Sunday 17 August 2014

KUPITA peter msigwa 2015 IRINGA MJIN NI NDOTO....ONA UONGO WA CCM

CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM )MKOANI IRINGA KIMEWEKA WAZI KAZI WALIZOZIFANYA KWA KUWA WAO NDIO WALIOLETA MAENDELEO YA MANISPAA YA IRINGA NA SIO MBUNGE WA JMBO HII MCH:PETER MSIGWA



Akihutubia wananchi wa mkoani iringa katika soko la kuu la manispaa ya iringa meya wa manispaa ya iringa AMANI MWAMWINDI alisema kuwa yeye ndiye anaye saini mikataba yote inayoleta maendeleo katka jimbo hili na sio kweli kama amabavyo mbunge wa jimbo hili peter msigwa kuwa maendeleo ya manispaa ya iringa.

MWAMWINDI kwa kuyaongelea maeneo ambayo serikali imeyafanyia kazi na yameleta maendelo katika manispaa ni pamoja na kutengeneza barabara zote kwa njia ya rami na kukalabati zile zote zilizokuwa zinahitajika kukalabatiwa kwa lengo la kuleta maendeleo katika manispaa.

pia MWAMWINDI alisema iringa inafanya vizuri upande wa elimu na usafi kwa kuwa wamejipanga toka zamani kwa kamati mabalimbali zilizokuwa zinakuja kukagua usafi katika maeneo ya manispaa wamekuwa wakiisifia kwa kuwa kila mwaka wanafanya mabadiliko ya kimaendeleo.
naye  katibu wa chama cha mapinduzi mkoani iringa HASANI MTENGA alimtaka mkurugezi kumuondoa halaka afisa SUMATRA KONDO kwa kuwa amekuwa akiwanyanyasa madereva wa daladala.bodaboda na bajaji hivyo hafai kuwa kiongozi kwakuwa anafanya kazi kwa faida yake mwenyewe.