Gari lililobeba Maiti Kumi za Mafunzo Laua Wawili Mikese
Gari la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), lililokuwa likisafirisha
maiti 10 za watu kwenda katika Hospitali ya Mtakatifu Francis Ifakara,
wilayani Kilombero, limewagonga watu wawili waliofariki dunia papohapo,
eneo la Mtego wa Simba, Mikese mkoani Morogoro.
Waliokufa katika ajali hiyo iliyotokea saa 5:25 asubuhi jana ni dereva na abiria wa bodaboda.
Maiti hizo zilizokuwa zimehifadhiwa katika mifuko maalumu ya plastiki, zinaelezwa kuwa zilikuwa zikipelekwa katika Hospitali ya Mtakatifu Francis, ili zitumike kwa mafunzo.
Akizungumzia ajali hiyo katika eneo la tukio, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Morogoro, Boniface Mbao alisema kuwa gari hilo lilikuwa likiendeshwa na Pankrasi Pascal, mkazi wa Ifakara, wilayani Kilombero.
Mbao aliwataja waliokufa kuwa ni Shaaban Rajabu na Ally Benulo, wakazi wa Kijiji cha Mikese, waliokuwa wamepakizana kwenye pikipiki.
Tukio hilo limekuja siku kadhaa baada ya mabaki ya miili ya binadamu kugunduliwa ikiwa imetupwa katika dampo moja lililoko Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam