Wednesday, 20 August 2014

TUKIO NA PICHA:5,000/= YAPOTEZA UHAI WA MTU IRINGA MJIN.

TUKIO KATIKA PICHA: MTU MMOJA AUAWA PAPO HAPO KWA KUCHOMWA NA KISU KISA WALIKUWA WANADAIANA TSH 5,000, KITUO CHA MABASI IRINGA

 Tunaomba Radhi kwa picha.
 Tukio tulilopokea muda mchache uliopita mtu mmoja ambaye jina lake halijafahamika amemuua mwenzake kisa walikuwa wanaiana Shilingi Elfu tano... Tunaendelea kufuatilia tukio zaidi .. endekea kufuatilia hapa hapa.
 Kijana huyo ambaye jina halijafahamika akiwa amefariki baada ya Kuchomwa kisu na mwenzake kisa madai ya Tsh 5000 tuu
Mamia ya watu wakiwa wanashuhudia tukio hilo.
Picha na Iringa yetu Blog

Agness Masogange Aingizwa Mkenge na Mnigeria na Kuikana Nchi Yake

Agness Masogange Aingizwa Mkenge na Mnigeria na Kuikana Nchi Yake

Udaku Specially on Wednesday, August 20, 2014
Stori: Sifael Paul na Imelda Mtema

Habari ya mjini kwenye ulimwengu wa mastaa Bongo ni taarifa kuwa video queen maarufu, Agness Gerald ‘Masogange’ amepatiwa passport (pasipoti) ya kuishi nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ na mwanaume anayedaiwa kuwa ni mfanyabiashara raia wa Nigeria.

MWANAUME KAMWINGIZA MKENGE?
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika, ishu hiyo ambayo imekuja miezi kadhaa baada ya ule msala wa Masogange wa madawa ya kulevya ‘unga’ inadaiwa ‘imeinjiniwa’ na mwanaume huyo ambaye haijajulikana kama naye amechukua uraia wa Sauzi au la.

KWA NINI MKENGE?
Ilisemekana kwamba ni mkenge kwa sababu ili Masogange apate pasipoti hiyo, ilibidi aikane nchi yake ya kuzaliwa ya Tanzania. Sheria za uraia wa Bongo kwa sasa zinakataza mtu kuwa na uraia wa nchi mbili.

KIKAZI ZAIDI!
Awali, miezi kadhaa iliyopita ilielezwa kuwa Masogange alitimka Sauzi kwa mwanaume huyo ambaye anadaiwa kufanya naye ‘kazi’ (haikutajwa aina ya kazi) nchini humo.
Miezi kadhaa iliyopita Masogange alionyesha kuukataa kabisa Utanzania, baada ya kuandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram kuwa kuanzia sasa hataitwa tena Agness, bali umma umtambue kama Thando, jina lenye asili ya watu wa taifa hilo kubwa zaidi kiuchumi barani Afrika.

Pia Masogange alitupia mtandaoni picha ya hati yake ya kusafiria ya Sauzi akidai kwamba maskani yake kwa sasa ni kwenye Jiji la Johannesburg nchini humo.Kitendo hicho kinamfanya Masogange ambaye ana asili ya Mkoa wa Mbeya, kuingia nchini kwa viza kama wageni wa mataifa mengine wanavyofanya, wakipewa muda walioomba wa kukaa au kufanya shughuli nyingine yoyote.

Kana kwamba haitoshi, endapo msichana huyo atakumbwa na kosa lolote la kisheria akiwa nchini, anaweza kufukuzwa na kutakiwa kutokuja tena, kama inavyotokea kwa wageni wengine na hivyo kumnyima fursa ya kuwaona wajomba na mashangazi zake walio Mahenge, Kondoa, Mkuranga na maeneo mengine Tanzania.

SHERIA INASEMAJE?
Kwa mujibu wa sheria za Kibongo, Tanzania hairuhusu uraia wa nchi mbili (duo citizenship) hivyo Masogange au Thando siyo Mtanzania tena.

MBALI NA MNIGERIA KUNA MSAUZI
Habari ziliendelea kuyeya kwamba mbali na Mnigeria huku, Masogange anadaiwa kuwa na mwanaume mwingine, raia wa Sauzi aitwaye Louis Dolnard ‘anayeminya’ naye nchini humo.
Kwenye Mtandao wa Instagram, mwanadada huyo amekuwa akitupia picha za mahaba niue na mwanaume huyo huku akidaiwa kumsifia jamaa huyo na kumpotezea aliyekuwa mchumba’ke, Evance Komu.

MASOGANGE ANASEMA?
Akizungumza na gazeti hili, Masogange anayeishi Mbezi-Beach jijini Dar, mara baada ya kukamilisha taratibu za pasipoti hiyo kwenye ubalozi wa Afrika Kusini nchini, mrembo huyo alikiri kukamilisha kila kitu hivyo kukwaa uraia wa nchi hiyo.

Kuhusu mwanaume huyo Mnigeria, Masogange hakuwa tayari kuzungumzia lakini alipoulizwa juu ya yule Msauzi, video queen huyo alikiri kumfahamu huku akigoma kufunguka zaidi.

TUMEFIKAJE HAPA?
Miezi kadhaa iliyopita, Masogange na mwenzake Melissa Edward walikamatwa nchini Afrika Kusini wakiwa na matirio ya kutengenezea madawa ya kulevya aina ya Crystal Methamphetamine ya Sh. bilioni 6.8 ambapo katika hukumu ya kesi hiyo, staa huyo alitakiwa kulipa faini ya randi 30,000 (Sh. milioni 4.8 za Bongo) au kifungo cha miaka 2 jela. Yeye alilipa faini hiyo akaachiwa huru. 


MENINAH: NAOGOPA MAPENZI YATAVURUGA MUZIKI WANGU

MENINAH: NAOGOPA MAPENZI YATAVURUGA MUZIKI WANGU

Mwimbaji wa Bongo Flava aliyewahi kuwa mshiriki wa BSS, Meninah Ladivah akifanya mahojiano katika kipindi cha Hatua Tatu leo.
Meninah akiwa studio na mtangazaji anayeongoza kipindi cha Hatua Tatu, Times Fm, Maryam Kitosi.
Mwimbaji wa Bongo Flava aliyewahi kuwa mshiriki wa BSS, Meninah  amesema anaogopa kuwa katika uhusiano wa mapenzi kwa sasa anaamini mapenzi yatavuruga muziki wake.

Akiongea katika kipindi cha Hatua Tatu cha 100.5 Times Fm, Meninah ameeleza kuwa hivi sasa yuko single na hajawa na mpango wa kuingia katika uhusiano kutokana na sababu hizo.

“Kwa sasa niko Single naangalia kazi yangu kwanza... Nikiingia kwenye mahusiano kazi yangu itakuwa shaghala bagala.” Amesema Meninah.

Hivi karibuni kulikuwa na tetesi kuwa mwimbaji huyo ana ukaribu na Diamond lakini alikanusha na kueleza kuwa hajawahi hata kuwa na ukaribu na mkali huyo.

Unaweza kuwa umeshasikia na unaamini Meninah yuko kwenye uhusiano na….. Lakini msikilize pia yeye. “Unajua watu wanaamini ukiwa msichana mzuri basi ni lazima uwe katika uhusiano!”

Meninah ameachia wimbo mpya unaoitwa ‘Pipi ya Kijiti’.

KILA SIKU MAPENZI YA DIAMOND NA WEMA TUUUUUU!!!!!!DUH,JISOMEE

Maneno ya Diamond Kwa Wema Kuwa na Marefiki Wapenda Starehe Yamchoma Vikali Aunt Ezekiel

Udaku Specially 
Star wa filamu nchini Aunty Ezekiel anadaiwa kuchomwa vilivyo na maneno ya Diamond kwa Wema Sepetu yanayodaiwa kumgusa yeye pia moja kwa moja kama rafiki wa Wema…

Diamond juzi alisema  kuwa Wema anapenda sana starehe na mashoga wapenda kujirusha badala ya kufanya kazi ili kujiletea maendeleo kwa kutumia fursa aliyonayo sasa.
Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na Aunty kikizungumza Udaku Special jana kwa sharti la kutotajwa jina kilisema kuwa baada ya Aunty kuona alichoandika Diamond aliachia msonyo wa kufa mtu kuonyesha hakupendezwa hata kidogo huku akibaki kuumia.

“Urafiki wa Wema  na Aunty muda si mrefu utakuwa kama ule wa Kajala, Aunty anataka kumuacha Wema na bwana’ke yeye achukue hamsini zake” kilisenma chanzo hicho.

BEYONCE NA JAY-Z:MAHAKAMAN KISA BLUE IVY WALIIBA

Beyonce na Jay Z Washitakiwa Kwa Kuiba Mtoto (Blue Ivy) na Kujifanya ni Wao

Udaku Specially on Wednesday, August 20, 2014
Tina Seals, a New York woman has allegedly moved to court seeking custody of Pop singer Beyonce and Rapper JayZ's daughter Blue Ivy as the legal mother.

According to sources, the woman's move to court  is aimed at determining if she is indeed the biological mother to Blue.

NewsOne reports that the legal documents indicate that Seals is the woman who actually gave birth to Blue and further associates her with the celebrity couple.

Prior to Blue's birth, there were rumours that Beyonce was only sporting a prosthetic pregnancy and they were planning on getting a surrogate to carry the baby. We all witnessed the bump grow and eventually she went into delivery and shared baby photos of their newborn from the hospital.

A majority of her fans have chosen to trash the rumour, saying that Seals is just delusional but a section of those who believe that the power couple is linked to the Illuminati claim that it could be possible that Seal 'has been used and was used' to breed as a surrogate for the stars.

Other sources reveal that Beyonce is not the first star she has pulled this kind of move on alleging that she previously filled against Kim Kardashian, Mariah Carey and even Kate Middleton.

Do you believe that Tina Seals could be the biological mother to Blue Ivy or is it just another obsessed fan trying to get 15 seconds in the spotlight?

VANESSA vs KIDOTI:NAN KAMZIDI MWENZIE?

Vanessa Mdee vs Jokate Mwegelo

Wednesday, August 20, 2014
They are both smart, classic, intelligent, talented, educated and they both have natural beauty.

RAIS KIKWETE AKIONGOZA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU DODOMA.

MWENYEKITI WA CCM RAIS KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA DODOMA

Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba Mhe Samwel Sitta, alipowasili kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwenye ukumbi wa NEC, Makao Makuu ya CCM Dodoma Agosti 19, 2014. Kulia ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda, kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utawala Bora), Mhe George Mkuchika akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Rehema Nchimbi
Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwenye ukumbi wa NEC, Makao Makuu ya CCM Dodoma Agosti 19, 2014. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Visiwani) na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.Kulia ni Makamu wa CCM (Bara) Ndg Philip Mangula akifuatiwa na Katibu Mkuu wa
CCM Ndg Abdulrahman Kinana
Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa katika Uwanja wa ndege wa Dodoma na Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Rehema Nchimbi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Dkt Emmanuel Nchimbi
Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mbunge wa Songea mjini Dkt Emmanuel Nchimbi, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Mbunge wa jimbo la Peramiho Mh. Jenista Mhagama, na Naibu Waziri wa Fedha na mbunge wa Iramba Magharibi Mhe Mwigulu Nchemba

ONA UNYAMA HUO:MWANDISHI WA MAREKANI ALIVOKATWA KICHWA.

MWANDISHI WA MAREKANI AKATWA KICHWA

Mwandishi wa habari wa Marekani aliyekatwa kichwa, James Wright Foley (kushoto), akiwa amevishwa kanzu maalum.
Kabla ya kuuawa kwake, Foley, aliwataka marafiki, wanafamilia wake na wapenzi wake wote kupambana na “wauaji wangu wa kweli” ambao ni serikali ya Marekani.
 
Foley akiwa na muuaji wake ambaye alisema kitendo cha kumwadhibu mwandishi huyo ni kulipiza kisasi mashambulizi ya ndege za Marekani nchini Iraq.
Muuaji wa Foley akijitayarisha kumkata kichwa.
 
Mama yake Foley, Diana, na baba yake John, wakiwa katika mkesha kanisani kuwataka wapiganaji wa ISIS kuwaachia mateka wao.
 
Foley enzi za uhai wake hadi alipopotea Novemba 2012, baada ya kutekwa huko Taftanaz, kaskazini mwa Syria.
Kikosi cha kiislam cha kijeshi chenye msimamo mkali kimeachilia video inayoonesha mauaji ya mwandishi habari mwenye asili ya Marekani. James Foley alipotea tangu

alipokamatwa mateka na kushikiliwa nchini Syria miaka miwili iliyopita na sasa ameuawa.
Ikulu ya Marekani imesema inaifanyia uchunguzi wa kina video hiyo na ikithibitika kwamba mwandishi huyo wa habari ni wa taifa hilo ,serikali ya Marekani itataka ufafanuzi wa kina ilikuaje na kwanini James Foley. auawe

CHOZI LA CHID BENZ JUU YA DIAMOND PLATNUMZZZ

 
CHID BENZ(CHUMA) ATOA CHOZI AKIKUMBUKA DIAMOND ALIKOTOKA
 
 
Chidi Benz alitabiri mbele ya Diamond Platnumz (wakati bado underground) kuwa angekuja kuwa msanii mkubwa.
Hata hivyo maneno muhimu ambayo rapper huyo alimwambia Diamond ni kuwa asije kunywa pombe wala kuvuta (unga/bangi) maishani mwake.
Chidi ambaye Jumanne hii ameachia single yake mpya 'Mpaka Kuche' aliyowashirikisha Diamond na AY, alikuwa akihojiwa kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM. Katika kuashiria kuwa hiyo ilikuwa ni interview iliyogusa sehemu ya katikati kabisa ya moyo wake, Chidi alijikuta akibubujikwa na machozi.
Chidi alikumbushia siku Diamond alipompigia simu kujitambulisha kwake kuwa ni msanii mchanga anayetaka kumshirikisha kwenye wimbo wake. Hata hivyo siku Diamond amefanikiwa kumpata Chidi hewani ilikuwa ni baada ya kujaribu kumtafuta kwa siku nyingi bila mafanikio na aliwahi kumweleza mama yake namna alivyo na hamu ya kumshirikisha rapper huyo aliyekuwa akimkubali.
Baada ya kumpigia simu, Chidi anadai alimuambia Diamond aende kwao maghorofani Ilala wakazungumze vizuri.
"Sasa nikamuona (Diamond) nikajua huyo dogo ndio yule niliwaambiaga watu kuwa ‘huyu dogo ana sura moja hivi imekaa.. sura yake lazima utaiongelea tu, lazima utasema kitu, namuona atakuja kuwa staa tu, simjui lakini the way alivyo, atakuja kuwa staa,” alikumbushia Chidi.

Taarifa ya Jeshi la Polisi kuhusu ajali iliyotokea Tabora Aug 19

Taarifa ya Jeshi la Polisi kuhusu ajali iliyotokea Tabora Aug 19.

IMG-20140819-WA0032
Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora ambayo ameitoa leo kwa Waandishi wa habari ni kuhusu ajali ambayo ilitokea jana Aug 19 majira ya saa 9 alasiri ambayo ilihusisha mabasi mawili.
IMG-20140819-WA0033
Mabasi hayo ni AM Coach na Sabena ambapo chanzo cha ajali hiyo kimedaiwa kuwa ni mwendo kasi wa mabasi hayo,majeruhi wamelazwa kwenye hosptali ya rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete ambao jumla yao ni 75,waliopoteza maisha jumla 17 na 10 wametambuliwa.
IMG-20140819-WA0034
Madereva wote wawili ni miongoni mwa watu waliopoteza maisha kwenye ajali hii ambayo ilitokea Aug 19 eneo la Mlogolo wilaya ya Sikonge Mkoani Tabora ambapo basi la Sabena lilikuwa likitoka Mbeya kuelekea Tabora na AM lilikua likitokea Mwanza kuelekea Mpanda.
IMG-20140819-WA0031
IMG-20140819-WA0029
IMG-20140819-WA0030   IMG-20140819-WA0033

Tuesday, 19 August 2014

MARIAGE CARTOON...

toon-1993

MWANAMKE KABLA YA NDOA, ANATAKIWA AWE ‘AMETOKA’ NA WANAUME WANGAPI?

MWANAMKE KABLA YA NDOA, ANATAKIWA AWE ‘AMETOKA’ NA WANAUME WANGAPI?

NIswali gumu lakini jepesi kwa mtazamo. Wengi wamekuwa wakiingia katika mjadala huu bila ya kujua suala lenyewe lina sura mbili tofauti.HAITAKIWI
Kwa majibu ya maandiko matakatifu mwanamke na mwanaume hawana ruhusa ya kukutana kimwili mpaka pale watakapopata baraka halali ya kuishi kama mume na mke. Kwa hiyo kumbe hakutakiwi kuwa na idadi!
Baraka hizi kwa siku hizi zinatoka makanisani (kwa Wakristo), misikitini (kwa Waislamu) na katika ofisi za serikali, wengi huita Bomani na husimamiwa na ofisi ya mkuu wa wilaya. Lakini pia kuna ndoa za kimila ambazo husimamiwa na makatibu tarafa.
NI DHAMBI
Kinyume na hapo, kukutana kimwili au kuzini ni dhambi mbele za Mungu. Wataalam wa maandiko wanaiita dhambi hii ni ‘ya kupanga’ na kuamua tofauti na nyingine kwa hiyo anayeitenda anakusudia.
HAKUNA KIFICHO
Lakini cha ajabu katika zama hizi za utandawazi, suala la wachumba au watu wasio katika ndoa kukutana kimwili limekuwa jambo la kawaida huku wengine wakilifanya halali kwa wazazi au ndugu.
IDADI KUBWA KIELELEZO?
John Tommy mwandishi wa Kitabu cha Love Me, Love You aliwahi kusema kuwa idadi kubwa ya wanaume waliofanya mapenzi na mwanamke mmoja kabla hajaolewa ni kielelezo tosha kwamba, mwanamke huyo hawezi kuja kuwa mwaminifu katika ndoa.
Alisema mwanamke aliyelelewa kimaadili, akakulia katika maadili hayo hadi kuolewa, angalau awe amefanya mapenzi na wanaume watatu, akiwemo anayemuoa. Hii ni taswira ya kuonesha uaminifu katika ndoa halali na kuifanya idumu.
WATU WANASEMAJE?
Baadhi ya watu wazima waliozungumza na  safu hii kwa nyakati tofauti walisema, kwa kawaida mwanaume wa kwanza kulala na msichana ambaye hajaingizwa ‘ukubwani’ siye atakayemuoa.
Kwa mujibu wa uzoefu uwezekano wa mwanaume huyo kutooa ni kwa sababu anakuwa mdogo kiumri. Mwanaume atakeyefuata atatenda jambo moja ambalo litamfanya msichana amuone mwongo na hivyo kutengana naye.
Wazoefu hao wanasema mwanaume wa tatu ndiye ambaye ana nafasi kubwa ya kutoa mwanga wa maisha ya ndoa kwa msichana akitangaza uchumba na ahadi nyingine ambazo awali msichana huyo hakuwahi kutamkiwa na waliomtangulia.
Na kipindi hicho ambacho msichana anaweza kuanza kuonekana kama anakomaa kiakili.
“Ukimuona mwanamke mpaka anaolewa ameshalala na wanaume zaidi ya watano hadi sita huyo ana hulka ya umalaya na hatakuwa mwaminifu katika ndoa. Kama una historia ya mwanamke wa sampuli hiyo jaribu kufuatilia nyendo zake,”  alisema bibi mmoja anayepata miaka 76 sasa hapa duniani.

MTOTO WA JACK CHAN ANASWA NA MAJANI(MMEA)

MTOTO WA JACK CHAN ANASWA NA BANGI

Watuhumiwa Jaycee Chan (kushoto) and Kai Ko (kulia).
Staa wa filamu wa siku nyingi, Jackie Chan.
MTOTO wa staa wa filamu wa Hollywood, Jackie Chan aitwaye Jaycee Chan anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Beijing, China baada ya kukutwa na gramu 100 za bangi.
Jaycee Chan ambaye pia ni staa wa filamu kama baba yake alikamatwa Alhamisi iliyopita pamoja na staa mwingine wa filamu kutoka Taiwan, Kai Ko ambapo wote walipimwa na kubainika wametumia madawa ya kulevya aina ya bangi huku gramu 100 za madawa hayo zikikutwa nyumbani kwa Jaycee.
Kwa mujibu wa polisi nchini China, iwapo atakutwa na hatia, Jaycee anaweza kwenda jela miaka mitatu.
Jackie Chan amesafiri kuelekea nchini humo kuona jinsi ya kumnusuru kijana wake huyo.

PAPA FRANCIS AMRUHUSU PADRI WA JIMBO LA MOSHI KUOA

PAPA FRANCIS AMRUHUSU PADRI WA JIMBO LA MOSHI KUOA


Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis.
KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amekubali kumuondolea sakramenti ya upadri, Padri Raymond Mosha wa Jimbo Katoliki la Moshi ikiwa ni miaka 20 tangu padri huyo aombe kujiondoa kwenye daraja hilo.
Barua ya uamuzi wa Papa Francis ilisomwa Jumapili ya juzi katika parokia na vigango vyote vya Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi wakati wa ibada za Jumapili zilifanyika katika makanisa ya jimbo hilo.
Miongoni mwa parokia ambazo barua hiyo ilisomwa ni Parokia ya Karanga ambako Paroko wake, John Matumaini alitoa tangazo hilo katika ibada zote. Uamuzi huo ambao ni nadra sana kutolewa na Papa, unamaanisha kuwa sasa hivi padri huyo yuko huru kuoa na kuwa na familia kama Wakristo wengine.
Hata hivyo, wakati uamuzi huo ukitangazwa rasmi juzi, tayari Padri Mosha ambaye ni profesa wa falsafa na maadili katika Chuo Kikuu cha Nelson Mandela Arusha, ana mke na watoto watatu ambao kwa sasa wako vyuo vikuu.
Padri Mosha alisema aliandika barua kuomba kuondolewa daraja hilo mwaka 1994 kabla ya uamuzi kutolewa juzi.
Katika orodha ya mapadre 185 wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi iliyopo katika tovuti ya jimbo hilo, jina la Padri Mosha linaonekana likiwa ni namba 23.
Akizungumzia hatua hiyo, Padri Mosha alisema: “Ninafurahi kufunguliwa kifugo hiki na hii itanifanya niishi kama Mkristo. Kwa vile hawajaniondolea sifa ya kutoa huduma kama vile ibada za mazishi, sakramenti ya mwisho na ubatizo, nitaendelea kutoa kwa wahitaji kwa sababu ninaupenda ukristo.
“Nashukuru sasa nimekuwa muumini wa kawaida nitaweza kufunga ndoa kanisani kwa kuwa nilikuwa nimefunga ndoa ya kisheria tu kwa DC.”
Kuhusu kwa nini aliamua kuacha upadri, Profesa Mosha alisema ni baada ya kufanya kazi hiyo kwa miaka 20 na akaona ipo haja ya kuwa na familia lakini kanisa lilikuwa haliruhusu.
“Sasa kwa kuwa kanisa haliruhusu mapadri kuoa ndiyo maana nikaamua kuandika barua ambayo hata hivyo, imechukua muda mrefu kujibiwa na tayari nina watoto watatu wako chuo kikuu."

CHEKA NA KATUNI:KITAMBO SANA

http://api.ning.com/files/FXc3J*dW*e0D4DUYd7XpxnMF-5aTWQLjQok0Owc4p9gs2cJusHMNCY4inviUaHuOb0U7*OPX6OIkwN759qR*ULGCWg5t*hr4/dilichenga.jpg

KATUNI:Kwanini NCHI MASKINI?

BABA AMULA MWANAE KINYUME NA MAUMBILE

Baba Amuingilia Bintiye Kinyume Cha Maumbile

August 19, 2014 
Vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia bado vinaendelea Zanzibar baada ya watu wawili kushikiliwa na polisi kwa tuhuma za kubaka.

Katika tukio lililotokea Agosti 4, mwaka huu Muhammed Khafidh Thabit (50), anadaiwa kumbaka mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 14.

Mtuhumiwa huyo alimuingilia binti yake huyo kinyume na maumbile na kumsababishia madhara makubwa mwilini wake.

Akizungumzia kuhusu tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mkadam Khamis Mkadam, alisema tukio hilo limetokea eneo la Misufini.

Alisema baada ya kuhojiwa mtoto huyo, alisema baba yake alikuwa akimlazimisha kufanya mapenzi baada ya mama yake kutengana na baba huyo.

Alisema uchunguzi wa kidaktari umeonesha kuwa mtoto huyo ameingiliwa mbele na nyuma.

Katika tukio lingine la mkoa wa Kusini Unguja  Polisi inamshikilia  Ali Hashim Ali (27) mkazi wa Mwera visiwani hapa kwa tuhuma za kumuingilia mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka tisa.

Kamanda wa polisi mkoani humo, Juma Said Khamis alisema kijana huyo alimrubuni mtoto huyo kwa kumuahidi kuwa atampatia mbuzi wa kufuga.

Alisema mtuhumiwa huyo alimchukua mtoto huyo na kumpeleka katika boma la nyumba na kumfanyia kitendo hicho cha kinyama.

Alisema mtuhumiwa ameshawahi kuwalawiti watoto wengine wawili wa kiume.

Watuhumiwa wote wapo chini ya ulinzi.
Akihutubia Baraza la Idi hivi karibuni, Dk Ali Muhammed Shein alikemea vitendo vya udhalilishaji na kutaka vipigwe vita.

Alisema takwimu za vitendo vya udhalilishaji zinaonesha kuendelea kuwepo kwa vitendo hivyo licha ya jitihada zinazochukuliwa na serikali na kushiriana na wanaharakati.

Ali Kiba Amefunguka Kuhusu Mambo Yaliyomkwaza Kutoka kwa Diamond

August 19, 2014
Mwanamuziki wa Bongo Flava, Ali Kiba amefunguka kuhusu mambo yaliyomkwaza kutoka kwa Diamond miaka michache iliyopita baada ya mkali huyo kutoka na wimbo wa ‘Kamwambie’ uliogeuka kuwa wimbo wa taifa wa Bongo Flava kwa muda. 

Akiongea na kipindi cha Mkasi, Ali Kiba ameeleza kuwa yeye ndiye mtu aliyepitisha ombi la Diamond kurekodi katika studio za SharoBaro kwa kuwa wakati huo alikuwa mdau mkubwa katika uongozi wa studio hizo lakini matokeo yake yalimgeukia hadi kuamua kujitoa katika team hiyo. 

Ameeleza kuwa mara baada ya Diamond kutoka na Kamwambie, aliona gazeti moja lililokuwa lililomkariri akisema kuwa yeye ndiye ‘fimbo’ ya Alikiba na amekuja kumfunika. 

Hata hivyo maneno yaliyowekwa kaitika gazeti hilo yalianza kuaminika kwa Ali Kiba baada ya kukutana nae mara kadhaa kwenye shows. 

“Lakini nilishawahi kukaa na Diamond katika mikutano ya Shows ambazo tunaitwa pamoja wasanii na nini na nini. Mimi napendaga kuongea nae kama mdogo wangu kwa sababu the way nilivyokuwa nikimtreat ni kama wadogo zangu wengine akina Bob Junior akina nani… Nilimsikia akiongea sana kwamba nimekufunika kwenye show fulani, nimekufunika kwenye show fulani. Kwa kweli the way nilivyokuwa nikimtreat kama mdogo wangu. Kwa hiyo yeye alikuwa ameconcentrate sana katika kunifunika.” Alieleza Ali Kiba. 

“Mimi sio mtu wa kumind sawa. Kwa hiyo alivyokuwa anaongea anajifurahisha. Hata kama amenifunika mimi nilikuwa naweza kumpigia makofi vilevile. Si nataka afanikiwe. Kwanza nafurahi. Napenda sana challenge. Inakufanya unaaamke.” Aliongeza. 

Kujirudia kwa neno ‘kufunika’ kila walipokuwa akikaa na Diamond kuligeuka kuwa kero kwa Ali Kiba huku mengine yakipenya kutoka kwa watu wake wa karibu. 

“Kwa hiyo kitu ambacho kilikuwa kinahappen tukiwa karibu hivi, ni hivyo vitu ambavyo akizungumziwa nimekufunikaa..nimekufunika. Nikawa nikitoa video nasikia maneno, kwamba ‘Ali amesikia maneno nimetoa hii na yeye ametoa hii’. Mi sijawahi kumsikia mwenyewe akisema. Ila watu wake wa karibu wa karibu wanakuja wanasema. Unaweza kumjua mtu tabia yake kwa kumuangalia, kwa kuishi nae.” 

Ali ameeleza kuwa hata baada ya kuamua kukaa kimya amlee mwanae wa kiume alisikia tena maneno kutoka kwa mwimbaji kwa Diamond kuwa amemkimbia. 

Hata hivyo, hii ilikuwa story ya zamani ambayo wengi wanaweza kuwa nayo lakini ikamhusu mtu ambaye kwa sasa amekuwa rafiki wa kudumu. 

Hivi karibuni Ali Kiba alisema kuwa hana tatizo lolote na Diamond na kuwataka watu wasimgombanishe na msanii huyo. Ni muda wa biashara. Yaliyopita si ndwele (maradhi) tugange yajayo kwa maendeleo ya Bongo Flava. Kilichobaki ni ushindani wa kibiashara kama alivyosema Babu Tale

Hasheem Thabeet Afunguka, Awaomba Radhi Mashabiki Wake

Tuesday, August 19, 2014
NINGEPENDA KUANZA KWA KUSEMA ASANTENI SANA KWA KUSHOW LOVE KWENYE HILI PAGE LANGU. BINADAMU WOTE TUMEUMBWA TOFAUTI, NA TUMEBARIKIWA TOFAUTI.

SOTE TUNA MAPUNGUFU NA SOTE TUNA MAMBO AMBAYO NDIYO YANAYOTUFANYA TUWE WATU AMBAO TULIVYO SASA. KWA HIYO KAMA ULISHAWAHI KUONGEA NA MIMI UTANIJUA NI MTU WA AINA GANI.

NA KAMA TULISHAWAHI KUKUTANA NA LABDA HATUKUELEWANA KAULI ZETU NAOMBA UNISAMEHE MIMI NI BINADAMU NA NAKOSEA KAMA WATU WENGINE TU. NA NINA MAMBO MENGI YANAENDELEA NIKIWA KAMA BINADAMU NA SIO KUWA NARINGA KWA AJILI YA USTAA AU KITU GANI.

MWISHO WA SIKU SOTE TUNAPITA TU HAPA, JANA ILIKUWA WAO, LEO MIMI, KESHO KUNA WENGINE WANAKUJA. HILO MUNGU NDIO ANAJUA.

NA KAMA HAUJAPATA HIYO NAFASI SIKU MOJA TUTAKUTANA. INSHALLAH.

UKATILI! Mwanamke Auawa, Achunwa Ngozi Mbeya

Tuesday, August 19, 2014
WATU wasiofahamika wamemuua mwanamke mkazi wa Kijiji cha Idiwili, Kata ya Iyula wilayani Mbozi na kumchuna ngozi ya shingo.

Pamoja na kumchuna ngozi marehemu, wauaji hao pia walinyofoa macho, ulimi na koromeo la marehemu.

Baada ya mauaji hayo ya kinyama wauaji hao waliutelekeza porini mwili wa marehemu huyo, Angelina Kameza (26).

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Barakaeli Masaki alisema: 

Tumepokea taarifa ya mauaji hayo ya kinyama lakini bado tunaendelea na upelelezi kujua chanzo chake ni kipi.

“Hatuwezi kuhusisha tukio hilo na imani za ushirikina kama baadhi wanavyosikika ila uchunguzi unafanyika kwa kuwa mwili wa marehemu ulikutwa hauna baadhi ya viungo.

Lakini uchunguzi wa awali unaonyesha marehemu alikuwa katika ndoa ya wanawake sita baada ya kuolewa na mwanaume mwenye umri wa miaka 70 aliyezaa naye watoto wawili.

Kabla ya kuolewa na mzee huyo, enzi za uhai wake aliolewa na mwanamme mwingine aliyefariki dunia katika mazingira yanayofanana na haya kwani naye alinyofolewa baadhi ya viungo vya mwili vikiwamo macho, ulimi na koromeo,” alisema Kamanda Masaki.

Aliwataka wananchi kutoa taarifa katika vyombo vya dola watakapopata taarifa za wauaji hao.

LULU APIGWA CHINI

Lulu Michael Apigwa Kibuti eti Kisa Kiserengeti Boy Alichopiga Nacho Picha

Tuesday, August 19, 2014

Udaku Special Kutoka Instagram leo unasema Etiiiiii....Jisomee Mwenyewe Hapa Chini:




MTOTO PENNY HUYO WEMA AKASOME...

Picha Mpya za Penny ni Shidaaa...Diamond Anaweza Mrudia Akiziona

Tuesday, August 19, 2014

Mrembo Penny Katika Pozi , Unaonaje Picha hizi ..? I think She is Cute More Than ......

HABARI NJEMA KWA JAMII YA WANA MBEYA; AGA KHAN KUANZA KUTOA HUDUMA ZA WANAWAKE KUJIFUNGUA

HABARI NJEMA KWA JAMII YA WANA MBEYA; AGA KHAN KUANZA KUTOA HUDUMA ZA WANAWAKE KUJIFUNGUA


HOSPITALI ya Aga Khna Primary Medical Center, Mbeya, inatarajia kuanza kutoa huduma za kisasa za wanawake kujifungua.
Habari za uhakika kutoka kwenye vyanzo vyetu vya habari, zimesema kuwa, Hospitali hiyo, ambayo ipo katikati ya Jiji la Mbeya, tayari imepata vifaa vyote vya kisasa na vimefungwa ndani ya hospitali hiyo.

Huduma hiyo inaanza kutolewa mwezi Septemba mwaka huu na wanawake wa kwanza watapewa huduma hiyo bure, bali wengine watakuwa wanajifungua kwa fedha zisizozidi Laki mbili.

wanawake wote wajawazito ambao zimefika siku zao za kujifungua, imeelezwa kuwa watatakiwa kufika katika hospitali hiyo bila kitu chochote kama zifanyavyo hospitali zingine, na wakishajifungua kila mmkoja atapewa taulo(Baby show) la mtoto.

Wapenzi wa jinsia moja kupigwa mawe hadharani Kenya?

Wapenzi wa jinsia moja kupigwa mawe hadharani Kenya?

Screen Shot 2014-08-19 at 8.03.13 AM
Nje ya bunge la Kenya.
Ripota wa TZA nchini Kenya Julius Kipkoech anaripoti kwamba nchi hiyo inarejea kwenye headlines kuhusu maswala ya kubuni sheria za kipekee ambapo sasa bunge la kitaifa linapanga kujadili sheria inayopendekezwa kwamba raia yeyote wa kigeni anayepatikana akishiriki uhusiano wa jinsia moja ahukumiwe kupigwa mawe hadharani hadi kufa na kama ni raia wa Kenya basi ahukumiwe kifungo cha maisha jela.
Mwandishi na mdhamini wa sheria hiyo Edward Onwong’a Nyakeriga anapendekeza kuharamishwa kwa ulawiti na kuhukumiwa jela kwa wanaotenda kosa hilo huku akisisitiza >> ‘upo umuhimu wa kuwalinda watoto na vijana ambao wanalengwa na dhulma ambazo kwa mda mrefu zinaepukwa kutokana na mabadiliko, teknolojia na habari isiyo chujwa na watoto mayatima kukosa mwakilishi pamoja na majaribio ya wanaoshiriki uhusiano wa jinsia moja kuwalea watoto ilihali wanaendeleza uhusiano wao’
Mswada huu wa chama cha Republican Liberty Party unaharamisha uhusiano wowote wa jinsia moja na tayari spika wa Bunge la kitaifa Kenya Justin Muturi ameupokea na kuuwasilisha kwa kamati ya sheria bungeni ambayo inatathmini kisha kutoa ripoti kwa bunge.
Screen Shot 2014-08-19 at 8.06.26 AM
Sio kila mmoja anakubaliana na ndoa za jinsia moja hata katika nchi zilizoendelea ambazo Marais wake wanaunga mkono ndoa hizo
Muswada huo pia unapendekeza kupigwa mawe hadharani hadi kufa kwa mtuhumiwa anayepatikana na kosa la kuwalawiti watoto wadogo au anayefanya kitendo hicho na kumuambukiza mtoto virusi vya ukimwi ambapo tayari wabunge 78 wamekubali kuunga mkono muswada huo kuwa sheria na wengine zaidi wanaendelea kushawishiwa.
Haya yanajiri wakati Bunge la kitaifa la Kenya likibuni kikundi mseto cha wabunge kuhusu maisha ya walio katika uhusiano wa jinsia moja na wameahidi kutoa mwelekeo wa jinsi ya kushughulikia jambo hilo huku muswada huu ukitarajiwa kupata upinzani mkali kutoka kwa wanaotetea haki za binadamu.
Mwandishi wa vitabu maarufu nchini Kenya Binyavanga Wainaina amekua miongoni mwa waliojitokeza hadharani na kukiri kushiriki mapenzi ya jinsia moja na wakati huohuo Mashirika ya kutetea haki za wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja hivi karibuni yaliwasilisha pendekezo la kutaka Wabunge kuondoa sheria zote zinazowazuia kuishi maisha yao kama watu wengine.
Katiba ya Kenya mwaka 2010 imeharamisha ndoa ya jinsia moja japo haiharamishi moja kwa moja uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja ambapo pia mwezi uliopita utafiti uliofanywa na kampuni ya Ipsos Synovate umeonyesha kwamba 64% ya Wakenya wanaamini kwamba hisia za kushiriki mapenzi na jinsia sawa ni jambo la kujifunza ilihali 14% kati yao wanaamini watu hao huzaliwa walivyo.
Baada ya kuisoma hii stori unaweza kuacha maoni yako kwenye comments hapa chini.

HIKI NDO ALICHOPOST MAULID KITENGE baada ya kuacha KAZI ITV/ONE

Alichoandika Maulid Kitenge baada ya kuacha kazi ITV/RadioOne

Screen Shot 2014-08-19 at 8.22.01 AMMaulid Kitenge yuko kwenye orodha ya Watangazaji wa muda mrefu wa michezo nchini Tanzania ambapo ujazo wa jina lake uliongezeka baada ya kuanza kufanya kazi na ITV/RadioOne zaidi ya miaka 10 iliyopita.
August 18 2014 Maulid aliandika yafuatayo kwenye page yake ya twitter 
Namshukuru sana Mungu leo nimemaliza miaka 14 ya kutumika kuwa kama mtangazaji wa michezo Radio one stereo na hakika naondoka rasmi
Mpaka asubuhi ya August 19 2014 Maulid alikua hajaandika tweet nyingine ya anakokwenda au atakachofanya baada ya kuondoka ITV/RadioOne
Screen Shot 2014-08-19 at 8.16.51 AM

ISOME HIYO:BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

August 19, 2014

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

Mkurugenzi Msaidizi Habari, Elimu na Mawasiliano toka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Bw. Cosmas Mwaisobwa akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu maandalizi ya utoaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2014/2015, wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa.
Baadhi ya Waaandishi wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi Habari, Elimu na Mawasiliano toka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Bw. Cosmas Mwaisobwa wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.



MCHAKATO WA MAOMBI YA MIKOPO KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015

  1. MAANDALIZI YA UTOAJI MKOPO KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ilitangaza mwongozo na vigezo vya utoaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2014/2015 kupitia magazeti na tovuti yake mnamo wezi Aprili 2014. Mwongozo huo, pamoja na mambo mengine, uliainisha sifa za waombaji mikopo na ruzuku, vipengele vya Mikopo, programu za vipaumbele kwa waombaji wa shahada ya kwanza, shahada za uzamili na uzamivu waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya juu zinazotambulika. Maombi ya mikopo kwa waombaji wapya yalifanyika kwa njia ya mtandao kwa anuani ya http://olas.heslb.go.tz au kupitia anuani ya tovuti ya Bodi ya Mikopo ambayo ni: www.heslb.go.tz.
Kulingana na Mwongozo wa Utoaji Mikopo na Ruzuku kwa mwaka wa masomo 2014/2015, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ilifungua maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao (OLAS) kuanzia Aprili 23, 2014 na kuendelea kupokea maombi hayo hadi Julai 31, 2014.

Mabadiliko machache yamefanyika, kubwa likiwa ni kwa wanufaika wanaoendelea na masomo, tofauti na ilivyokuwa miaka iliyopita, hawakutakiwa kujaza tena fomu kuthibitisha uhitaji wao wa mikopo kwa mwaka unaofuatia, isipokuwa kwa wale ambao waliopenda kusitisha kuendelea kupokea mkopo kutoka Bodi. Wanufaika wa mikopo wanaoendelea na masomo wataendelea kupata mikopo yao kulingana na viwango walivyopangiwa awali.

    1. Maombi yaliyopokelewa

Jumla ya maombi 58,037 yalikuwa yamepokelewa hadi kufikia tarehe 31 Julai, 2014. Kati ya maombi hayo, jumla ya maombi 37,689 ni ya waombaji wa kiume na maombi 19,592 ni ya waombaji wa kike. Uchambuzi zaidi wa waombaji wa mikopo unaonyesha kuwa Waombaji wa kundi la diploma ya ualimu wa sayansi ni 480 (Me – 324, Ke – 156), Waombaji wa shahada ya uzamili/uzamivu (kwa vyuo vya ndani ya nchi) ni 276 (Me – 194, Ke – 82), Waombaji wa shahada ya kwanza (kwa vyuo vya ndani ya nchi) ni 56,922 (Me – 37,460, Ke – 19,462), Waombaji wa shahada ya uzamili/uzamivu (nje ya nchi) ni 126 (Me- 88, Ke – 38) na Waombaji wa shahada ya kwanza (nje ya nchi) ni 233 (Me – 141, Ke – 92).

1.2 Uchambuzi wa Maombi
Baada ya kufungwa rasmi kwa kipindi cha kupokea maombi ya mikopo, hatua inayoendelea kwa sasa ni uhakiki (verification) wa taarifa za waombaji, kwa kuzipitia nyaraka mbalimbali zilizoambatanishwa na waombaji mikopo ambazo ni cheti cha kuzaliwa, vyeti vya taaluma, vielelezo vya mdhamini, saini ya mwombaji na mdhamini wake na ushuhuda wa Mwanasheria au Hakimu kwamba vivuli vya nyaraka zilizowasilishwa kwenye Bodi ni halisi.

1.3 Upangaji wa mikopo
Mchakato wa uchambuzi na upangaji wa mikopo utakamilika baada ya majina ya wanafunzi waliodahiliwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) kujiunga na vyuo mbalimbali yanapowasilishwa rasmi kwenye Bodi ya Mikopo. Udahili wa wanafunzi unafanywa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kwa mfumo wa pamoja wa udahili (CAS) unaotumiwa na vyuo takribani vyote vya elimu ya juu nchini. Kwa vyuo ambavyo havimo katika mfumo wa pamoja wa udahili (CAS) hutuma TCU majina ya wanafunzi ambao vimewadahili ili waweze kuthibitishwa kabla ya kupatiwa mikopo. Taarifa za udahili ni muhimu katika zoezi la upangaji wa mikopo kwa kuwa zinatoa mwongozo wa gharama halisi za programu za mafunzo. Wanafunzi wanaostahili na waliotimiza masharti na vigezo vya ukopeshaji ndio hupangiwa mikopo kulingana na bajeti iliyotengwa na Serikali.

1.4 Kutangazwa kwa majina ya wanafunzi waliopata mikopo
Majina ya wanafunzi waliopata mikopo kulingana na udahili yatatangazwa kwenye tovuti ya Bodi na taarifa hiyo pia itatangazwa katika vyombo vya habari ili kuwataarifu wadau wote ikiwa ni pamoja na wanafunzi, vyuo vya elimu ya juu, wazazi na umma kwa ujumla. Nakala za majina ya wanafunzi waliopangiwa mikopo zitatumwa kwenye vyuo husika.

  1. WANAFUNZI WA MASOMO YA STASHAHADA YA UALIMU

Kwa kutambua umuhimu wa masomo ya Sayansi na kukabiliana na upungufu
wa walimu wa masomo hayo katika ngazi ya shule za Msingi na Sekondari, mwaka huu serikali imetoa fursa ya mikopo kwa wanafunzi watakaojiunga na masomo ya Stashahada maalum ya Ualimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati.

Wanafunzi wapatao 5,000 wanatarajiwa kujiunga na Stashahada hii maalum katika Chuo Kikuu cha Dodoma na wote watanufaika na mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.

  1. HITIMISHO

Kwa Taarifa hii, Bodi inapenda kuwataarifu wadau wote kuwa mchakato wa utoaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2014/2015 unaendelea vema.

Aidha, Bodi inawasisitizia waombaji wa Mikopo, wazazi/walezi na umma kwa ujumla kutambua kuwa Mikopo ya Wanafunzi wa elimu ya juu ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Uchangiaji wa Elimu ya juu na hivyo iwapo kuna waombaji wanaoweza kujigharamia, wasiombe mikopo ili kutoa nafasi kwa wahitaji wengi zaidi kunufaika.

Imetolewa na:


KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU.
na fredy mgunda