Thursday, 4 September 2014

HUZUNI YA LEO::WENGI WAMZIKA MWANAHARAKATI MAREHEMU LOVENESS T. NDIBALEMA KATIKA MAKABURI YA SABA ABA MBEYA.

04.09.2014
Marehemu Loveness Ndibalema Enzi za uhai wake
 Mwili wa Marehemu ukiwa Unaingia katika makaburi ya Saba saba Mbeya.
 Baadhi ya wachezaji wa Tanzania Prisons wakiwa wanapeleka mwili wa Marehemu katika Makaburi ya Sabasaba Mbeya
 Mtumishi wa Mungu akiwa anaomba kabla ya kuanza Ibada Fupi ya Mazishi
 Mtumishi wa Mungu ambaye pia ndiye aliyekuwa akiongoza ibada ya mazishi akisoma neno na kutoa mahubiri mafupi
 Watu mbalimbali waliofika kwa ajili ya kumsindikiza Marehemu Loveness Ndibalema wakati wa mazishi
Wa kwanza Mbele kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akiwa na Kamanda Mkuu wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi aliye nyuma ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya wakiwa katika Mazishi hayo.
 Mwili wa Marehemu ukiwa unaingizwa katika Nyumba yake ya milele
 Mtumishi wa Mungu aliyekuwa anaongoza Mazishi hayo akiweka Mchanga katika kaburi ishara ya kumzika Marehemu 
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akiweka Mchanga katika kaburi la Marehemu
 Mume wa Marehemu Loveness Ndibalema akiweka Shada katika kaburi la Mke wake 
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmad Msangi akiweka Shada la Maua katika kaburi la Marehemu
 Mmoja wa wanafamilia akisoma wasifu wa Marehemu
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akitoa nasaha wakati wa Mazishi ya Marehemu Loveness Ndibalema.
 Msemaji wa Familia akitoa neno la Shukurani wakati wa mazishi ya Marehemu Loveness Ndibalema.

Na Mbeya yetu Blog

IJUE HISTORIA NA MGUNDUZI WA 'THE MAGIC SPRAY' INAYOTUMIKA VIWANJA VYA SOKA DUNIANI

September 4, 2014
Huyu ndiye mtengenezaji wa aina mpya ya kinyunyizio ‘9-15’, Muargentina Pablo Silva.
Kinyunyizio hicho kikitumika katika baadhi ya mechi.
Aina mpya ya kinyunyizio ‘9-15’.
KWA mara ya kwanza kuona marefa wa mpira wa miguu wanabeba kinyunyizio ‘spray’ kwa wengi wetu ilikuwa ni kipindi cha Kombe la Dunia lililofanyika miezi mitatu iliyopita nchini Brazil.
Historia inaonesha jinsi gani kinyunyizio kilivyogunduliwa enzi za miaka ya 1980 na baadhi ya wachezaji kama Sir Bobby Charlton na refa Neil Midgely kuuomba uongozi wa FA kuiruhusu kutumika katika Ligi Kuu ya Uingereza bila ya mafanikio. Uzinduzi huu ulishawahi kufika mpaka ofisi za Adidas kwa muendelezo na bado wazo hili lilipigwa chini pia.
Mwaka 2000, Mbrazili mbunifu, Heine Allemagne alitengeneza /kuboresha kifaa kama hicho na kukiita “Spuni” ambayo kwa mara ya kwanza ilitumika rasmi katika ligi kuu ya nchini humo (Brazil) mwaka huo huo.
Na baada ya hapo marefa waliungana mkono katika utumiaji wa kinyunyuzio hicho na hivyo kuanza kukubalika katika mpira wa miguu huko America ya Kaskazini. Kuanzia kipindi hicho kinyunyizio hicho kilionekana kutumika katika mapambano ya kimataifa (International Football Competitions) mbalimbali.
Juni 2014 aina mpya ya kinyunyizo iliyotengenezwa na Muargentina Pablo Silva na kuitwa ‘9-15’ ikimaanisha umbali wa kupiga mpira wa adhabu ndogo na ukuta wa kuzuia, kilianza kuonekana kimataifa katika matangazo ya Kombe la Dunia 2014 yaliyotoka kufanyika miezi mitatu iliyopita licha ya kuwa na matangazo ya bidhaa hiyo tokea mwaka 2008.
Copa America ya mwaka 2011 ndiyo ulikuwa mwanzo wa kutumika kwa bidhaa hiyo kwa ngazi za kimataifa na hatimaye kuanza kutumika rasmi na ligi nyingine za nje kama MLS ya Marekani Kusini, Kombe la Dunia 2013 chini ya miaka 20, Ligi ya Uturuki, Ligi ya Mabingwa Ulaya chini ya miaka 17 na Kombe la Dunia 2014.
Ama kweli subira ya vuta heri, baada ya miaka 14 sasa kinyunyizio hicho kinatumika katika ligi kubwa zote ikiwemo Bundesliga ya Ujerumani, Seria A ya Italia, Ligue 1 Ufaransa, La Liga ya Hispania, Premier League Uingereza na A-League ya Australia.
Bwana Pablo Silva unakaribia kuwa tajiri wa kufa mtu lakini hatuna budi kukushukuru kwa uvumbuzi wa karne mpya uliotuletea. Kila la kheri.
(Na ‘Mpenda Michezo’ / GPL)

AGA KHAN YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA KWA HOSPITALI ZA HALMASHAURI 4 ZA MBEYA‏

Thursday, September 4, 2014

 Mwenyekiti wa kamati ya afya Aga Khan Mbeya (kushoto)Sultan Thawer, akitoa taarifa kabla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya tiba kwa Halmashauri nne za Mkoa wa Mbeya.
 Mwenyekiti wa kamati ya afya Aga Khan Mbeya (kushoto)Sultan Thawer, akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro kabla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya tiba kwa Halmashauri nne za Mkoa wa Mbeya.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro,akisaidiwa na Mganga mkuu wa Mkoa,Dk. Seif Mhina,Katibu tawala Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja na Mwenyekiti wa Kamati ya afya Aga Khan Sultan Thawer wakikata utepe kuashiria kukabidhi msaada wa vifaa hivyo.
 Mwenyekiti wa kamati ya afya Aga Khan Mbeya,Sultan Thawer, akipongezwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro baada ya kukabidhi msaada.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akiangalia baadhi ya vifaa vilivyotolewa na Hospitali ya Aga Khan.
 Meneja wa Hospitali ya Aga Khan Mbeya, Abel kide, ambaye pia ni mratibu wa Mradi wa tuunganishe mkono pamoja akimuonesha moja ya mashine mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro.
 Mkuu wa Mkoa na viongozi wa Aga Khan wakiangalia moja ya mashine zilizokabidhiwa kwa Halmashauri nne za Mkoa wa Mbeya.
Picha ya pamoja
Chanzo Mbeya yetu.

ONA PICHA ZA RAIS KIKWETE NA BIBI YAKE OBAMA WALIVOKUTANA NAIROBI

Posted  September 4, 2014

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Bibi yake Rais wa Marekani, Mh. Barack Obama, Mama Sarah Obama walipokutana leo kwenye hoteli ya Villa Rosa Kempiski jijini Nairobi, Kenya, wakati Rais Kikwete akijiandaa kurejea nchini. Mama Sarah Obama anatarajia kuzindua taasisi ya kusaidia elimu kijijini Kogelo nchini Kenya, alikozaliwa Baba yake na Rais Obama wa Marekani itakayofahamika kama (Sarah Obama foundation) ambapo atajenga shule kuanzia za awali mpaka sekondari. Rais kikwete sasa hivi yuko mjini Kondoa kuendelea na ziara yake ya Mkoa wa Dodoma. (PICHA NA IKULU)

Wajumbe Kundi la 201 watoa tamko dhidi ya wanaolichafua Bunge Maalum la Katiba na Wajumbe wa kundi hilo

September 4, 2014
Askofu Amos Muhagachi akitoa tamko juu ya tuhuma mbalimbali dhidi ya kundi la 201 la wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba leo 03 Septemba, 2014 katika Ukumbi wa Spika, Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa kundi la 201 ya Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Dkt. Francis Michael akikanusha kuhusu madai ya wajumbe wa kundi hilo kupewa rushwa kuhusu mchakato wa Katiba Mpya.
Sheikh Hamid Jongo akiviasa vyombo vya habari kutoa ushirikiano ili kuhakikisha kuwa mchakato wa kupata Katiba Mpya unafanikiwa kwakuwa hata wao (vyombo vya habari) unawahusu pia.

Askofu Donald Mtetemela akichangia mada wakati wa mkutano wa kutoa tamko kuhusiana na tuhuma mbalimbali dhidi ya kundi la 201.
Baadhi ya wajumbe wa kundi la 201 pamoja na waandishi wa habari wakifuatilia tamko hilo leo 03 Septemba, 2014 katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Spika Bungeni mjini Dodoma.
(Picha zote na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma)
WAWAKILISHI wa Taasisi za dini wa Bunge Maalum la Katiba toka wajumbe 201 wametoa tamko lao dhidi ya tuhuma mbalimbali zinazoendelea katika kulichafua Bunge hilo ikiwemo baadhi ya wajumbe wa kundi hilo wakituhumiwa kudaiwa kupewa rushwa.
Tamko hilo limetolewa leo 03 Septemba, 2014 na viongozi wa kiroho akiwemo Askofu wa Kikristo Amos Joseph Muhagachi pamoja na Sheikh Hamid Masoud Jongo wakiwa wameongozana na Mwenyekiti wa kundi hilo la 201, Mhe. Dkt. Francis Michael na wajumbe wengine wa kundi hilo, wakati walipofanya mkutano na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Spika uliopo Bungeni mjini Dodoma.
Akisoma tamko hilo, Askofu Amos Muhagachi ambaye pia ni Mjumbe wa kundi hilo amesema kuwa kama ilivyoelezwa hapo awali kabla ya kuanza kwa shughuli za Bunge hilo, kila mjumbe alikula kiapo cha kuwa mwaminifu na mtiifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa kadiri ya uwezo wake na ufahamu wake, kufanya kazi zinazomhusu bila upendeleo.
Askofu Muhagachi ameendelea kusema kuwa wameshangazwa na kusikitishwa kuona kwamba mchakato wa kutayarisha Katiba itakayopendekezwa na Bunge hilo kwa wananchi unachafuliwa taswira yake, Bunge Maalum la Katiba linachafuliwa, shughuli zake kuingiliwa na kupotoshwa na wajumbe wenzao walioko nje ya Bunge hilo, makundi, taasisi na vyombo mbalimbali vya habari, uhalali na ukweli wa shughuli za Bunge hilo unapotoshwa na wananchi wanaaminishwa mambo yasiyo na ukweli.
Upotoshwaji huu umezua mijadala mbalimbali katika jamii ya Watanzania bado unaendelezwa”, alisema Muhagachi.
Aidha, Muhagachi amezitaja baadhi ya tuhuma zinazotolewa na wajumbe wenzao dhidi ya Bunge hilo na wajumbe wa kundi hilo zikiwemo.
Bunge Maalum la Katiba halina uhalali kwa kuwa hao wajumbe wenzetu walioondoka wameliondolea uhalali wake kwa vile hawapo, kwamba Kanuni za Bunge Maalum la Katiba zinavunjwa ovyo ovyo, Kwamba kinachojadiliwa sasa katika Bunge hili ni Waraka mwingine na si Rasimu iliyotayarishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Inadaiwa na watu pamoja na Taasisi mbalimbali kwamba viongozi wa dini, wajumbe wa Bunge hilo na wajumbe wa kundi la 201 kwamba wanapewa rushwa baadhi ya Vyombo vya Habari vimeandika tuhuma hizi, pia madai mengine ni kwamba wajumbe waliomo katika Bunge hili ni wachache ikilinganishwa na hao waliopo nje ya Bunge na tuhuma ya nyingine ni ile ya kwamba Bunge hili lazima lisitishwe au livunjwe na Mhe. Rais.
Tunapenda kuwafahamisha Watanzania wenzetu kwamba mchakato wa Katiba una hatua tatu kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na mpaka hivi sasa ni hatua moja iliyokamilika, aidha hatua ya pili ndiyo inayoendelea na hatua ya tatu bado haijaanza”, alisema Muhagachi.
Akitoa tamko hilo, Askofu Muhagachi amesema kuwa wao kama wawakilishi wa Taasisi za Dini, ambao kuuhubiri, kuutangaza na kuusimamia ukweli ni moja ya majukumu yao katika jamii, hivyo wameskitishwa na taarifa potofu zinazosambazwa kwa makusudi na makundi, taasisi na baadhi ya vyombo vya habari.
Tukiwa kama wajumbe wa Bunge hili ambao tunafahamu kwa kina na tunaridhika na kila hatua ya mchakato huu, tuna wajibu wa kusahihisha upotofu huu unaoendeshwa kwa makusudi na hivi kuwaeleza Watanzania ukweli na hali halisi inayojiri hapa Bungeni, Watanzania msifadhaishwe na wala msibabaishwe, hali ni shwari, mchakato unaendelea kwa amani na utulivu”, alisisitiza Muhagachi.
Naye Sheikh Hamid Masoud Jongo ameviasa vyombo vya habari kutilia mkazo katika kutoa taarifa zilizosahihi ili mchakato wa Katiba uendelee kwa amani kwani nao ni moja ya kundi la watu inayowahusu.
Vyombo vya habari vina nguvu ya kuhabarisha umma juu ya mambo mengi yanayoendelea nchini, ni vema tukishirikiana sote kwa pamoja ili kuhakikisha kuwa tunapata Katiba yetu kwani hata nyie Katiba hii inawahusu hasa katika kudai haki na uhuru wa vyombo vya habari”, alisema Sheikh Jongo.
Aidha, Mwenyekiti wa wajumbe wa Kundi hilo la 201, Mhe. Dkt. Francis Michael ameongezea kwa kukanusha suala la rushwa kwa wajumbe wake huku akisisitiza kuwa wajumbe wake katika kundi hilo ni watu wenye heshima zao hivyo madai hayo hayana ukweli wowote ule.

Wednesday, 3 September 2014

HII NDO iPHONE6 ITAKAVOKUA...PICHA ZILIZOVUJA MTANDAONI

PICHA ZA iPHONE 6 ZAVUJA MITANDAONI

Posted September 3, 2014
Muonekano wa iPhone 6 itakapokuwa kwenye Apple Stores.
 Ukubwa wa iPhone 6 utakavyokuwa.
 iWatch itakavyokuwa.
Eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya uzinduzi huo.
PICHA za simu mpya kutoka kampuni ya Apple aina ya iPhone 6 zimevuja mtandaoni ikiwa ni siku chache kabla ya kuzinduliwa rasmi nchini Marekani.
Picha hizo zimeonyesha simu hiyo ambayo itaitwa iPhone Air itakayokuwa katika urefu wa aina mbili inchi 5.5 na inchi 4.7.
Uzinduzi wa simu hiyo utakuwa sambamba na uzinduzi wa saa iitwayo iWatch na vyote vitafanyika Jumanne ijayo ya Septemba 9, mwaka huu katika eneo ambalo marehemu Steve Jobs alizindua kompyuta aina ya Mac miaka 30 iliyopita.
Simu hiyo itakuwa na kioo chenye ‘Retina display+’, sensa ya mapigo ya moyo, uwezo wa kuichaji bila waya 'wireless charging support' na vinginevyo.

KUTOKA BUNGENI....Matukio katika Picha Bunge Maalum la Katiba Mjini Dodoma 03 Septemba, 2014.

September 3, 2014

Baadhi ya Wajumbe toka Kamati mbalimbali wakiendelea kuwasilisha taarifa za Kamati zao katika Bunge Maalum la Katiba leo 03 Septemba, 2014 Bungeni Mjini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza Bunge Maalum la Katiba leo 03 Septemba, 2014 Bungeni Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta (kulia) akiteta jambo na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru wakati wa Bunge Maalum la Katiba leo 03 Septemba, 2014 Mjini Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakifuatilia uwasilishwaji wa taarifa toka katika Kamati mbalimbali leo 03 Septemba, 2014 Bungeni Mjini Dodoma.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria Bunge Maalum la Katiba leo 03 Septemba, 2014.
     na fredy mgunda

#Exclusive: Diamond Platnumz azungumza kwa mara ya kwanza mambo 6 kuhusu fujo zilizotokea Ujerumani

Screen Shot 2014-09-01 at 12.16.12 AM 

Kuanzia siku tatu zilizopita stori kubwa kwenye kiwanda cha burudani Tanzania imehusu fujo zilizotokea Ujerumani kwenye show aliyokwenda kufanya Diamond Platnumz huko Stuttgart.
Kilichotokea ni kwamba saa kumi alfajiri ndio promota alimpeleka Diamond kwenye ukumbi kunakofanyika show. Kwa nini ilitokea akamchelewesha? nini kilitokea baadae? hizi hapa chini ni kauli za Diamond mwenyewe kwenye exclusive na millardayo.com
1. ‘Mpaka sasa hivi nashindwa kuelewa tatizo lilikua nini, siamini kama tatizo lilikua ni hela, balance iliyokua imebaki ni balance ndogo kama EURO 3500 hivi ambazo ni zaidi ya milioni 7 za Tanzania, ninavyojua Mapromoter wengi wa nje wakifanya show huwa wanauza na vinywaji wenyewe na wanapata hela nyingi sana kwenye vinywaji kuliko hata viingilio so nahisi labda walivuta muda ili waendelee kuuza vinywaji zaidi’
2. ‘Walichelewa kunipeleka kwenye show, walinifata kwenye mida ya saa tisa usiku na wakawa hawana hela yangu iliyobaki, nikawaambia siendi kokote mpaka wamalize kunilipa, walikua na EURO 1500 wakati nilikua nawadai 3500 nikawaambia lazima wanipe hela yote, wakaifata ndio tukaenda kwenye show’
Screen Shot 2014-09-01 at 12.16.38 AM3. ‘Tukafika kwenye show saa10 kasoro, kweli hata ningekua mimi shabiki ningekasirika ningefanya vurugu, wengine walilipa zaidi ya laki moja na wametoka kwenye miji na nchi jirani, niliwaambia wanipeleke nikafanye show ndani ya ukumbi japo tulikuta watu wengi sana nje lakini Mapromota walikua waogawaoga kunipeleka ndani’
4. ‘Nikakuta watu wengi na vurugu nje, nikamwambia promota atupeleke ndani tungefika kwenye stage ingetulia baada ya sisi kuimba manake ni vitu tunakutana navyo kwenye muziki lakini promota walikua waogawaoga, askari wa Ujerumani karibu gari 7 wakaja pale lakini mtiti ukawa mkubwa’
5. ‘So dakika ya mwisho tukaona hapashukiki ndio wakaturudisha hotelini, kiukweli nimesikitishwa sana manake nilikua nimejipanga vizuri na ilikua ni mara yangu ya kwenda kuperform pale Stuttgart, imenisikitisha manake watu walikua kuniona alafu mwisho ikashindikana kuwafikishia walichokitarajia’
Screen Shot 2014-09-01 at 12.16.59 AM 
6. ‘Nafikiri October tutakua na show nyingine na itafanyika kulekule, nilikua nazungumza na uongozi wangu kwamba wanataka show nyingine na tayari wameshatuma hiyo hela ya show nyingine’ .

UMEIPATA HIYO....Meya wa Italia amuandikia Yesu barua

Meya wa Italia amuandikia Yesu barua

 3 Septemba, 2014
Meya Giovanni Calabrese
Meya wa mji mmoja nchini Italia ameghadhabishwa mno na kile alichotaja kuwa uzembe na uvivu miongoni mwa wafanyikazi wa baraza lake la jiji.
Na ameamua kuchukua hatua anayoamini itawatia adabu.
Ameandika barua ya wazi ya malalamiko kwa Yesu Kristu. Amesema katika barua yake anaomba miujiza kutoka mbinguni kuwasaidia wafanyikazi hao na kuokoa mji wake.
Mji huo mdogo uitwao Locri uko chini kusini mwa pwani ya Uitaliano, wengine wakitania wakisema uko kidole gumba cha mguuni mwa uitaliano.
Kweli hautarajiwi kuwa na shughuli nyingi lakini meya wa mji huo Giovanni Calabrese asema kuna mipaka, imetosha,Uvivu umekithiri.
Katika barua yake anayosema amemwandikia Yesu Christo ili auokoe mji huo anataja matatizo mawili makuu.
Genge la mjini humo la kimafia na pili wengi wa wafanyakazi wa mji huo ambao amewataja kuwa ni wavivu .
Anafafanua kuwa ni wafanyakazi wachache mno ambao wanatekeleza kazi zao ipasavyo, waliosalia hukaa tu , wakiangalia, wakisubiri ujio wa hundi yao ya malipo ya mshahara ambao hamna kazi yoyote walioufanyia.
Mayor Giovanni anamlalamikia Yesu kuhusu hasa mahudhurio ya mashaka ya wafanyikazi hao - wengi wakiwa na tabia ya kutoa vijisababu vya kukosa kufika kazini.Hata baadhi yao kusingizia magojwa ya ghafla ili kukwepa zamu zao kazini.
Kisha barua hiyo yachukua mkondo wa kufoka, meya huyo akielezea jinsi alivyong'ang'ana angalau kurudisha huduma ya taa za barabarani zilizokuwa zimeharibika huku ndani ya maghala ya baraza hilo kukiwa na taa mpya yaani balbu zipatazo 15,000... Na mji unabaki kuwa kiza !
Barua ya Meya Giovanni haikuishia hapo amewatia pia lawamani polisi wa baraza hilo la mji wa Locri -kwamba wamezembea --- kwa maneno yake halisi anasema wamelala - kwa sababu wameshindwa kutoza faini madereva wasio na nidhamu barabarani ambako uendeshaji magari kiholela umeshamiri.
Hadi sasa hamna aliyetoa jibu lolote la hadharani kuhusu barua hiyo lakini ukitathmini hisia kali zilizojaa kwenye barua hiyo ya meya Giovanni huenda wakakosoa mtindo wake huo wa uongozaji wa baraza hilo.

HII NDO KICHENI PATI YA LUCY KOMBA...FUNIKO...

Posted by GLOBAL on September 3, 2014
Stori: Imelda Mtema
NI mshangao! Sherehe ya kicheni pati ya staa wa filamu Bongo, Lucy Komba imewashangaza waalikwa wengi baada ya kutawaliwa na vitu vingi vya kiasili tofauti na matarajio ya wengi.
Staa wa filamu Bongo, Lucy Komba.
Sherehe hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta jijini Dar ambapo mbali na watu wa kawaida, wake wa viongozi mbalimbali nchini pamoja na baadhi ya wasanii wa Bongo Movies walihudhuria.
Miongoni mwa matukio ambayo yaliibua mshangao kwa waalikwa ni bibi harusi mtarajiwa (Lucy) kutinga ukumbini hapo akiwa ndani ya baiskeli yenye magurudumu matatu (guta) akiwa na wapambe wake ambao walikuwa peku miguuni.
Kwenye guta hilo lililotengenezewa kibanda cha asili kilichowekwa nyasi juu, Lucy alikaa ndani yake huku wapambe wake wakiwa wameshika nyungo ndogo kuashiria asili ya Mtanzania.
Akiwa kwenye usafiri wa baiskeri ya matairi matatu maarufu kama 'Guta'.
Kama hiyo haitoshi, Lucy aliwaacha hoi waalikwa kutokana na vazi lake ambalo ni tofauti na wanavyovaa wengine katika sherehe kama hiyo kwani alitinga kipensi kifupi kwa ndani chenye rangi ya bendera ya Tanzania huku kwa nje kikifunikwa na kitambaa chepesi.
“Ama kweli hii ni ya aina yake, hebu angalia nguo yake alivyoitengeneza kwa kweli inavutia sana, full utamaduni,” alisikika mmoja wa watu walioudhuria sherehe hiyo.
Ulipofika wakati wa kufungua shampeni, nayo ilikuwa ya aina yake. Aliandaliwa pombe ya kienyeji ya mkoani Ruvuma ijulikanayo kama Kangara ambayo aliiweka ndani ya kibuyu kidogo huku akipita kugongesha na wageni waalikwa.
Akiingia ukumbini kwa mbwembwe.
Baadhi ya marafiki zake waliotoka nchi mbalimbali akiwemo muigizaji kutoka nchini Italia, Angela Howell, alidondosha chozi la furaha alipoona waalikwa wanakula ndafu badala ya keki kama ilivyozoeleka na wengi.
Lucy Komba anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni na mchumba wake aitwaye Stanley, raia wa Denmark. Watafanya sherehe kubwa Bongo na baadaye kuangusha nyingine Denmark.