Msanii wa Bongo fleva aliyetamba na hits Song kibao Q chillah amefunguka na kusema kuwa ameacha kweli kutumia madawa ya kulevya na kamwe hawezi kurudia tena maana madawa hayo yalimfanya kuwa na maisha ya ajabu,kama kuona kila mtu ni adui yake,kutokuwa na amani Q Chillah amefunguka hayo leo alipokuwa akichat Live katika ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipengele cha Kikaangoni Live kinachofanywa kila siku ya Jumatano kuanzia saa sita mchana.
Q Chillah amesema toka ameeacha kutumia madawa hayo ya kulevya kwa sasa ni mwaka wa tatu hivyo anawashauri vijana kutojaribu wala kushawishika kuingia katika matumizi ya dawa za kulevya hivyo wanapaswa kujitambua na kutambua dhamani yao kama vijana na kujua kuwa taifa linawategemea hivyo wakiingia katika matumizi ya dawa za kulevya watashindwa kutimiza ndoto zao nyingi na kuharibikiwa kimaisha.
Mbali na kuzungumzia juu ya matumiz ya dawa za kulevya pia Q Chillah ameweka wazi mikakati yake ya kurudi tena katika game la Bongo Fleva na kuweza kushika hatamu katika muziki huo kutokana na uwezo wake katika muziki,hivyo amenza kwa kuachia wimbo wake mpya alioufanya na msanii Mb dogy,wimbo huo ambao leo umetambulishwa katika kipindi cha Power Jams ya East Africa Radio unakwenda kwa jina la Nipende Nikupende.
Ni kweli nilikuwa kimya katika muziki kutokana na matatizo ya hapa na pale hivyo sikuacha muziki bali nilianguka kimuziki lakini leo ndio nimerudi rasmi katika game na nimetambulisha wimbo mpya niliofanya na Mb Dogy hivyo mashabiki zangu kaeni mkao wa kula sasa.
SIJAROGWA NA DIAMOND ILA NAMKUBALI
Q Chillah amefunguka na kusema kuwa baadhi ya vyombo vya habari na waandishi walimkariri vibaya ila hajarogwa na msanii yoyote yule na nyota ya msanii Diamond kwa sasa imewaka kwake ndio maana anafanya vizuri maana mwenyezi mungu ndiye kamfungulia njia ya yeye kuweza kuwika na kufanya vizuri kwa sasa na hakuna uchawi kama amabvyo baadhi ya watu wanavyosema.
"Hapana sikweli Diamond hanirogi bali Mungu kamfungulia njia na daima nitasapoti kazi za wenzangu,tukumbuke kuwa mchawi Mungu binaadam njia tu namkubali Diamond kama ambavyo watu wenginewanavyomkubali"
Baadhi ya waandishi wa habari wamekurupuka na hizo habari ila mimi siamini saaana nyota,naamini katika uwezo wa mtu sababu bila uwezo binafsi nyota haiwezi onekana hata kidogo,hivyo hata Diamond ameonyesha uwezo wake binafsi ndio maana ameweza kufungua njia na kufika mbele zaidi kimuziki ila siamini uchawi namwamini mungu.
No comments:
Post a Comment