Tuesday 2 September 2014

KWA MSAADA WA MUUMBA TU>>VITA DHIDI YA EBOLA YASHINDIKANA...

MSF:Vita dhidi ya Ebola vinashindikana

 2 Septemba, 2014
Nchini DRC watu 31 wamefariki kutokana na Ebola
Rais wa shirika la kimataifa la madaktari wasio na mipaka, MSF Juliana Liu, ameambia mkutano wa umoja wa mataifa kuwa vita dhidi ya ugonjwa wa Ebola katika kanda ya Afrika Magharibi vinashindikana.
Akiongea mjini New York, alisema kuwa miezi sita tangu kuzuka kwa ugonjwa huo nchini Guinea, Liberia na Sierra Leone, jamii ya kimataifa imeshindwa kukabiliana na tisho la kuenea kwa ugonjwa huo.
Zaidi ya watu 1500 wamefariki kutokana na ugonjwa huo katika kanda ya Afrika Magharibi katika mlipuko mbaya zaidi wa ugonjwa huo kuwahi kuripotiwa tangu kugunduliwa kwake katika kanda ya Afrika ya kati karibu miaka 40 iliyopita.
Wakati huohuo kuna hofu kwamba, mlipuko wa Ebola unatishia mavuno ya wakulima mashambani katika kanda ya Afrika Magharibi.
Shirika la kimataifa la chakula na kilimo limeelezea wasiwasi kuhusu hali ya chakula nchini Liberia, Sierra Leone na Guinea, nchi tatu ambazo ziliathirika zaidi kutokana na Ebola.
Shirika hilo limesema mavuno ya Mchele na Mahindi yataathirika zaidi katika msimu huu unaokuja.
Upungufu wa chakula unatabiriwa kuwa mbaya zaidi katika miezi michache ijayo.

No comments:

Post a Comment