nendaa tu! Power of love sio kufaidi goodtimes ni kuhimili mikimikiki! Wapambe nuksi kina lara 1 tunakutia ndimu ondoka bwanaa, kwanini afanye hivo, ndo unakole kweli kweli. Usiruhusu tendo moja la kijinga likupotezee 7 yrs of your life n hard work! Kwani ukisamehe hilo fumanizi utababuka? Vitakuuma vitapoa mnaanza upya! Hatoki mtu inaitwa! Atafanya visa wee akikuona mkomavu atachoka mwenyewe!

6th lesson! JIFUNZE KULET THINGS GO! Sio basi ukimfumania mara moja kila akikosea kidogo unamshikia kooni ile ugoni wa mwaka juzi. Kitu kidogo unaretrieve file! Au ulimsaidia mwaka juzi alipokwama, akikunyima hela kidogo unakumbushia, mwaka juzi fyoko fyoko! Daaah! Sio issue. Inatakiwa uwe mkomavu ukisema umesamehe kitu basi ndo unakizika kooni forever! Haukitaji tena! Unamuepusha shaitwani kukaa kati kati yenu kila wakati! Unavomsamehe mara nyingi inaondoa hata ile ladha ya kukusoea tena! Sababu anajua utamsamehe na wala hutomuuliza tenaaa! Mwenyewe anajistukia. Ananza kuona kweli huyu si binadamu wa kawaida, labda namtendea ndivo sivo.

7th lesson! MUME NAE BINADAMU LOLOTE LINAWEZEKANA! Usiwe na expectations kubwa sanaaaaaa! Ukamuona yule malaika labda hawezi kukosa. Aaaaah! Wapi! Jua tu yule binadamu kupitiwa inawezekana pia, na hata akipitiwa unajua umejipanga kusort hizo issue out kuendeleza libeneke! Ila kama ndo ulikuwa unamuona mungu mtu, siku akiteleza waweza kuga kwa pressure! Wakati cha ajabu hamnaa mbona! Kwani ye wa kwanza kufanya hivo? Au wa mwisho? Hamnaaaaa!

By Lara 1