Tuesday, 9 September 2014

HATARI TUPU...UNADHANI BARABARA HII TRAFFIKI ATAKIMBIA AU ATAKIMBILIA?JIONEEE


Mbeya yetu iliwashuhudia Abiria hawa bila Kujali hatari wakiwa wanajipanga kupanda katika Gari la Mizigo huku kukiwa na usafiri wa usalama na wakutosha kabisa. Wakina mama wengine walikuwa na Watoto wao bila kujali afya zao kwa kuwa barabara hiyo ilikuwa na vumbi la kutosha.
Askari wa usalama barabarani akiwa kazini
Askari wa usalama barabarani akitumia mamlaka yake kulisimamisha Gari lililoshehena Mizigo na Abiria Juu
Hata hivyo uchunguzi umebaini Bajaji kubeba abiria ili kulisubiria Lori mbele kama inavyo onekana Pichani.
Cha Kushangaza zaidi hakuna abiria aliyeshushwa wala mizigo na kuamriwa kuendelea na Safari , Je hapa tuseme ni usalama wa barabarani au ni Hatari barabarani 
Kwa Furaha Abiria walioshushwa na Bajaji wakisubiri Lori kwa matumaini ili kuendelea na Safari yao.
Safari inaendelea bila wasi wasi kila Lori na Safari yake na kwa nafasi
Mizigo Imesheena na abiria wamesheena
Safari inaendelea bila wasi wasi ambapo Tulibaini kwa ukaribu kabisa Gari la kwanza la Mizigo likipita Ishara kuonesha kuwa liliruhusiwa pasipo na Pingamizi
Lori la pili nalo linapita nalo bila wasiwasi , Tazama hapo juu huyo abiria wa mbele alivyo jiegesha je Kuna tahadhari yotote hapa? Hapa pia tulibaini Askari wa usalama wa barabarani aliliruhusu bila kipingamizi
Na Hatimaye huku mbele tukashuhudia Mistubishi ambayo tuliiona ikiwa imesimamishwa na Askari wa usalama wa Barabarani nayo ikipita tena ikiwa na watu wengi ndani yake mpaka wengine hawajakaa  vizuri kama wanavyo onekana a


WAKATI Serikali na wadau mbali mbali nchini wakihaha kuepusha ajali zinazoendelea kuangamiza roho za watu, hali imekuwa tofauti kwa baadhi ya madereva na wamiliki wa vyombo vya usafiri.
Ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani umejitokeza mara nyingi Barabara za Mbeya-Chunya kupitia Kawetele na Mbeya-Mkwajuni Kupitia Mbalizi ambapo yamekuwa yakibeba abiria na mizigo licha ya kuwepo mabasi yaliyoruhusiwa Kisheria.

 Mbeya yetu imeshuhudia  magari matatu aina ya Fuso na Scania kubeba mizigo na kuning’iniza abiria juu jambo linalohatarisha usalama wa abiria na mali zao.
Magari hayo yalikutwa hivi karibuni  yakitokea jijini Mbeya na kuelekea Wilayani Chunya majira ya saa Tisa alasiri huku wasimamizi wa sheria za usalama barabarani na Sumatra wakiyaruhusu kuendelea na safari licha ya kuyaona yakifanya safari zake kila siku.
Mbeya yetu ilishuhudia magari hayo yenye namba za usajili T 168AZG aina ya Fuso, T 432 AAK aina ya Scania na T 646 BRQ aina ya Mitsubishi Fuso yakiwa yanapita barabarani eneo la Mwansekwa na kuyashuhudia yakipita Lwanjiro kwa ishara kuwa yaliruhusiwa kuendelea na safari.

Hata hivyo usalama wa abiria hao umekuwa mashakani licha ya Serikali kuimarisha barabara ya Mbeya-Chunya na kuwepo kwa magari ya abiria Lukuki yanayofanya safari zake kila siku na Sumatra kuamua kupunguza Gharama za usafiri. Ambapo awali walikuwa wakitozwa Tsh 10,000 kati ya Mbeya na Chunya na sasa nauli imefikia hadi Tsh 5,000. 
Hali hii Hatari huwa mbaya zaidi wakati wa minada inayofanyika maeneo mbalimbali katika Wilaya ya Chunya na Magari hiyo yamekuwa yakipita pembezoni mwa kituo cha Polisi cha Wilaya hiyo.


CHANZO:MBEYA YETU BLOG.

King Mswati Noma Sana Aongeza Mke Mwingine Bikira, Sasa Ana Wake 14 , Angalia Picha





KING Mswati Mfalme wa Swaziland amefikisha wake kumi na nne 14 baada ya juzi jumatatu kumchagua mke mwingine mwenye umri wa miaka 19 masharti ya mwanamke anaetakiwa kuchaguliwa ni sharti awe bikra.

Takribani wasichana 80,000 walipita mbele ya wageni wa heshima 46 ambapo na mfalme alikuwa ameketi mbele akiwa kaketi na malkia aliechaguliwa mwaka jana LaFogiyane Baadhi ya wasichana wanakimbia katika taifa hilo kutokana na sheria hizo.

Wasichana hao hupita wakiwa nusu uchi ndipo mfalme anachagua mke wake kafikisha wake 14

DIAMOND ANAYAJUA HAYA???AU WEMA ALIPOZI TU NA PREZZOOO

Hivi karbuni wema na dangote wamekua hawaelewani katika mapenzi yao, na sasa kuna uvumi mwingi mitaani hizi ni baadhi ya picha za wema akiwa na prezzoo wa kenya zilizowashtua wengi kwani prezzo anajulikana kwa tabia ya kupenda mastaa hivyo watu kubaki na maswali kulikoni picha hizi






HAYA NDO MADHARA YA KULA CHIPS KWA AFYA YAKO


Kama moja ya njia ya kupunguza gharama za matumizi, watu wengi wanatumia mafuta yaleyale zaidi ya mara moja kukaangia vyakula mbalimbali.

Jambo hili linafanywa sehemu mbalimbali kama vile nyumbani, migahawani, hotelini, shuleni na zaidi mitaani kwa wakaanga shipsi, mihogo, mandazi, samaki na kitimoto.

Watu wanaotumia mafuta zaidi ya mara moja inawezekana wanafuata mazoea na kijamii lakini kwa kujua ama kutojua hatari za hulka hiyo kiafya.

Mtu anavyotumia mafuta zaidi ya mara moja, ubora wa mafuta hayo unapungua. Mafuta yenye ubora mdogo yakitumika kukaangia vyakula yananyonywa mengi katika vyakula.

Mtu akila vyakula hivyo atapata uzito kupita kiasi, lehemu kwa wingi na shinikizo la damu. Vitu ambavyo vyote vinachochea ugonjwa wa kisukari na magonjwa ya moyo.   Zaidi ya hayo, mafuta yaliyotumika kukaangia vyakula huwa yana mabaki ya vyakula. Mafuta hayo yakipoa vijidudu vya bakteria watakula mabaki hayo na kuzaliana kwa wingi.

Mafuta yenye mabaki ya vyakula yanapokosa hewa huwa yanaweza kuwa na mazingira mazuri ya bakteria aina ya “Clostridium botulinum” kuzaliana.

Bakteria wa aina hiyo anasababisha ugonjwa hatari unaotokana na ulaji wa vyakula vyenye sumu unaoitwa “botulism”.

Kuyahifadhi mafuta katika friji au friza unapunguza bakteria kuzaliana. Lakini watu wa namna hiyo kwenye jamii huwa wanayahifadhi tena wakati mwingine kwenye mazingira machafu.

Mtu anavyotumia mafuta kukaanga vyakula zaidi ya mara moja, uwezo wa mafuta hayo kuhimili joto unapungua na yanaweza kuzalisha kemikali kama vile zinazoitwa “freeradicals” ambazo zinaweza kuharibu ubora wa chakula na kuharibu chembehai na kuongeza uwezekano wa mtu kupata ugonjwa wa saratani.  Mafuta yanayotokana na mimea yanahimili zaidi joto wakati wa kukaanga vyakula kuliko yale yanayotokana na wanyama.

Mafuta yaliyosafishwa pia, yanahimili zaidi joto kuliko yale yasiyosafishwa. Mafuta ya aina hiyo ndiyo yatumike.

Mafuta yaliyosafishwa ya zaituni (olive), jamii ya karanga, soya na alizeti ni miongoni mwa yale yenye uwezo mkubwa wa kuhimili joto kali na hivyo ni mazuri kwa matumizi ya kukaangia vyakula.

Kwa usalama wa afya na ubora wa vyakula vitakavyo kaangwa, watu wanashauriwa kutumia mafuta mapya kila wakati wanapokaanga vyakula.

Hata hivyo, uzoefu unatuonyesha kuwa kwa watu wanaokaanga kiasi kikubwa cha vyakula ndani ya chombo chenye mafuta mengi, siyo rahisi kila wakati kutumia mafuta mapya kwani ni gharama na inaweza kusababisha hasara.

Mafuta yanaweza kutumika zaidi ya mara moja kukaangia kwa masharti yafuatayo. Mtu anapokaanga vyakula asitumie moto mkali sana kwa sababu utaharibu mafuta na chakula anachokiandaa.

Hii haina maana kuwa atumie moto mdogo kiasi ambacho chakula hakitaiva na kushindwa kuua vijijidudu vilivyomo katika vyakula vibichi.

Mtu asichanganye mafuta mapya na yale yaliyotumika. Vyakula visiwekwe chumvi nyingi ili kulinda nguvu ya mafuta kuhimili moto.

Mafuta yakipoa, yachujwe haraka kwa kutumia kitambaa safi ili kuondoa mabaki ya vyakula. Mafuta yafunikwe na kuhifadhiwa katika chombo safi.

Sunday, 7 September 2014

7 WAHUKUMIWA KIFO KWA UBAKAJI AFGHANISTAN

Posted September 7, 2014
Mmoja wa watuhumiwa hao waliohukumiwa kifo.
Hukumu hiyo wakati ikitolewa.
WANAUME saba nchini Afghanistan, leo wamehukumiwa kifo baada ya kubainika kuwa waliwabaka kwa zamu wanawake wanne waliokuwa wakitoka harusini Agosti 23, mwaka huu nje ya mji mkuu wa nchi hiyo, Kabul.
Hukumu hiyo inajiri baada ya kesi iliyochukuwa masaa mawili na nusu ambapo wawili kati ya saba hao walikana madai hayo.
Wanaume hao wakiwa wamevaa nguo za polisi Agosti 23, 2014 waliwavamia msafara wa watu waliokuwa wakitoka harusini eneo la Mji wa Paghman, karibu na Kabul na kuwatoa wananwake wanne kisha kuwabaka na kuwaibia kwa mabavu.
Hukumu hiyo ya kifo ilitolewa kwa kosa la wizi wa mabavu huku hukumu ya miaka kumi na tano ikisimamia ubakaji.
Rais Hamid Karzai aliunga mkono wito wa watu hao kunyongwa hadharani iwapo watapatikana na makosa.
HABARI: BBC

PICHA YA LEO:::MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA


               BAADHI YA WANANCHI WA KATA YA MIGOLI

MAMBO YA SIASA:::ZUBAA UCHEKWEE...WANNE WA CHADEMA WAENDA CCM IRINGA...

September 7, 2014


 KATIBU WA CCM MKOANI IRINGA HASSAN MTENGA AKIWAHUTUBIA WANANCHI WA MIGOLI
MMOJA YA VIJANA WAOJIUNGA NA CCM NA KUACHANA NA CHADEMA ANAITWA  BENI HOYA AKIWA NA KATIBU WA CCM MKOA WA IRINGA HASSANI MTENGA
 MTENGA AKIIPOKEA KADI YA WAPINZANI KUTOKA KWA BENI HOYA WA KATA YA MIGOLI
               BAADHI YA WANANCHI WA KATA YA MIGOL 

Akiwahutubia wananchi wa kata ya migoli katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa iringa HASSANI MTENGA amewataka wananchi wa kata ya migoli wilaya ya iringa vijijini kuwa makini katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni na kuongeza kuwataka kuungana katika kazi za kimaendeleo ili kuleta maendeleo ya kata hiyo.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katibu huyo amesema kuwa wananchi wa migoli wanahitaji maendeleo na kuongeza kuwa hawatakuwa na maendeleo ikiwa na migogoro baina yao itaendelea na kuwataka wananchi kukaa pamoja na kuijenga kata hiyo.

Hata hivyo baadhi ya vijana wapatao wanne wa kata hiyo waliamua kurudisha kadi zao za chama upinzani cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA)kutokana na maneno makali yenye ukweli wa maisha ya mtanzania yaliyotolewa na katibu chama cha mapinduzi mkoani iringa.

Kwa upande wake diwani wa kata hiyo HESSEINI KISWILI amesema kuwa toka ameingia madarakani amefanikiwa kuboresha sekta ya elimu na kuwafanya wanafunzi wa kata hiyo kusoma kwa utulivu na mazingira yaliyo salama.

Aidha KISWILI ameongeza kuwa upande wa afya nako wameboresha na kuokoa maisha ya wananchi wa kata hiyo kwa kuwapa gari la kubebea wagonjwa na kupunguza vifo vya akina mama ambavyo vilikuwa vikitokea hapo awali na kuongeza kuwa wafamenya kazi kwa kujenga nyumba za waganga sehemu zote zenye huduma ya afya.
Wakizungumza baada ya kujiunga na chama cha mapinduzi vijana hao walisema kuwa vijina wengi wamekuwa wakiiga mikumbo na kuingia kwenye vyama vya upinzani bila kujua faida na hasara za kuingia huko 
 
vijana hao wameongeza kuwa wamekuwa wakijiingiza kwenye maandamano yasiyo na faida kwao na kusababisha kurudisha maendeleo nyumba hivyo wamewaomba vijana wengine kufanya maendeleo na kuacha kuandamana basipo sababu za kuleta maendeleo
MWISHO.
NA FREDY MGUNDA

Benki Kuu ya Tanzania imetoa toleo jipya la sarafu ya shilingi 500

September 7, 2014

Mkurugenzi Huduma za Kibenki kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Bw. Emmanuel Boaz(wa kwanza kulia) akiwaeleza waandishi wa habari(Hawapo Pichani) sababu zilizopelekea kutoa toleo jipya la sarafu ya shilingi 500, ambapo alisema noti ya shilingi 500 inatumika zaidi kwenye manunuzi ya kawaida ya kila siku hivyo hupita kwenye mikono ya watu wengi na kuchakaa haraka,noti hizi hukaa katika mzunguko kwa muda mrefu bila kurejeshwa kwenye mabenki na sarafu hukaa kwenye mzunguko kwa muda mrefu kuliko noti. Katikati ni Mshauri wa Fedha kutoka ofisi hiyo Bw. Hassan Jarufu na Mwisho ni Meneja Msaidizi, Sarafu Bw. Abdul Dola.

 Mkurugenzi Huduma za Kibenki kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Bw. Emmanuel Boaz (kulia) na Mshauri wa Fedha kutoka ofisi hiyo Bw. Hassan Jarufu wakiwaonesha waandishi wa Habari(Hawapo Pichani) Toleo jipya la sarafu ya Shilingi 500 inayotarajiwa kuingizwa kwenye mzunguko kuanzia mwezi Oktoba 2014.
Picha na Hassan Silayo-MAELEZO



Na Frank Mvungi MAELEZO
Benki Kuu ya Tanzania imetoa toleo jipya la sarafu ya shilingi 500 itakayoanza kutumika Oktoba 2014 itakayokuwa mbadala wa Noti ya shilingi 500 inayoonekana kuchakaa haraka.
Hayo yamesemwa  leo Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Huduma za kibenki wa benki hiyo Bw. Emmanuel  Boaz  wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
“Noti ya shilingi 500 hupita kwenye mikono ya watu wengi zidi na ndiyo inayotumika zaidi kwenye manunuzi ya kawaida hivyo kuchakaa haraka ndio maana tumeamua kutoa toleo la sarafu itakayoanza kutumika mapema mwezi wa 10 mwaka huu.”alisema Boaz.
 
Akifafanua zaidi Boaz amesema Sarafu hukaa kwenye mzunguko kwa miaka mingi zaidi kuliko noti na pia noti zimekuwa zilikaa katika mzunguko kwa muda mrefu bila kurejeshwa kwenye mabenki kwa wakati muafaka ili zibadilishwe.
Akitaja sifa za sarafu hiyo mpya Boaz amesema kwanza umbo lake ni la duara lenye michirizi pembezoni na kipenyo cha milimita 27.5 na uzito wa gramu 9.5.
Sifa nyingineni kuwa ina rangi ya fedha na imetengenezwa kwa madini aina ya chuma na Nickel na kwa upande wa mbele ina sura ya Rais wa kwanza wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar sheikh Abeid Aman Karume na kwa nyuma ina taswira ya mnyama nyati akiwa mbugani.
Pia Boaz alibainisha kuwa sarafu hiyo kwa upande wa  nyuma ina kivuli kilichojificha ambacho huonesha thamani ya sarafu ya 500 au neno BOT inapogeuzwa geuzwa.
Kwa upande wa matumizi Boaz amesema sarafu hiyo itakapoanza kutumika itatumika sambamba na noti za shilingi 500 hadi zitakapokwisha kwenye mzunguko.
Benki  Kuu ya Tanzania ndiyo chombo chenye jukumu la kutoa sarafu na noti halali (legal tender) zinazotumika  nchini ambapo katika kutimiza jukumu hili Benki kuu hutengeneza noti na sarafu zenye uwiano mzuri wa thamani (denomination) unaozingatia uwezekano wa zile zenye thamani kubwa kuweza kugawika katika zile zenye thamani ndogo.

HABARI NJEMA KUTOKA HESLB:::FEDHA ZA VITENDO ZA PELEKWA VYUONI.

VYUO VYOTE SASA VYAPELEKEWA FEDHA ZA MASOMO KWA VITENDO

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk Shukuru Kawambwa.
Vyuo vyote nane ambavyo vilichelewa kupatiwa fedha za mafunzo kwa vitendo vimepatiwa fedha hizo na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania, (Tahliso), Musa Mdede, vyuo vinne vilivyopatiwa fedha hizo wiki iliyopita na kumaliza mgogoro kati ya Tahliso na Bodi ni Tumaini Makumira- Iringa, Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo Kikuu Kishiriki cha Kumbukumbu ya Stefano Moshi (SMUCCO), Chuo Kikuu cha Jordani (Morogoro), Saut (Mwanza) na Saut Tabora.

Alisema vyuo ambavyo vilipatiwa fedha hizo Agosti 23, mwaka huu ni Chuo Kikuu Teophilo Kisanji (Teku), Chuo Kikuu cha Katoliki cha Sayansi , Afya na Tiba-Bugando (CUHAS-Bugando) kwa wanafunzi wa fani ya udaktari wa mwaka wanne.

Kwa mujibu wa chanzo ndani ya HESLB, tayari fedha hizo zilipelekwa kwa vyuo hivyo vitatu Jumanne iliyopita na kwamba iwapo hazijafika itakuwa ni tatizo katika benki walikopeleka.

Mapema wiki iliyopita, HESLB ilisema bado inaendelea na utaratibu wa kukamilisha malipo ya fedha kwa vyuo vilivyobaki, baada ya kukamilisha kwa vyuo vitatu.

Kabla ya kutolewa kwa fedha hizo, Tahliso walikuwa wametangaza mgogoro na  HESLB kutokana na kucheleweshewa fedha hizo wanazodai kuwa ni Sh. bilioni 6.6.
CHANZO: NIPASHE

GARDNER G HABASH:::"HATUNA TATIZO" Haya wapambe..shiiiiiiii

Tetesi za Kuachana na Lady Jay Dee na Chanzo Chake, 'Hatuna Tatizo'

Gardner G Habash amekanusha taarifa zilizokuwa zimesambazwa kwenye mitandao kuwa yeye na mkewe Lady Jay Dee wako kwenye wakati mgumu wa ndoa yao.

Akizungumza katika Exclusive Friday ya 100.5 Times Fm, Gardner ameeleza kuwa hizo ni taarifa zisizo za kweli ambazo amekuwa akizisikia tu.

“Hakuna tatizo. Kusema ukweli nimekaa na Lady Jay Dee kwa miaka mingi sana na hii sio mara ya kwanza kuzungumzwa kwa mambo kama hayo. Na tumeshazoea. Hata kama kuna kitu kinazungumzwa, mimi hata sina habari kwa sababu nimeshazoea. Kwa hiyo na mimi pia nimesikia kama ulivyosikia wewe. Lakini tatizo hakuna.” Amesema Gadner.

Ameeleza kuwa chanzo cha tetesi hizo kinaweza kuwa siku ambayo yeye alionekana polisi  katika kesi ya usalama barabarani na Lady Jay Dee hakufika.

Amesema huenda watu walichukulia tofauti lakini ukweli ni kwamba yeye ndiye aliyemshauri asiende ili kuepusha attention zaidi.

Na kwa watu kuzungumza…unajua Jay Dee ni mtu mashuhuri, ni mkubwa sana. Kiasi kwamba kitu kidogo tu kikitokea, hata akijikwaa kinazungumzwa kwa ukubwa huo. Kwa mfano mimi nimepata shida kidogo ya kesi ya traffic, kwa hiyo nikamshauri mwenzangu asije pale polisi kwa sababu ya kuogopa tu vitu kama mapicha na nini. Kumbe watu walinotice kwamba hakuja. Kuanzia hapo ndio ikaanza ‘aah kuna tatizo..kuna tatizo’.

Lakini kwa kweli kuzungumzwa kwa msanii mkubwa kama yule ni jambo la kawaida. Na ni jambo ambalo ameshalizoea na mimi nimeshalizoea pia.”

Hivo karibuni Jide alipost picha ya mkono inayoonesha pete yake ya ndoa kumaanisha uimara wa ndoa yao tofauti na kilichokuwa kikisemwa.

URAIS!URAIS!URAIS!!!!!!!!SIO KAZI RAHISI...DR.KIGWANGALA NAE ATANGAZA NIA

MBUNGE WA JIMBO LA NZEGA DK KHAMIS KIGWANGALA ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS 2015

Posted by GLOBAL on September 7, 2014
1
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Serikali za Mitaa na Mbunge wa Jimbo la Nzega, Dk. Khamis Kigwangala, akitangaza nia yake ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania wakati alipokutana na waandishi wa habari ambapo amesema hajasukumwa na mtu yeyote ila ni yeye mwenyewe ameamua kwa moyo wake.
02
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Serikali za Mitaa na Mbunge wa Jimbo la Nzega Dk. Khamis Kigwangala akimtambulisha mke wake Dk. Bayoum Awadh wakati wa mkutano huo.
2
Mzee Nasser SAid Mussa baba mzazi wa Dk. Khamis Kigwangallah na mama yake mzazi Mama Bagaile Lumola.
 4
Mzee Nasser Said Mussa ambaye ni baba mzazi wa Dk. Khamis Kigwangala na mama yake mzazi Mama Bagaile Lumola na watoto wake Sheila kulia ni Hawa.
8
Mchungaji Patrick Saso akifanya maombi kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
9
10
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.
DSC_0103
Sheikh Abubakary Mwita akiomba dua kabla ya kuanza kwa mkutano.

WAZIRI MWAKYEMBE ATEMBELEA ENEO LA AJALI YA MABASI MUSOMA, AWAJULIA HALI MAJERUHI


Posted by GLOBAL on September 7, 2014
Waziri wa Uchukuzi, Dkt Haririson Mwakyembe akiwa na Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani, Mohamed Mpinga, wakiangalia gari la Mwanza Coach walipotembelea eneoe la ajali jana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, ACP Philipo Kalangi kulia, akiwa na Dkt Harrison Mwakyembe, wakiangalia gari dogo aina ya Nissan Terano linalodaiwa kupata ajali baada ya kugongwa na basi la Mwanza Coach na kutumbukia mtoni.

Dkt Mwakyembe, Waziri Gaudensia Kabaka na Dkt Samson Winani (mwenye shati la kitenge) wakimwangalia mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo.
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akimjulia hali Mwandishi wa Habari wa Raia Tanzania, Veronica Mwakyembe ambaye alikuwa amelezwa Musoma.
Mawaziri Dkt Harison Mwakyembe na Gaudensia Kabaka walifurahia jambo wakati wakimjulia hali Frorance Focus.
Meya wa Manispaa ya Musoma, Kisurura akimpa pole Kenneth Chilemile mkazi wa Nyegezi Mwanza, aliypata ajali akiwa katika gari dogo aina ya Nissan Terano, ambapo baba yake Ibrahimu Mashida pamoja na dereva wake walipoteza maisha.
Wahudumu wa afya wakisaidiana kusukuma kitanda cha mgonjwa wa ajali ya Mwanza Coach na J4 Express.
Mwandishi wa Mwananchi, Florance Focus akiwa amelazwa katika Hopitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara baada ya kupata majeraha kichwani na miguuni. Hata hivyo amehamishiwa Bugando kutokana na hali yake kuwa mbaya.
Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Jackson Msome (wa kwanza kulia), Mkurugenzi wa Manispaa ya Musoma, Ahmed Sawa na Meya wa Manispaa ya Musoma, Kisurura wa kwanza kushoto wakimjulia hali Mwandishi wa Mwanacnhi Florance Focus baada ya kupata ajali.
Mwandishi wa Channel Ten, Augustine Mgendi akimwangalia Veronica Mwakyembe aliyepata ajali akisafiri na basi la Mwanza Coach. Mwakyembe ambaye ni mwandishi wa habari wa Raia Tanzania amehamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando kutokana na kupata mvunjiko kwenye bega na majeraha ya mguu wa kushoto.
Waombolezaji wakiwa wamebeba majeneza ya miili ya marehemu waliokufa katika ajali ya mabasi ya Mwanza Coach na J4 Express wakienda kuzika katika makaburi ya Musoma

Ushauri Kwa Wapinzani wa Lowassa Ndani ya CCM


Nimekuwa nikiona wapinzani wa Lowassa ndani ya ccm wakihangaika kila njia wakijaribu kuangalia ni namna gani wanaweza kumshughulikia jembe hili la kaskazini linalo mtanguliza Mungu mbele wakati wote wa mambo yake.

Lakini leo nimeona walau niwape ushauri kidogo baada ya kuona kila mnapo jaribu mnaangukia pua ni kwamba Lowassa ni mtu anaye mcha Mungu tofauti na wapinzani wake ndani ya CCM wamekuwa mara nyingi wanatumia nguvu za kiza na fedha nyingi wakifiri watamuweza Lowassa, lakini cha kushangaza mzee Lowasa amekuwa akizidi kuchanja mbuga kila kukicha na nyota yake kuonekana iking'ara kila siku japo kafungukiwa.

Naomba niwadokezee siri kuwa mgeukieni Mungu achaneni na nguvu za giza na mazingaombwe ndio njia tu ya kuweza kupambana na Lowassa japo mpaka muda kama ni soka basi tunaweza kusema Lowasa anaongoza kwa bao 3 bila,

Mkizingatia ushauri wangu mtasonga mbele epukeni kwenda kuchanjwa chale mwili mzima mrudieni Muumba atawasaidia.

By kiloriti