Saturday, 30 August 2014

MAMBO YA UNYANGE HAYO::MISS TANZANIA USA PAGEANT YAPAMBA MOTO.

MISS TANZANIA USA PAGEANT YAPAMBA MOTO, MAMISS WAANZA KUWASILI TAYARI KUWASHA MOTO LEO JUMAMOSI‏

 Miss Tanzania USA Pageant kesho itafikia ukingoni itakapofanyika Downtown, Silver Spring Maryland nchini Marekani katika picha Jesca Kalemera (aliyesimama) akijinoa mwishomwisho mbele ya washiriki wenzake huku Pendo Rancy (kushoto) mmoja ya waratibu wa Miss Tanzania USA Pageant akimsikiliza wengine katika picha ni washiriki wa Miss Tanzania USA Pageant 2014 Maria Rutayuga (wapili toka kushoto), Mercy Sukaya (watatu toka kushoto) ambaye anatokea Michigan na anayefuatia ni Grace Mlingi.
 Washiriki wa Miss Tanzania USA Pageant wakifuatilia jambo kutoka kushoto ni Maria Rutayuga, Mercy Sukaya na Grace Mlingi.
 Kushoto ni Pendo Rancy mmoja ya waratibu akimsikiliza mmoja ya washiriki wa Miss Tanzania USA Pageant (hayupo pichani) huku Maria Rutayuga akifuatilia kwa makini.
 Pendo Rancy akiwaeleza jambo washiriki wa miss Tanzania Usa Pageant walipokua wakijinoa mwisho mwisho kwa ajili ya Jumamosi Aug 30, 2014 watakapo washa moto kumtafuta miss Tanzania USA Pageant mpya.
 Kutoka kushoto ni Maria Rutayuga kuotoka Maryland, Jesca Kalemera kutoka New Jersey, Mercy Sukaya kutoka Michigan na Grace Mlingi kutaoka Maryland.
 Washiriki wakimsikiliza mmoja ya waratibu alipokua akiwaelekeza jambo kwenye hotel waliyofikia ya Double Tree iliyopo Dwntown Silver Spring.

UZAZI WA MPANGO::::WATAKIWA KUZAA WATOTO KWA MPANGO NA SIYO BAHATI.

August 30, 2014

WATAKIWA KUZAA WATOTO KWA MPANGO NA SIYO BAHATI.


Watanzania wametakiwa kuzaa watoto kwa kwa kupanga na siyo kwa bahati mbaya kama wenge wao wanavyosema  ikiwa ni pamoja na kuondokana na dhana kwamba kila mtoto anazaliwa na Bahati yake.

Wito huo umetolewa leo na Mganga mkuu wa mkoa wa Mwanza Dr Valentino Bangi wakati wa ufunguzi wa Zahanati wa Marie Stopes uliofanyika katika katika wilaya ya Nyamagana.

Dr Bangi amesema kuwa watanzania wengi wamekuwa na mazoea ya Kuzaa watoto wengi licha ya kwamba hawana uwezo wa kuwatunza hali inayopelekea ongezeko la watoto waishio katika mazingira Magumu.

Katika hatua nyingine Dr Bangi ametoa wito kwa makampuni ya Bima ya Afya kutumia uwepo wa zahanati hiyo kuwekeza katika afya na kuwataka vijana jijini Mwanza kutumia Zahanati hiyo kupata Elimu ya Mapambano ya virusi vya ukimwi.

Awali akisoma Hotuba kwa niaba ya Mkurugenzi wa Rasilimari watu wa Marie Stopes iliyosomwa na Bi Elly Reweta,amesema kuwa Zahanati hiyo itatoa huduma zote za matibabu ikiwa ni pamoja na huduma za uzazi kwa vijana iliyopewa jina la  CHAGUA MAISHA THE GOOD LIFE.

Uzinduzi wa Zahanati hiyo jijini Mwanza una kamilisha idadi ya Zahanati kumi katika mikoa mbalimbali nchini zinazomilikiwa na Marie Stopes ikiwa ni pamoja na  Hospitali kubwa moja iliyopo jijini Dar es Salaam.
 
na fredy mgunda

DAAH::::Ukweli Kuhusu Kifo cha Betty Ndejembi

Ukweli Kuhusu Kifo cha Betty Ndejembi, Unyanyasaji Kwenye Mitandao ya Kijamii Yahusika

Saturday, August 30, 2014

Ninaandika makala hii nikitambua bayana kuwa itamuudhi kila mtu anayeingia mtandaoni kwa minajili ya kuwanyanyasa watu wengine. Lakini siku zote ninaamini katika busara hii: kuuchukia ukweli hakuufanyi kuwa uongo. Ukweli ni ukweli na uongo ni uongo. Ukweli hauwezi kuwa uongo, na kadhalika uongo hauwezi kuwa ukweli. Kamwe asilani.
Wakati tunaomboleza kifo cha ndugu yetu Betty Ndejembi hatuwezi kukwepa ukweli kwamba siku chache kabla ya kifo chake binti huyo alinynyaswa mno kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter. Japo hadi muda huu hatuwezi kuhusisha moja kwa moja uhusiano kati ya unyanyasaji huo na kifo cha binti huyo, ukweli tu kwamba mtu akinyanyaswa masaa kadhaa kabla ya kifo chake, waweza kujenga picha flani.
Naomba ieleweke kuwa simlaumu mtu kwa sababu sina mamlaka ya kufanya hivyo bali dhima ya makala hii ni rambirambi zangu na kuzungumzia tatizo la unyanyasaji mtandaoni, sambamba na suala zima la unafiki kila kinapojiri kifo hususan cha mtu maarufu.
Tuna tatizo kubwa huko mitandaoni. Tumefika hatua ya kuwapa umaarufu watu wenye matusi ya nguoni, wazushi, wambeya, wanafiki, wanaharamu na kila aina ya binaadamu wanaostahili laana lakini twaishia kuwatukuza. Kwa Twitter, matusi imekuwa ni njia ya mkato ya kupata umaarufu. Kuna wenzetu wengi tu wenye 'umaarufu' huko Twitter, na ukidadisi chanzo cha 'umaarufu' huo, utaambiwa 'ah huyu ana matusi si mchezo!'
Kuna watu wazima na akili zao wanatumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii aidha kunyanyasa wenzao kama si kusherehesha unyanyasaji huo. Marehemu aliitwa majina kadhaa ya kumdhihaki kabla ya kukutana na mauti. Kuna waliomwita Di Maria na wanajifahamu. Japo sijui chanzo cha 'ugomvi na aliogombana nao' (na ndio maana sikujihusisha nao kwani haukunihusu), kuna wanafiki wengi tu waliokuwa katika nafasi nzuri ya kuzima moto huo hasa kwa vile baadhi yao walikuwa wakizifahamu pande zote mbili za 'ugomvi' husika.
La kukera zaidi ambalo ni wazi litajichomoza wakati wa maombolezo haya ni unafiki: baadhi ya watu walewale waliodiriki kumwandama marehemu wakati wa uhai wake watageuka kuwa wenye uchungu mkubwa baada ya kifo chake. Hii inanikumbusha suala ambalo nimeshawahi kulizungumzia mara kadhaa, katika hali ya utani japo wenye uweli, kwamba 'wakati mwafaka kabisa wa kutafuta vipaji vya uigizaji ni kwenye misiba: watu walewale waliokuwa wakikuchukia kwa nguvu zote watageuka wenye uchungu mkubwa kwa kifo chako.
Ukiangalia baadhi ya tweets za mwisho za marehemu ni wazi kuwa binti huyo alikuwa anahitaji msaada kutoka kwa wanaomjali
Hata pasi uelewa wa taaluma ya saikolojia, tweets za aina hii zinaashiria tatizo, na laiti 'wenye upendo wa dhati' wangeingilia kati muda huo, huenda muda huu Betty asingekuwa marehemu. 
Na hizo tweets mbili ambazo ni miongoni mwa za mwisho kabisa za marehemu ni ushuhuda tosha wa jinsi alivyokuwa akisumbuliwa na wanyanyasaji dhidi yake mtandaoni. Ndio pengine kilichomuua ni maradhi ya kawaida ya kibinadamu lakini kila mwenye ubinadamu hatoshindwa kuhusisha unyanyasaji huu na hali mbaya ya afya aliyokuwa nayo hadi anafariki.
Kuna watakaolaumu kuwa ninatumia kifo cha binti huyo kwa 'maslahi binafsi.' Hapana, sina maslahi yoyote binafsi hasa ikizingatiwa kuwa sikuwa nikifahamiana na marehemu. Hakuna anani-follow na mie sikuwa nam-follow. Labda maslahi pekee niliyonayo ni upinzani wangu mkali dhidi ya unyanyasaji wa mtandaoni. Vyovyote ilivyo, marehemu alikuwa bullied kabla hajafariki na atakayetaka kukataa ukweli huo na akatae lakini utabaki kuwa ukweli usioweza kugeuka uongo. Na kwa hakika, kila aliyeshiriki kumnyanyasa binti huyo atakuwa anasutwa na nafsi yake, hata kama atatafuta hifadhi kwenye 'huu sio wakati wa kulaumiana' au 'we failed you Betty.' 
Mara nyingi nimekuwa nikiwalaumu watu wanaodai 'Instagram imekuwa mbaya' au Twitter imeharibika siku hizi' ambapo mara zote nimewakumbusha wahusika kuwa katika hii mitandao ya kijamii, ni muhimu kuwa makini katika nani wa kum-follow. Maana yangu ni kwamba ukim-follow mtu mwenye matusi, utashuhudia matusi katika anachoandika. Ukim-follow mtu wa busara, utashuhudia busara.
Hata hivyo, katika siku za hivi karibuni kumeibuka kundi kubwa tu la watu wenye busara na elimu zao lakini wepesi wa kuvutiwa na vitu vya 'kipuuzi' - umbeya, matusi, majungu, na upuuzi mwingine, na hawasiti kushea na wanaowa-follow. Ni hivi, mtu akitweet tusi, kisha ukali-retweet, utambue kuwa unalikuza (amplify) tusi hilo. Na kimsingi, kwa kiasi kikubwa, tuna-RT vitu tunavyoviunga mkono. Uki-RT tusi maana yake unaliunga mkono. Na ni wazi mwenye kujiheshimu, na kuheshimu 'watu wa maana' wanaom-follow hawezi ku-RT upuuzi.
Tatizo kubwa sasa ni kwamba waweza kuamua kuwa-follow watu unaodhani wana busara au akili za kutosha lakini ukaishia kusoma vitu vya ajabu ajabu kwenye timeline yako kutokana na haya 'mahaba' ya ku-RT vitu vya kipuuzi. 
Binafsi, nadhani chanzo kikubwa cha mitandao ya kijamii kuwa 'sehemu za kukera, kuogopesha, kunyanyasana, nk' ni ile hali ya baadhi ya wenzetu kutokuwa na vitu muhimu vya kufanya katika maisha yao. Ni wazi kwamba ukiwa busy na maisha yako hutokuwa na muda wa kubughudhi wenzako. 
Kingine kinachopelekea social media kuwa 'dunia uwanja wa fujo' ni ugonjwa mkubwa unawasumbua baadhi ya wenzetu: kusaka sifa wasizostahili. Wanasema,. ashakum si matusi, 'lugha ya mpumbavu ni matusi,' na ndo maana baadhi ya wenzetu wasio na cha maana cha kuongea katika hadhara hukimbili matusi, unyanyasaji, maneno macha
Nitamke bayana kuwa siandiki makala hii nikitegemea kuungwa mkono na wahusika wa unyanyasaji mtandaoni. Na kwa hakika kuna uwezekano mkubwa wa makala hii kuzua 'kampeni ya chuki' dhidi yangu kutokana na makala hii. Tatizo kubwa la wenzetu hawa ni kutotaka kuambiwa kuwa 'Hapana, hili ni kosa. Na kosa ni kosa, haliwezi kuwa sahihi.' Lakini pamoja na uwezekano wa 'kuwashiwa moto' kutokana na makala hii, wito wangu kwa kila mwenye busara na akili ni kuliangalia tukio hili la kusikitisha kama 'wake up call.' Tujifunze, tujisahihishe. Tuache kusherehesha vitu vya kipuuzi mtandaoni.
Ifike mahala, ukishindwa kumkemea mtu mwenye tabia mbaya mtandaoni basi chukua option  rahisi ya kum-unfollow au ikibidi kum-block. Na ifike mahala kuwafahamisha watu wanaoendekeza utoto, majungu, umbeya, unyanyasaji na upuuzi mwingine kuwa kama hawana kitu cha maana cha kufany katika maisha yao basi isiwe sababu ya kuwasumbua wenzao wenye majukumu katika maisha yao.
Tukemee maovu badala ya kutarajia yataondoka yenyewe tu. Tuomboleze kifo cha Betty kwa kusema 'NO' kwa cyberbullies (wanyanyasaji wa mtandaoni). Tufike sehemu tuache kuwasujudia wahuni wanaodhani matusi ni sehemu ya wimbo wa taifa. Tuwakwepe waendekeza majungu, wanyanyasaji, wataka sifa za kipuuzi, na watu wasiofaa katik maisha yetu.
Wakati 'tunatafuta haki kwa marehemu Betty kutokana na unyama aliofanyiwa,' suala ambalo ni la kisheria, kilicho ndani ya uwezo wetu ni kukemea unyanyasaji mtandaoni (cyber bullying). Wakati hadi muda huu hatuwajui waliomfanyia marehemu unyama huo, takriban sote twawajua vema wanyanyasaji wa mtandaoni. Tuanze na hawa, kwani leo wamefanya kwa kwa marehemu Betty kesho itakuwa kwako.
Mwisho kabisa, ni muhimu kwetu sote kutambua kuwa tulitoka kwa udongo na tutarudi kwa udongo. Kifo ni hatma ya kila mmoja wetu.Betty ametutoka lakini nasi twaelekea huko. Visa, chuki, kunyanyasana, na vitu vingine visivyopendeza japo ni kama sehemu ya maisha yetu havipaswi kupewa nafasi katika maisha yetu haya ambayo hakuna mmoja wetu mwenye japo 'lue' ya lini yatafikia kikomo. TUPENDANE na TUHESHIMIANE.
Kwako marehemu Betty, hakuna tunaloweza kusema au kufanya sasa kurejesha uhai wako. Na hakuna neno sahihi la kuonyesha jinsi gani kifo chako kimewagusa wengi. Kubwa tunaloweza kufanya ni kukuombea kwa Mwenyezi Mungu akupatie pumziko la milele na mwanga wa milele akuangazie upumzike kwa amani. Amina.
Evarist Chahali

UDAKUZZZZ::::::JIONEE MCHEPUKO WA LADY JAY DEE

Lady Jay Dee Adaiwa Kuopoa Ka Serengeti Boy , Picha Zanaswa

Saturday, August 30, 2014
Na Musa Mateja
OHOOO! Siku chache baada ya ndoa ya Legendary wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ na mtangazaji mahiri nchini, Gardner Gabriel Habash ‘G Habash’ kudaiwa kuvunjika, gumzo limeibuka kufuatia kunaswa kwa picha za Jide na kijana mmoja (dogodogo) aliyetajwa kwa jina la Meddy Ahmed ‘Mtoto wa Vitoto’, Risasi Jumamosi linakupa kinaga ubaga

TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini, Mtoto wa Vitoto huyo amekuwa na urafiki uliotukuka na Jide kwa muda mrefu kabla na baada ya mtafaruku wa ndoa ya Jide na mumewe Gardner hivyo kudaiwa kuwa ndiyo faraja ya mawazo ya mwanamuziki huyo hususan kipindi hiki cha changamoto ya mgogoro wa ndoa yake.

Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kuwa, ukaribu wa Jide na bwa’mdogo huyo ulipitiliza kiasi cha watu wa karibu na staa huyo kuanza kuhisi huenda wana uhusiano usiofaa.
“Ukaribu wao ulipitiliza hadi kila mtu wa karibu na Jide akautilia shaka, isitoshe kama unavyojua, Jide si mtu wa kuweka mambo yake hadharani. Mbaya zaidi Jide amekuwa akimposti dogo huyo kwenye mitandao yake ya kijamii,” kilisema chanzo hicho


ADAI NI MARAFIKI
Huku akiashiria sauti ya kutojiamini, dogo huyo alisema yeye na Jide ni marafiki wakubwa katika mazingira ya kawaida, pia  ni shabiki wake kama walivyo wengine ila ishu ya picha mtu yeyote anaweza kupiga.

Kuhusu kuendesha gari linalodaiwa ni la Jide, dogo alisema hajawahi ila ameshapiga nalo picha na mtu yeyote anaweza kufanya hivyo kama ana uhusiano mzuri na mwanamuziki huyo.
“Jide ni rafiki yangu na mimi ni shabiki wake wa kawaida. Kwa hiyo hilo siyo tatizo lakini pia kuhusu gari mimi sijawahi kuendesha gari la Jide lakini nimewahi kupiga nalo picha kweli kama shabiki mwingine na hakuna shida, ila siyo wapenzi, ni marafiki tu,” alisema Mtoto wa Vitoto.
GPL

INAUMA SANA:Mama amefariki baada tu ya kujifungua hawa Mapacha watatu.

Inasikitisha: Mama amefariki baada tu ya kujifungua hawa Mapacha watatu.

1 
‘Ni kweli tumepokea Watoto watatu ambao ni wachanga wakiwa na kilo 1.7 na 1.8 kutokea Misungwi, mama yao alifariki muda mfupi tu baada ya kujifungua na chanzo ni maamuzi yake ya kukataa kupewa matibabu yanayohitajika ambayo ni kufanyiwa Opareshen’
‘Aliweka saini kabisa ya kukataa kufanyiwa opareshen ili ajifungue kwa kutumia njia hiyo hivyo ikabidi ajifungue kwa njia ya kawaida ambayo ilimfanya atokwe na damu nyingi sana na ndicho kilichosababisha kifo chake’ hizi ni sentensi za mwanzo kutoka kwa Dr. Baraka Malegesi wa hospitali ya Bugando ambao ndio imewahifadhi hawa watoto kwa sasa.
Akihojiwa na millardayo.com Dr. Malegesi ameendelea kusema ‘tumewapokea watoto na bado tuko nao hapa tunawahudumia vizuri wako na mama yao mdogo lakini hali ni ngumu kwa sababu maisha ni magumu kwake na tumejitolea hospitali kuwapa maziwa lakini gharama ni kubwa kwa sababu wiki ni zaidi ya elfu 70 kuwahudumia sasa katika kipato cha chini ndugu zake hawana uwezo’
Daktari huyu amesema kama kuna Mtanzania yeyote anaguswa kusaidia watoto hawa kwa fedha yoyote ile hata ya kutuma kwa M-Pesa, anaweza kufanya hivyo wakati wowote.

2
Inawezekana kabisa una uwezo wa kuwasaidia kiasi chochote kile cha fedha ulichonacho kuwafanya Malaika hawa waishi vizuri kwani mama yao mdogo hana uwezo kabisa wa kuwalea, kama umeguswa niachie mawasiliano yako kwenye comment za hii post mtu wangu.

BOKO HARAM WATEKA KANISA

BOKO HARAM WATEKA KANISA




Kundi la kigaidi la Boko Haram nchini Nigeria  limeshambulia na kuteka  kanisa la katoliki nchini humo. 

Kwa mujibu wa vyombo vya habari  tukio hilo limetokea katika mji wa Madagali, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ambapo inaelezwa kuwa, wanachama wa Boko Haram, baada ya kuvamia kanisa hilo wanaendelea kulidhibiti hadi sasa.

 Jason Obasuyi, mmoja wa makasisi wa mji huo amenukuliwa akisema kuwa, hali ya Wakristo wa mji wa Madagali ni mbaya sana. Aidha ameitaka serikali ya Abuja kuchukua hatua za haraka kurejesha usalama katika mji huo. 

Katika siku za hivi karibuni, wanachama wa kundi hilo la kigaidii lenye uelewa potofu wa mafundisho ya dini Tukufu ya Kiislamu, wameelekeza mashambulizi yao katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa Nigeria, sambamba na kuidhibiti miji mingi ya maeneo hayo na kutangaza utawala wao. 

Hivi karibuni wanamgambo wa kundi hilo walitangaza kuanzisha kile walichokitaja kuwa eti ni utawala wa Khilafa huko kaskazini mashariki mwa mji wa Gwoza. 

Abubakar Shekau kiongozi wa kundi la Boko Haram alisema katika mkanda wa video kwamba, ameanzishai utawala wa khilafa katika mji wa Gwoza baada ya kuuteka mji huo mapema mwezi huu.

AJALI!!AJALI!!!WATU WATATU WANUSURIKA KUFA...DAR

WATU WATATU WANUSURIKA KUFA KWA AJALI DAR

Mchina aliyekuwamo kwenye gari akizungumza kwa simu, pembeni yake ni askari wa usalama barabarani.
Dereva wa Opa ambaye hakufahamika jina lake mara moja.
Watu wakishuhudia gari likitolewa mtaroni.
Gari la break down likivuta Opa iliyoingia mtaroni.
Aliyenusurika katika ajali hiyo, Abdukarim akiwa pembeni akitafakali.
Watu wawili akiwemo raia wa China na dereva ambaye ni mtanzania wamenusurika kufa katika ajali iliyotokea maeneo ya Millennium Tower, Kijitonyama jijini Dar es Salaam ikihusisha gari ndogo aina ya Opa.
Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema chanzo cha ajali hiyo ni gari la zimamoto lililokuwa linatokea njia ya Mikocheni kuingia barabara kubwa.
“Gari la fire lilikuwa kasi sana huku likipiga king’ora, kwa hiyo kujihami dereva mwenye Opa akajikuta ameingia mtaroni, tunashukuru hakuna aliyeumia,’’ alisema Robert.
Aidha mtu mwingine aliyenusurika katika ajali hiyo ni Abdukarim ambaye alikuwa ndani ya mtaro huo akisafisha. Kamera ya GPL ilishuhudia askari wa usalama barabarani akiwa eneo la tukio huku break down likianza kuitoa gari hiyo mtaroni.

Oparesheni tokomeza yarejeshwa kinyemela,WATU WATESWA SANA



Oparesheni tokomeza yarejeshwa kinyemela, wavuvi wakandamizwa; serikali yaruka kihunzi

Posted By Fikra Pevu
OPARESHENI iliyoacha makovu kwa wananchi wengi walio kando na hifadhi za wanyama pori mwaka jana 2013, kisha kusitishwa na kuundiwa Tume ya Uchunguzi, imerejeshwa na wajanja wachache huku wakiwaumiza wananchi na kuchukua rushwa katika maeneo inapofanyika zoezi hilo.

Uchunguzi uliofanywa na FikraPevu umebaini kuwa hali hiyo inaendelea katika kijiji cha Kilangawana, Kata ya Kipeta katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa ambapo imeelezwa kuwa kijiji hicho kilichopo kando ya Ziwa Rukwa na pori la Uwanda linalosemekana kuwa na tembo wanne wasiozaliana; wananchi wake mpaka sasa wanaishi kwa mashaka kutokana na vitendo wanavyofanyiwa na baadhi ya askari wa wanyamapori.

Wananchi kijini hapo wameiambia FikraPevu kuwa baadhi yao wanategemea uvuvi na biashara ya maji kutoka mto Momba na kuwa walianza kupigwa na kuporwa mali zao na askari hao mara tu baada ya ziwa hilo kufungwa tangu Desemba  31, mwaka jana kisha kufunguliwa kwa uvuvi Julai mosi mwaka huu.

Mmoja wa wanananchi hao ambaye ni mvuvi, Majuto Mwambogoja (35), amesema kuwa tangu Agosti 3, 2014, askari hao wamevamia fukwe za Ziwa Rukwa na kuanza kuwapiga wavuvi na kupora mali zao.

“Tuliamua kuandamana ili tuweze kupambana nao ili lolote litakalotokea liwe hivyo hivyo maana tunanyanyaswa, kupigwa na kuporwa mali zetu bila kutueleza tatizo letu, lakini Mwenyekiti wa CCM kata, alitutuliza na kutusikiliza lakini mambo bado yanaendelea’’ alisema Mwambogoja.

Vitisho vyatawala

Imebainika kuwa kila wakati wananchi walipowahoji askari hao ili kujua makosa yao, waliwatishia kuwa wakiendelea kutowatii watawapa kesi ya ujangili ya kukutwa hifadhini wakiwa na silaha aina ya kisu, upanga na shoka, vitu ambavyo wavuvi wanamiliki kwa ajili ya uvuvi halali.

Naye Magoma Mserikali (44) na Gwamaka Mwansasu, alikaririwa na FikraPevu akisema kama wao ni wavunjaji wa sheria walitegemea wanapokamatwa wangepelekwa mahakamani, lakini ajabu askari hao wanawapiga viboko, kupora mali zao na kuomba rushwa.

“Ilikuwa Agosti 7 na 17-18 mwaka huu, wamekuja tena wamepiga sana watu, kupora mali zikiwemo samaki, fedha, kuharibu ngalawa na kuondoka na samaki ambao wanaenda kuwauza! Tunajiuliza hii serikali ikoje wakati tunavua kihalali eneo hili? Tukikimbilia kwenye visiwa kuishi huko ndani ya maji wanatufuata nako!” alisema Mserikali.

Walisema askari hao wanafanya vitendo kama vilivyofanywa na oparesheni tokomeza, ambapo walichoma hata makazi ya watu kwa kisingizio kuwa zipo ndani ya hifadhi, jambo ambalo lilisababisha mpaka mkuu wa mkoa wa Rukwa kufika Kijijini hapo mwaka jana, na kuwa pori la Uwanda, halina ishara zozote zinazoonesha kuwa ni pori la hifadhi la serikali na kwamba wananchi hawaruhusiwi kupita ndani ya pori hilo ili kwenda kuvua samaki katika ziwa Rukwa, ingawa hakuna njia zaidi ya kupita ndani ya pori hilo.

Kijana Amon Staphod Mwandosya (25) – (Pichani), mmoja wa waathirika wa vipigo vya askari hao, ambaye mpaka sasa ana majereha ya vipigo, alisema aliitwa na askari hao kuwateremshia mzigo kwenye gari yao, baada ya hapo alihitaji kupata haki yake, akasukumwa akiwa juu ya gari, alipodondoka akaanza kushushiwa kipigo jambo ambalo lilimfanya akimbie kuokoa maisha yake.

“Ilikuwa tarehe 6 mwezi huu, niliitwa na askari hao kuwashushia mchele debe kumi kwenye gari yao, nilipomaliza na kuanza kuwadai Shilingi Elfu sita (6,000/=), ndipo wakaniambia niondoke haraka, nilipozidi kudai nikaanza kupigwa” alisema Mwandosya huku akionesha majeraha mikononi, jino lililovunjwa na kuvua nguo ili kuonesha majeraha zaidi.

Alipoulizwa kama alienda kutoa tarifa Kituo cha Polisi na kutibiwa, amesema hajaweza kufanya hivyo kwasababu hana imani kwamba angesikilizwa na mpaka sasa anaendelea kujitibu kwa kununua dawa dukani na dawa za kienyeji.

Uongozi wa Kijiji cha Kilangawana, ulipoulizwa kuhusiana na vitendo hivyo, ulisema hauna taarifa zozote za kusitishwa uvuvi, bali wanachoshuhudia ni askari hao kupita kijijini na kupiga wavuvi ziwani, ambao ni wakazi wa kijiji hicho na wengine.

Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Ludovick Akilimali, ameiambia FikraPevu kuwa oparesheni hiyo imezuka bila hata uongozi wa Kijiji kujua, kwasababu taarifa zilizopo ni kwamba ambao wamepigwa marufuku ni wakulima na wafugaji waliokuwa wanalima kwenye pori hilo.

Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Oscar Kamkwamba, amesema kuwa wananchi wa eneo hilo wanashindwa kuchangia maendeleo kutokana na kupigwa marufuku na askari pori kuvua samaki, kwasababu ndiyo tegemeo la uchumi wao na tayari wawakilishi wa Mkurugenzi wanayo taarifa tangu Agosti 8, mwaka huu.

“Mwenyekiti uwe unawaweka wazi waandishi wa habari, hapa Kijijini watu wote wanategemea uvuvi, hakuna hata kipande cha kulima, watu wasio wavuvi wanachota maji na kuwauzia wanaovua kwa ajili ya kunywa’’ alisema Mtendaji huo.

Kwa upande wa wajumbe wa serikali ya Kijiji ambao waliokuwepo katika mahojiano kati ya FikraPevu na Mwenyekiti wa Kijiji hicho, walisema kuwa wanaiomba serikali iangalie oparesheni hiyo na kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kufika haraka eneo hilo ambapo Agosti 18, mwaka huu, yalitaka kutokea maafa makubwa baada ya askari hao kuvamia kijijini na kuanza kupora mali za watu na kuwarusha kichurachura.

Mkuu wa wilaya hiyo Mathew Sedoyeka, amekaririwa na FikraPevu akisema kuwa hafahamu kama kuna wananchi wake wananyanyaswa na kama oparesheni hiyo ni halali.

“Sina taarifa, ninachokijua ni kwamba Ziwa lilifungwa na kufunguliwa, wavuvi wameruhusiwa kuvua kuanzia Julai mosi, 2014, na watu ambao hawatakiwi kuonekana katika pori hilo ni wakulima na wafugaji siyo wavuvi kwenda kuvua” alisema Sedoyeka.

Awali wananchi hao kuwalalamikia Tanapa kuhusika na zoezi hilo ambapo FikraPevu ilipowatafuta viongozi wa Tanapa akiwemo Afisa habari wake, Pascal Shelutete, ambaye alisema kuwa pori hilo halipo chini ya TANAPA bali lipo chini ya Idara ya Wanyamapori.

Hata hivyo Ofisi ya Idara ya Wanyamapori kitengo cha habari wamesema anayepaswa kuzungumzia suala hilo ni msemaji wa Wizara ya Maliasili na utalii, Nurdin Chamuya, ambaye alipotafutwa naye alikwepa kujibu suala na kusema anayepaswa kuzungumza suala hilo ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Wanyamapori, Paul Sarakikya, ambapo juhudi za kumtafuta kwa njia ya simu, hazikuzaa matunda baada ya simu yake ya kiganjani kuiba bila kupokelewa.

JANA AJALI LEO MAPYA::::MALORI YAFUNGA BARABARA UYOLE MUDA HUU...

Saturday, August 30, 2014

  MUDA HUU : MALORI YAFUNGA BARABARA UYOLE





ENDELEA KUFUATILIA HAPA.. TUKIO KAMILI BAADAE
Chanzo MBEYA YETU.

Friday, 29 August 2014

MBUZI WA BWANA HERI HAO!!!WANAKULA SHAMBA LA BWANA HERI

MIFUGO YANASWA IKITEMBEA BARABARANI JIJINI DAR ES SALAAM

Posted August 29, 2014
Mbuzi wakiwa kandokando ya barabara ya Kawawa.
MCHANA huu kamera yetu imewanasa mbuzi wakitembea kando ya barabara ya Kawawa, jijini Dar es Salaam eneo la Msimbazi ikiwa haina mwangalizi,  jambo ambalo ni hatari kwa watumiaji wa barabara hiyo, hasa wanaotumia vyombo vya moto.

PICHA YETU>>UNAMUONAJE DR.POMBE MAGUFULI HAPO

TANZIA!TANZIA!!!!TAARIFA ZA MSIBA WA MAREHEMU MARIAM JARUFU.

TAARIFA ZA MSIBA WA MAREHEMU MARIAM JARUFU.
Friday, August 29, 2014




Marehemu Mariam Jarufu amefikwa na umauti baada ya kupata ajali ya gari maeneo ya Gairo juzi usiku 26 August 2014. DC wa Mvomero alikuwa anapita akaona gari imedondoka upande na kama kuna mama ahangaika...ndio kusimama kukuta gari imegonga mti upande damu zimetapakaa mbele kote...akapigia simu kituo cha karibu police waje na ambulance. Wakafika mapema Mariam alikuwa hai akiongea na dereva. Nyuma watoto wazima na mama mdogo...wakatolewa kupandishwa ktk ambulance. Mariam aliumia sana kichwani na mdogo wake miguu na mwili kidogo. Ila kufika katika ambulance just 10mins drive akafariki Mariam na dereva kupoteza fahamu mpaka jana asubuhi.

Kwa watu wa UK
KUTOKANA NA MSIBA WA NDUGU YETU Mariam Jarufu ULIOTOKEA TANZANIA KWA AJALI YA GARI TUNAPENDA KUWAFAHAMISHA KUWA MSIBA UPO NO.32 COLNE TINKERS BRIDGE MILTON KEYNES MK 6 3 DJ. WOTE MNAKARIBISHWA KUTOA SHUKRAN NA RAMBIRAMBI ZENU ASANTENI

Kwa watu wa Tanzania:
 Msiba uko Mbezi Beach unapita shule ya Mwalimu Nyerere sehemu inaitwa Naguruwe ukiulizia utaonyeshwa wanazika Ijumaa makaburi ya Kinondoni

Hii ndo gari iliyo chukua uhai wa mwenzetu
Naomba tujumuike kwa pamoja kuifariji familia hii kwa msiba huu mzito. Wale watu wa UK ambao tuko Bongo na mgependa kwenda msibani basi tuwasiliane twende kwa pamoja leo jioni tukatoe pole zetu.
R.I.P MARIAM.

CCM OYEE!!!!RAIS KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BARABARA

RAIS KIKWETE AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BARABARA YA MBANDE-KONGWA 16.5KM


Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kulia akizungumza na Mbunge wa Kibakwe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa George Simbachawene huku Mbunge wa Kongwa ambaye pia ni Naibu Spika Job Ndugai akishuhudia kushoto.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakwanza kushoto akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi pamoja na Mbunge wa Kongwa ambaye pia ni Naibu Spika Job Ndugai wakifurahia mara baada ya Rais kuweka jiwe la Msingi Ujenzi wa Barabara ya Mbande-Kongwa 16.5Km .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi, Mbunge wa Kongwa ambaye pia ni Naibu Spika Job Ndugai, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Profesa Juma Kapuya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe, akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa barabara ya Mbande-Kongwa 16.5Km.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma pamoja na kikundi cha ngoma za asili cha Kibaigwa kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuhutubia mamia ya Wakazi wa Kibaigwa.
Sehemu ya barabara Mbande-Kongwa 16.5Km ambayo ujenzi wake umewekwa jiwe la Msingi.

Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katikati akizungumza na Mbunge wa Kongwa ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Profesa Juma Kapuya(kulia) kabla ya uzinduzi wa barabara ya Mbande-Kongwa 16.5Km.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya uzinduzi na ufunguzi wa barabara ya Mbande-Kongwa 16.5Km.
Viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Ujenzi pamoja na Taasisi zake wakimsubiri Rais Dkt. Jakaya Kikwete kuzindua rasmi mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Mbande-Kongwa 16.5Km. Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi

HUKO NDO KWA WAKUBWA SERIKALI JIJIN MBEYA...JIONEE BARABARA ZAO NZURI SANA...

Friday, August 29, 2014

KERO ZA BARABARA: MBEYA YETU YAMULIKIA BARABARA YA VETA , AMBAPO KUNA VIONGOZI WA KUBWA WA SERIKALI WANAISHI HUKO PAMOJA NA CHUO CHA MAFUNZO YA UFUNDI STADI VETA.

Hii ni moja ya Kero ya kakipande kadogo sana na korofi ambako wananchi wanaoishi eneo hili wamelalamika sana na kudai kuwa hakuna anayesaidia kwa njia zozote..

Mbeya yetu baada ya kupata taarifa hizo iliona ni vema na haki kutembelea eneo hilo na kujionea wenyewe ambapo mpaka sasa wenye magari wamelazimika kuikimbia barabara hiyo kutokana na kuchakaa vibaya kwa njia hiyo

hata hivyo baadhi ya wakazi wamelalamika sana kuwa njia hiyo hasa hako kakipande kadogo kamekuwa kero kubwa na kusababisha hata mataili yao ya magari kuharibika, kuisha na kuyabadilisha kila wakati
Pia Mbeya yetu ilibaini wazi kuwa kuna Chuo cha ufundi stadi cha veta na hii ikiwa ni moja ya njia kuu na ambapo katika Chuo hicho kuna zaidi ya wanafunzi Elfu mbili sasa swali likaja je hawa wanafunzi hakuna waliosomea Fani ya ukandarasi hata waje kumwaga kifusi na kuziba mashimo hayo?

Na kubwa zaidi katika eneo la barabara hiyo kuna viongozi wakubwa wa Serikali wanaishi huko akiwemo Mkuu wa Majeshi Tanzania, Waziri Asiye na Wizara Maalum, Aliyekuwa naibu Waziri wa Elimu, Viongozi wa  wa Mkoa, Pamoja na Watu wenye uwezo na Baadhi yao pia wameikimbia barabara hii.

Zifuatazo ni picha za  Baadhi ya maeneo ambayo Tochi yetu imemulikia kwa umakini.

 Hiki ndicho kipande cha barabara hiyo ambapo ndipo inapoanzia kwa kutazama unaweza ukasema ni salama lakini ukiangalia kulia kwako utagundua kama kuna shimo lililofunikwa na udongo, Eneo hilo ni mashimo ukipita vibaya unaweza acha tairi zako za Gari
 Haya ni Mawe yaliyochongoka , wengi wamepatwa na pancha katika eneo hili na kusababisha wahame njia hiyo hata kama wanaishi jirani na maeneo hayo.
 Eneo hili ni kucheza Sindimba tuu
 Hakuna Unafuu hata kidogo
 Kwanza kabisa kwa vumbi hili hapa ni hatari sana pia barabara kipande hiki inazidi kuwa mbaya zaidi 
 Hapa huwezi hata kwepa ni lazima utapita tuu na kupita kwake lazima utasababisha majanga na chombo chako cha usafiri


SWALI ... JIJI MPO? JE MMEKUONA NA HUKO.. KAMA BADO PITIENI MTAZAME

WHY THIS???WHO WILL WIN THE WAR AT THE END??

WAPIGANAJI WA ISIS WATOA ONYO LINGINE KWA MAREKANI

Posted  August 29, 2014

Mateka 15 wa Kikurd wanaoshikiliwa na wapiganaji wa ISIS.
SAA chache baada ya kuuwa wanajeshi 300 wa Syria, Kundi la wapiganaji wa ISIS limetoa onyo lingine kwa Marekani likiachia video inayowaonyesha mateka 15 wa Kikurd ambao nao watauawa iwapo Marekani haitaondoa majeshi yake.

ISIS wamesema wataendelea kuwachinja mateka hao mpaka Marekani itakapoondoa majeshi yake.
Katika video hiyo, Kundi la ISIS linaonekana likimchinja mmoja wa mateka hao wa Kikurd waliokamatwa wakati wa mapigani nchini Iraq.

Wapiganaji wa ISIS wakiwaswaga wanajeshi zaidi ya 200 waliokamatwa katika ngome ya anga ya Tabqa nchini Syria katika jangwa kuelekea eneo la mauaji