Monday 18 August 2014

MAREKAN KAMA BONGO TUI:GAVANA AWAAMURU POLISI KUTUMIA MABOMU

Missouri kuwatumia National Guard

 18 Agosti, 2014 

Missouri kuwatumia National Guard kuzima ghasia
Jimbo la Missouri Marekani limeamua kuwatumia maafisa wa kitengo maalum cha National Guard'' ilikuzima maandamano ambayo yamekuwa yakiendelea mjini Fergusson kwa muda sasa tangu auawe kijana mmoja mwenye asili ya Kiafrika na polisi wa mji huo.
Gavana wa jimbo hilo Jay Nixon alitia sahihi amri ya kuwatumia kitengo hicho maalum kinachutumika tu wakati wa Vita na majanga ilikukabili utovu wa usalama katika jimbo hilo la Ferguson.
Maandamano yamezidi kwenye mji huo wa Ferguson, licha ya kuwepo kwa amri ya kutotoka nje ambayo imekiukwa kwa usiku wa pili mfululizo.
Missouri kuwatumia National Guard kuzima ghasia
Polisi katika jimbo hilo wamelazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi na risasi za raba ilikukabiliana na wenyeji waliokasirishwa na mauaji ya kijana mmoja ambaye anashukiwa kuwa alikuwa ni mwizi wa kimabavu.
Maafisa wa polisi wa Ferguson, katika kitongoji cha St Louis, walisema walishambuliwa na hawakuwa na “na jinsi mbadala” ila kujibu tu.
Cpt Ron Johnson anayeongoza operesheni hiyo huko Ferguson anasema kuwa waandamanaji waliwatupia mabomu ya kujitengenezea pamoja na chupa zaidi ya saa tatu kabla ya marufuku ya kutotoka nje kuanza rasmi.
Kitengo maalum cha National Guard kutumiwa Missouri
Mauji ya kijana huyo Michael Brown ambaye alikuwa amehitimu shule ya upili na ambaye alipigwa risasi na askari mzungu imetibua kovu la ubaguzi wa rangi katika karne ya 21.
Uchunguzi wa kwanza wa mwili wake unaonesha kuwa kijana huyo alipigwa risasi mara sita ikiwemo risasi mbili zilizoingia kichwani kulingana na ripoti ya New York Times.
Mkuu wa sheria nchini Marekani Eric Holder ameagiza uchunguzi kufanyika upya kwa mwili ya mwendazake.