Friday 10 October 2014

MAUAJI IRINGA::JESHI MKOANI IRINGA LINAMSHIKILIA NGAGA KWA KUMPIGA RISASI RAFIKI YAKE



NA FRIDAY SIMBAYA, IRINGA
Jeshi la polisi mkoani Iringa linamshikilia Gwerino Ngaga (70) mkazi wa Mbigili kwa kosa la kumpiga risasi  kifuani Thadei Mbugu(40) mkazi wa Mbigili  na kusababishia kifo chake papo hapo.


Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi akielezea tukio hilo la kinyama kwa waandishi wa habari ofisini kwakw leo alisema kuwa limetokea Oktoba 9 majira ya saa moja za jioni  katika kijiji chaMbigili kata ya Lugalo tarafa ya mazombe wilaya ya kilolo mkoani hapa.


Kamanda Mungi alisema kuwa awali kabla ya tukio marehemu pamoja na mtuhumiwa wakiwa na wakezao walikuwa wakinywa pombe  za kienyeji katika kilabu kinachoendeshwa na mke wa Gwerino.


Mungi alisema kuwa sababu kubwa ya  mtuhimiwa kumpiga risasi marehemu Thadei lilitokea mara baada ya mke wa mtuhumiwa kumuomba pesa marehemu mbele ya mkwewe na mumewe kitendo kile kilimuudhi mtushtakiwa  na  kuamua kuenda nyumbani kuchukua bunduki aina ya shortgun na kumpiga  kifuani hali iliyopelekea kupoteza maisha. 

‘’Hawa jamaa walikuwa wote na wake zao wakipata kinywaji sasa wakati wanakunywa huyu mke wa mtuhumiwa alimuomba marehemu ampe hela ya  kutumia na mke wa  wa marehemu aliposikia mumewe akiombwa hela alifoka kwa nguvu kwa kulaani kitendo cha mumewe kumhonga mke wa mtu hela tena kilabuni huku angali akiwa na mumewe’’
“Sasa mume wa yule mke aliposikia mkewe anapewa hela na marehemu alimuuliza kisa cha kumdhalilisha kwa kumpa mkewe hela mbele yake ndipo marehemu akamjibu kwa dharau kuwa amezeeka na hivyo hana hela hivyo anamsaadia kumlea kitendo kilichomuudhi mstakiwa na kumlipua kwa bunduki yake,”  alisema Mungi.




Mtuhumiwa huyo anashikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi wa karibu ili kubaini nini chanzo hasa kilichosababisha mtuhumiwa kuchukua bunduki na kumpiga mwenzie kwani hapo awali kulikuwa hakuna ugomvi wowote na wote walikuwa ni majirani wanaokaa mtaa moja .


Mungi alieleza kuwa  baada ya kufanya uchunguzi wa awali walibaini kuwa bunduki hiyo  aina ya shotgun iliyotumika katika mauaji hayo  inamilikiwa kihalali na Gwarino Ngaga mkazi wa Mbigili.

No comments:

Post a Comment