Friday, 12 September 2014

BURUDANI::UZINDUZI WA COKE STUDIO AFRICA WAFAANA DAR‏

Mwanamitindo Rio Paul (kulia) akiwa na rafiki zake muda mfupi baada ya uzinduzi wa msimu wa pili wa  Coke studio Africa, Hyatt Hotel, jijini Dar es Salaam.
Wanamuziki Vanessa Mdee, Jo Makini na Shaa wakiwa katika picha ya pamoja kwenye 'red Carpet  wakati wa uzinduzi huo.
Kutoka kushoto ni Joh Makini, Shaa, Bukuku (Mc wa shughuli hiyo), Maurice (bland meneja wa Coca-cola) na Vanessa Mdee.
Kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola,  jana usiku ilizindua  msimu wa pili wa onyesho la runinga lijulikanalo kama  ‘Coke Studio Africa’ ambalo linatarajiwa konyeshwa kila Jumatatu na kituo cha Shirika la Utangazaji cha TBC.
Akizungumza na wandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt jijijini Dar es Salaam, Meneja bidhaa wa Coca-Cola Tanzania, Maurice Njowoka alisema, ni furaha na fahari kwa watanzania na waafrika kwa ujumla kwa kukutana pamoja na kuonyesha uwezo wa vipaji vyao hivyo, ambapo watu watapata kuona na kujifunza vipaji na radha nzuri kutoka kwa wasanii 24 wa bara la Afrika.
“Muziki ni lugha isiyo na mipaka na njia muhimu ya kuonyesha hisia na furaha, tungependa kusambaza furaha Barani Afrika kupitia muziki kwa kushirikiana na wasanii,” alisema Njowoka.
Alisema, ujumbe wa msimu wa mwaka huu ni ‘Ushirikiano  wa Afrika, muziki wa afrika’, ambapo pia mbali na wasanii nyota pia wameweza kushirikisha bendi, watayarishaji muziki na madj bora wa bara la Afrika.
Njowoka aliwataja wasanii hao kwa mwaka huu na nchi zao kwenye mabano ni pamoja na  Flavor Nabania,
Omawumi, Waje, Burna Boy, Chidima, Olamide, Iyanya, Seyi Shay,Yemi Alade na Phyno (wote kutoka Nigeria),  wengine ni Fena Gitu, Rabbit, Victoria Kimani na Jay A (Wote kutoka Kenya),  Navio, Jacie Chandiru na Lilian Mbabazi (Kutoka Uganda),  John Makini, Shaa, Diamond na Vanessa Mdee (Kutoka Tanzania). Wengine ni Neyma, Jose Valdemiro na  Marllen (Msumbiji) huku watayarishaji wa muziki ni Silvastone (Ghana), Chopstix na Afrologic (Nigeria), Kevin Provoke,Kagwe Mugai na Owuor Arunga (Kenya) na wengieo.
Hata hivyo, mbali na kuonyeshwa kila Jumatatu kupitia runinga ya TBC,  mashabiki wanaweza kufuatilia pia kupitia tovuti ya Coke studio ambayo ni www.cokestudioafrica.com.
Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na mastaa mbalimbali wakiwemo wanamitindo, wabunifu, mamiss, wasanii wa filamu, muziki, vichekesho.
 
                           Mwisho

KUTOKA MBEYA::MKUU WA MKOA WA MBEYA MH. ABBAS KANDORO AWAASA MADEREVA WA MABASI PAMOJA NA ABIRIA KUHUSIANA NA USALAMA PAMOJA NA AJALI ZILIZOTOKEA HIVI KARIBUNI.


 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh, Abbas Kandoro akiongea na Madereva na Abiria leo asubuhi saa kumi na moja katika kituo Kikuu cha Mabasi Mbeya
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi wa kwanza kulia akiwa katika mkutano huo

Baadhi ya Madereva, Abiria na ma Agent wa mabasi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya
Mabasi yakianza kuondoka



Picha na Mbeya yetu

MSIKITI WA MTAMBANI KINONDONI WAUNGUA TENA



(Msikiti wa Mtambani ukiungua kwa moto. Picha na Maktaba yetu)
Habari zilizotufikia ni kwamba Msikiti wa Mtambani uliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam unateketea kwa moto hivi sasa. Hii ni mara ya pili msikiti huo kutetekea kwa moto baada ya kuungua Agosti 13 mwaka huu. Habari zaidi zitawajia hivi punde.

KUTOKA BUNGENI:::HUU NDIO MSIMAMO WA MH.SITTA KUHUSU KATIBA MPYA.

Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta ‘amekomaa’ kuhakikisha Bunge Maalumu la Katiba linafanya kazi kwa kasi na kukamilisha kila kitu ifikapo tarehe yake ya mwisho, Oktoba 4, ikiwamo kupiga kura za kupitisha Katiba inayopendekezwa kazi ambayo amesema itafanywa hadi nje ya nchi kwa wajumbe watakaokuwa huko. 
Sitta alilazimika kutoa matamko mawili kwa nyakati tofauti, mara ya kwanza wakati kikao cha Bunge kilipoanza jana akieleza jinsi Rasimu ya Katiba inayopendekezwa itakavyokamilika ifikapo Septemba 21 na baadaye mchana wakati akiahirisha Bunge alipotangaza mikakati ya kukusanya kura za wajumbe hadi nje ya nchi kuanzia Septemba 26, mwaka huu.
Sitta alitumia fursa hiyo kuwataka wajumbe wa Bunge hilo watakaokuwa nje ya nchi kwa matibabu au sababu nyingine kuacha mawasiliano yao ili waweze kupiga kura wakiwa hukohuko.
Alisema uongozi wa Bunge umeanza kufanya mawasiliano na balozi mbalimbali za Tanzania nje ya nchi ili wawepo watumishi wake watakaokula kiapo cha kisheria ili wasimamie upigaji kura.
sitta
Kauli za Sitta zimekuja siku moja baada ya Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kuweka bayana makubaliano baina ya wajumbe wake na Rais Jakaya Kikwete kuwa hataongeza muda wa uhai wa Bunge hilo, hivyo litakoma Oktoba 4, mwaka huu na hakutakuwa na upigaji wa kura ya maoni kupitisha Katiba hiyo hadi baada ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 2015.

Kauli za Sitta

Akizungumza bungeni kwa kujiamini lakini bila kugusia ratiba ya Bunge hilo iliyokuwa inafikia Oktoba 30, mwaka huu, Sitta alisema ratiba ya Bunge hilo itaendelea kama tangazo la Rais katika Gazeti la Serikali linavyosema.
GN hiyo namba 254 iliyotolewa Agosti Mosi, mwaka huu, ililiongezea Bunge hilo siku 60 ambazo zinamalizika Oktoba 4, mwaka huu baada ya siku 70 za awali kumalizika bila kupatikana katiba inayopendekezwa.
“Kwa taarifa tu na msisitizo, ni kwamba ratiba yetu ya Bunge Maalumu inaendelea kama ilivyopangwa,”alisema Sitta huku akishangiliwa kwa makofi na wajumbe waliokuwamo.
“Siku 60 za Bunge hili ambazo ni nyongeza ya siku tulizopewa na Rais kwa mujibu wa sheria usipohesabu siku za Jumamosi, Jumapili na sikukuu, zinaishia tarehe 4 Oktoba,” alisema Sitta.
Alisema kikao cha Kamati ya Uongozi kilichoketi juzi, kimeelezwa kuwa Bunge hilo linakwenda vizuri na kwamba Kamati ya Uandishi imejipanga kuwapatia Rasimu ya Katiba Septemba 21, mwaka huu.
“Kwa hiyo ni dhahiri kabisa kwamba lengo tulilopewa na Taifa la kutoa Katiba inayopendekezwa tutalimudu ndani ya wakati,” alisema Sitta ambaye pia ni Mbunge Urambo Mashariki (CCM) na kuongeza:

“Tunaangalia upigaji kura wa wenzetu ambao hawapo kwa sababu mbalimbali nje ya ukumbi huu ukiacha wale waliosusa, wapo wengine wana sababu za kutokuwapo kama vile hospitalini. Kwa hiyo itakapofika wakati wa kupiga kura, tutatoa maelezo ya utaratibu upi utatumika kuweza kuwapata hao kwa sababu akidi inahusu sisi sote ambao tuliteuliwa na Mheshimiwa Rais.”
Kwa mujibu wa tafsiri ya Kanuni za Bunge, “Akidi” maana yake ni idadi ya wajumbe inayoruhusiwa kwa madhumuni ya kuanza kikao cha Bunge Maalumu, Kamati au kufanya uamuzi wa Bunge Maalumu au wa Kamati ya Bunge Maalumu.
Sitta alitangaza pia kuwa mjadala ambao ulianza Jumanne iliyopita ungeendelea hadi keshokutwa, tofauti na tangazo lililotolewa awali na Makamu Mwenyekiti wake, Samia Suluhu Hassan kuwa majadiliano yangechukua siku nane hadi Alhamisi ijayo.
Ili kukamilisha dhamira hiyo, Jumamosi imerudishwa kuwa siku ya kazi, licha ya awali kuondolewa pamoja na siku za Jumapili na sikukuu na kuzifanya za kazi kinyume na utaratibu uliokuwa umezifuta kwa kuzingatia “sheria za kazi.”
Baadaye, kabla ya kusitisha shughuli za Bunge mchana, Sitta alitoa tangazo jingine, akibainisha kuwa upigaji kura utaanza Septemba 26 na utafanyika hata kwa wajumbe watakaokuwa nje ya nchi.
Sitta alikuwa akitoa tangazo hilo kurejea maombi ya baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo ambao ni waumini wa Kiislamu wanaopanga kwenda Hija kuanzia Septemba 22, mwaka huu.

Lukuvi ajiweka kando

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alipoulizwa jana iwapo anadhani siku zilizobaki zitatosha kumaliza shughuli za Bunge zilizokuwa zimepangwa hadi mwisho wa Oktoba, alitaka tamko la Sitta ndilo linukuliwe.
“Si umemsikia mwenyekiti mwenyewe leo (jana) asubuhi akiji-commit (akiahidi) kwamba Bunge hili litamaliza kazi yake mpaka kupatikana kwa katiba inayopendekezwa? Unataka nini tena,” alisema.
Alipoulizwa ratiba ya awali inayokoma Oktoba 31, mwaka huu, Lukuvi alisema GN iko wazi juu ya ukomo wa Bunge hilo.
Kwa upande wake Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema alipoulizwa iwapo Rais ajaye atawajibika kisheria au la kuendeleza mchakato wa Katiba pale ulipoishia alisema:
“Katiba na sheria tuliyonayo haimbani rais ajaye kuendeleza mchakato kwa sababu anaweza kuja na vipaumbele vyake, lakini njia pekee ya kumbana ni kurekebisha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba,”alisema.

Hata hivyo, Jaji Werema alisema wataangalia uwezekano wa kuifanyia mabadiliko sheria hiyo ili itamke kuwa upigaji wa kura ya maoni unaahirishwa hadi wakati wa Rais ajaye ili mchakato uendelee kuwa hai.
Hata hivyo, pamoja na Bunge hilo kuongeza kasi ili kukamilisha kazi, taarifa zinasema bado Katiba inayopendekezwa inaweza kukwamishwa na upatikanaji wa theluthi mbili.
“Baadhi ya Kamati hazikupata theluthi mbili, sidhani kama tutapata Katiba inayopendekezwa. Angalia mawaziri na wabunge wenyewe wa CCM hawahudhurii,” ilidokezwa.
Kigogo mmoja wa Serikali alisema juzi kuwa ijapokuwa CCM wanajiaminisha kupata theluthi mbili Bara na kwamba wasiwasi uko Zanzibar lakini hata bara theluthi mbili inaweza isipatikane pia

Aamrishwa kukoma kusambaza HIV

Jaji nchini Marekani amemuamrisha mwanamume mmoja mwathiriwa wa virusi vya HIV kukoma kusambaza virusi hivyo na badala yake kupata matibabu.
Inaarifiwa mwanamume huyo amewaambukiza watu 8 virusi kwa kukusudia katika kipindi cha miaka minne
Mwanamume huyo, aliyetambuliwa tu kwa herufi...'AO' katika stakabadhi zake, ametakiwa na mahakama kupata ushauri nasaha ili aweze kuwakinga wapenzi wake katika siku za usoni.
Maafisa wanasisitiza kwamba sio lengo lao kuufanya uhusiano wa kimapeni kuwa uhalifu bali wanataka zaidi kulinda umma.
Mwanamume huyo huenda akatozwa faini au kufungwa jela ikiwa hatafuata sheria kama alivyotakiwa.
Takriban watu 50,000 nchini Marekani huambukizwa virusi vya HIV kila mwaka , kulingana na shirika la kupambana na maambukizi (CDC).
Asilimia 16% ya watu milioni 1.1 wanaishi na virusi vya HIV bila ya kujua kwamba wameambukizwa.
Mwanamume huyo, alipatikana na virusi vya HIV mwaka 2008 na kuanza kusambaza kwa watu wengine na hadi sasa watu 8 wamethiriwa baada ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi naye.
Alisambaza virusi hivyo licha ya kupokea ushauri nasaha ikiwemo kutumia kinga kila wakati anapojihusisha na tendo la ndoa.

Thursday, 11 September 2014

UNG'ENG'E HUO::A DISPATCH FROM THE WAR ON WOMEN WHO USE DRUGS



Representatives of the International Network of People who Use Drugs (INPUD)

Being imprisoned for sex work after testing positive for HIV, an increased likelihood of domestic violence, the removal of children, and a heightened risk of contracting blood-borne viruses: these are some the hardships faced by women who use drugs around the globe. 

The silence created by the stigma surrounding their drug use, coupled with a lack of adequate programs designed to service their needs, renders these women invisible casualties of the war on drugs.

At the recent International AIDS Conference in Melbourne, a group of drug activist women came together to for Women Drugs Users: Our Voices, Our Lives, Our Health, a seminar discussing the difficulties encountered by women who use drugs in their own countries. 

In August, to help improve the lives of female drug users, the United Nations Office on Drugs and Crime (UNODC), UN Women and the International Network of People who Use Drugs (INPUD) released a joint policy brief, calling for gender equality in the field of harm reduction. 

The key outtake: there is much to be done.

A victim of domestic violence in Tanzania

In Tanzania domestic violence is rife and widely accepted, with statistics from a 2010 report showing that 39 percent of women surveyed between the ages of 15 to 49 had experienced it. But the situation is much worse for women who use drugs. 

In a recent, yet unpublished Pangaea study, 93 percent of women drug users who were not on an opioid substitution program reported experiencing domestic violence.

Susan Masanja, founder and coordinator of Real Activist Community Tanzania, spoke about the situation at the International AIDS Conference. Masanja is a long-term drug user who’s experienced domestic violence and undertaken the drawn-out court process to receive a protection order. She said when women do report an incidence of violence to police, their drug use is often used as a reason to dismiss their claims.

Masanja also explained that because of the stigma that comes with drug use, many of these women find it difficult to gain employment and turn to sex work. They then face being arrested and at times forced by police to have sex in return for their release. Although there is no accurate data available, Masanja believes that most women who use drugs in her country have hepatitis C, while around 80 percent are living with HIV.

Susan Masanja.

“There needs to be more harm reduction services, first of all, and sexual reproduction and health rights. 

Lots of women have sex without any protection. You need education about family planning,” explained Masanja. In regards to domestic violence, she said: “There needs to be more advocacy networks… because in our culture and tradition it's OK for a woman to be beaten by a man.”

Due to the issues being confronted by these women and others like them, the UNODC joint policy brief entitled Women who inject Drugs and HIV was released last month. It outlines that most harm reduction programs are geared towards men, so changes need to be made to these services addressing the specific needs of women. In order to have gender equality in harm reduction, it is essential that women who use drugs are involved in the development and implementation of these programs.

Monica Beg, chief of the HIV/AIDS section at UNODC, told VICE that women who use drugs face unique challenges because of physiological factors, such as pregnancy and that they are more likely to acquire HIV than male drug users. “This requires a wide range of tailored services for women who use drugs beyond standard harm reduction services,” she said. 

“To move forward and quicken the pace of the response we will need commitment and we will need champions starting from senior policy makers to programme managers… to say straight and loud that accessing gender responsive harm reduction services is not a privilege—it is a right.”

In 2012, the Greek health minister Andreas Loverdos instated Provision 39A, allowing Greek authorities to carry out the forced HIV testing of hundreds of women in Athens.

 The move, which was condemned by human rights groups around the world, led to the imprisonment of 31 female drug users. They were accused of being sex workers and—because they were living with HIV—causing serious bodily harm to their clients.
Chairwoman of the Greek Drug and Substitute Users Union, Efi Kokkini, described this incident as “one of the most terrible human rights violations in Greek history.”

 At the seminar, she explained that these women had their names and photos revealed to the media and some remained in prison for up to ten months. It was subsequently found that only one of the women was actually a sex worker.


Kokkini, who injected drugs for many years, is now on the methadone program. She thinks that women who use drugs and sex workers need to mobilise and claim their human rights.

 “Drug use would not be demonized if a safe environment was available to drug users, if the war on drugs, prohibition and criminalisation stopped today and harm reduction practices were established to heal the wounds this war has caused,” she said.
Nyah Harwood, a PhD candidate at the Centre for Social Research in Health at the University of New South Wales, spoke at the seminar about trans women who use drugs. 

She said trans women have never been assigned an epidemiological category, so when research is carried out and in harm reduction programs, they are often overlooked. Although there is little data available regarding trans women who use drugs and HIV rates, she stated that the rates are extremely high. Harwood pointed to a 1992 study in Rome cited by Viviane Namaste, which found that 100 percent of trans women who use drugs were living with HIV, when they’d lived within that same environment for a period of four years.

According to Harwood, when harm reduction programs are being developed by governments, the most vulnerable people in the community should be consulted, those being: indigenous people, trans people of colour, sex workers and injecting drug users.

 “The things that destroy people's lives are the laws that we have around drugs and drug use,” she said. “The laws that we have at the moment criminalise people. 

They stigmatise people who use drugs and therefore people don't want to go and get tested for blood-borne viruses. They don't want to get treatment and everything to do with drug use is done in the dark trying to hide away from the authorities.”

Jude Byrne, chair of INPUD, said that because of the societal standards placed upon women, often women who use drugs don’t speak about their experiences or utilise services and “hide because they're children will be taken off them.”

Byrne was on the committee that helped write the UNODC joint brief. 

She sees the brief as an important statement, as it is coming out of an office that is renowned for its prohibitionist stance.

 “For them to come out and say that women who use drugs are struggling and put a paper out on that indicates that even they get it,” she said. “Even the top organisation globally that supports prohibition is saying that women are really suffering, on what on the one hand we're supporting, but on the other hand we see is not helping.”
SOURCE:KALULUNGA

DOKII AGOMA KUZUNGUMZIA NDOA

Na Gladness Mallya
MWANADADA  anayefanya vizuri kunako gemu la muziki Bongo, Ummy Wenslaus ‘Dokii’ hivi karibuni alinaswa akitoa meno yote nje baada ya kushuhudia sherehe ya msanii mwenzake, Lucy Komba na kusema ya kwake hawezi kuizungumzia kamwe.
Msanii mkongwe wa tasnia ya filamu bongo Ummy Wenslaus ‘Dokii’
Akizungumza na paparazi wetu, Dokii alisema amefurahi sana Lucy kuolewa na Mzungu na alidhani kwamba ni mzee kama Waafrika wengine wanavyopenda kuolewa na Wazungu wazee lakini amempata kijana mzuri anayevutia hivyo ana bahati ya pekee lakini kwa upande wake ndoa hataki hata kuisikia.
“Kuhusu mimi siwezi kuzungumzia na huwa sipendi kabisa kuzungumzia suala la ndoa yangu kama nimeolewa au nitaolewa ila naendelea kumpongeza Lucy kwani siyo msichana yule wa kujisikia wala nini anaongea na kila mtu,” alisema Dokii ambaye hajawahi kumwanika mwanaume wake.

UGONJWA WA MWAAFRIKA..Makalio Makubwa For Ladies Ndio HabariYa Mjini, Some are Real Blessed ! But Others Mh!




Ni shida Hapa Mjini kwa Wadada , Kila Mdada anataka Awe na Mkia as ndo kitu kina kiki hapa Town, Inafikia Wengine wanaamua kutafuta Makalio Fake kwa Njia yoyote ile Kama kumeza dawa za mchina ama kuvaa vigodoro..Wadada Jamani Taratibu Siku hizi Wanaume hata hatujui lipi Fake lipi Original...

KIAFYA ZAIDI:::WANAWAKE: MSITUMIE SUKARI SIYO NZURI SANA!

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa hivi karibuni na jarida moja la masuala ya afya la nchini Uingereza (BMC Public Health), unywaji wa vinywaji vyenye sukari, kiasi cha mara tatu kwa wiki, huweza kunenepesha matiti na unenepaji wa matiti huongeza hatari ya mwanamke kupatwa na saratani ya matiti.
Waliofanyiwa utafiti huo ni wanawake 776 ambao hawajafikia ukomo wa hedhi (Premenopausal) na wanawake 779 waliofikia ukomo wa hedhi (Postmenopausal).
Pamoja na maswali mengine waliyoulizwa, wanawake hao waliulizwa kiasi wanachokula kwa upande wa vyakula na vinywaji vyenye sukari kama vile chokoleti, keki, ice cream, soda, n.k na huwa wanaweka vijiko vingapi vya sukari kwa vinywaji wanavyotayarisha, kama chai au juisi.
Akiongelea matokeo ya utafiti wao, mtafiti na mwandishi kiongozi wa utafiti huo kutoka Chuo Kikuu cha Laval cha Quebec, nchini Canada, Caroline Diorio alisema kuwa matokeo yalionesha kuwepo kwa uhusiano mkubwa kati ya utumiaji wa sukari kwa wingi na kuongezeka kwa ukubwa wa matiti ya wanawake kutoka makundi yote mawili (wasichana na watu wazima).
Katika utafiti wao, wamegundua zaidi kuwa wanawake waliofikisha ukomo wa hedhi matiti yao yaliongezeka ukubwa zaidi kwa kula vyakula vingi vyenye mafuta, wakati wanawake ambao hawajafikisha ukomo wa hedhi, waliongezeka ukubwa wa matiti yao kwa kula vinywaji vyenye sukari visivyopungua vitatu kwa wiki.
Matokeo ya utafiti huo yanatoa picha kwamba kuwa na matiti makubwa kunakosababishwa na ulaji wa sukari pamoja na mafuta kwa wingi huongeza hatari ya kupatwa na saratani ya matiti kwa asilimia 3.
Dk. Dioro anamalizia kwa kusema kuwa utafiti zaidi unahitajika, hususan katika makundi ya watu wenye matumizi makubwa ya sukari. Lakini hata hivyo, amesema kuwa hadi utafiti mwingine utakapofanyika na kuthibitisha vinginevyo, kwa sasa uhusiano wa matumizi makubwa ya sukari na unenepaji wa matiti kwa wanawake uko wazi.
Kwa kuwa unenepaji wa matiti una uhusiano mkubwa na ulaji mkubwa wa mafuta na sukari kwa njia mbalimbali kama zilivyoanishwa hapo juu, na kwa kuwa unenepaji wa matiti unaongeza pia hatari ya mwanamke kupatwa na saratani ya matiti, ni sababu tosha kabisa ya wewe kuamua kuachana na unywaji wa vinywaji baridi vyenye sukari nyingi kwa faida ya afya yako.
Kama ambavyo mara kwa mara tumekuwa tukisisitiza, tuepuke sana matumizi makubwa ya sukari na tunapoitumia basi tuitumie kwa kiasi kidogo sana na badala yake tupendelee kutumia asali na kula kwa wingi matunda na mboga za majani ambazo huwa na sukari asilia ambayo haina madhara mwilini.

Kwenye rekodi za 2014 na hii ya huyu Mungu anaeonekana Kenya imo.

Screen Shot 2014-09-11 at 9.20.14 AM
Kituo cha TV cha K24 kiliripoti juu ya uwepo wa Mungu nchini Kenya ambae ibada zinafanyika nyumbani huku yeye mwenyewe akisema ‘Mimi ni Mungu, nimekuja kuvunja mambo yote yaliyoandikwa’

MBINU 5 ZA KUJIFUNZA MAPENZI ILI USIACHIKE, USISALITIWE!

MBINU 5 ZA KUJIFUNZA MAPENZI ILI USIACHIKE, USISALITIWE!

HAWANA NAO VIPI::STEVE NYERERE, MTITU WAFIKA PABAYA!

STEVE NYERERE, MTITU WAFIKA PABAYA!

SHE IS PRETTY.....Fantastica bella...WASTARA HUYO...HUTAKI KIMBIA

Staa wa filamu za Kibongo,Wastara Juma

HURUMA YA LEO::JOHARI AZIDI KUTESEKA PENZI LA RAY!

Nimeacha Poda na Sijarogwa na Diamond na Ninamkubali Kinoma- Q Chillah


NAE NI RAIS>>>Sababu za kufukuzwa kazi Rais wa shirikisho la muziki Tanzania.

MOTO WA KARATASI::CWT YAITANGAZIA MKWARA SERIKALI - YATOA SIKU 14 ILIPE MADENI YOTE

Jengo la chama cha walimu CWT Mkoa wa Iringa
 Mwenyekiti wa Chama cha walimu CWT Mkoa wa Iringa Mwalimu Stanslaus Mhongole, akisikiliza jambo katika mkutano wa kutoa tamko baina ya uongozi wa CWT na baadhi ya wanahabari mkoani Iringa.
 
 Katibu wa CWT Mkoa wa Iringa Mshamu Ally Mshamu akiwa katika mkutano baina ya baadhi ya wanahabari mkoani Iringa na uongozi wa CWT - wakati wakitoa tamko.
 Baadhi ya viongozi wa CWT mkoa wa Irinbga wakisikiliza jambo kutoka kwa wanahabari (hawapo pichani) wakati wa utoaji wa tamko.
 Frenk Leonard- Mwandishi wa habari wa gazeti la Habari leo na mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoani Iringa akiwa katika mkutano huo wa CWT.
 Geofrey Nyang'olo- mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi akiwajibika katika mkutano huo wa CWT.
Heriety mwandishi na mtangazaji wa kituo cha redio County fm  akisikiliza jambo kutoka kwa viongozi wa CWT mkoa wa iringa.
 Yohana Mgaya mtangazaji na mwandishi wa habari wa kituo cha redio Furaha akiwa kazini katika mkutano huo.
 Victory Meena mtangazaji na mwandishi wa habari wa kituo cha redio Nuru fm akiwajibika kazini.
 Eliasa Ally mwandishi wa habari wa gazeti la Majira akifuatilia jambo katika mkutano huo baina ya viongozi wa CWT na wanahabari.
 Silvanus Kigomba mwandishi wa habari wa Televisheni ya ITV na radio One, akiwa kazini katika mkutano huo wa CWT.

Yuvenary  Kimario mwandishi wa habari wa kituo cha radio Country fm na mwakirishi wa gazeti la Nipashe. akiwa kazini


 

 


 

 

CHAMA cha walimu Tanzania- CWT mkoa wa Iringa kimetoa siku 14 kwa Serikali mkoani humo, iwe imelipa madeni  yote inayodaiwa na walimu wake– huku kikitishia kutofanyakazi  kuanzia Septembe 15 endapo agizo hilo halitatekelezwa.

CWT imesema kamwe haiwezi kuendelea kuifumbia macho serikali, huku walimu wake wakiishi maisha duni na yenye kukatisha tamaa, na mbaya zaidi kikilalamikia punguzo la fedha za mifuko ya jamii, ambazo huwasaidia watumishi pindi wanapostaafu.

Akisoma tamko hilo mbele ya baadhi ya waandishi wa habari mkoani Iringa – Mwalimu Stanslaus Muhongole ambaye ni mwenyekiti wa CWT mkoa wa Iringa amesema…

“Chama cha Walimu Mkoa wa Iringa kinaunga mkono Tamko la Chama makao makuu (CWT) na chama cha wafanyakazi wa taasisi za elimu ya juu Tanzania (THTU) kwa tamko lao walilolitoa kwa pamoja katika kupinga mpango wa serikali wa kupunguza Mafao ya wastaafu kupitia Mifuko ya hifadhi ya jamii.

Muhongole amesema wao kama walio wa mkoa wa Iringa wanasisitiza kuwa mpango huo wa serikali hauna nia njema kwa maendeleo ya nchi, hasa kwa walimu ambao wamekubali kulipwa mishahara midogo isiyokidhi mahitaji.

Amesema licha ya walimu kuwa na mishahara duni lakini wamekubali kukatwa sehemu ya mishahara hiyo na kuiwekeza katika mifuko ya hifadhi ya jamiiili iwe na manufaa pindi wanapostaafu.

…..“Chakushangaza serikali badala ya kuboresha mafao ya walimu ndani ya mifuko hiyo, tena inashiriki kuchukua fedha kwenye mifuko yetu kwa ajili ya kuendeshea shughuli zake na hivyo kuwaacha walengwa wa mifuko wakiambulia fedha kiduchu tofauti na hali halisi ya uwekezaji,” amesema.

Mhongole amesema Wizara ya kazi na ajira kwa kushirikiana na Mamlaka ya mifuko ya hifadhi ya jamii (SSRA) inadiriki kuandaa mpango wa kupunguza mafao ya wanachama wastaafu wa mifuko hiyo ya pensheni kwa watumishi wa umma (PSPF) na watumishi wa serikali za mitaa (LAPF) ili kuibeba Serikali dhidi ya madeni inayodaiwa na mifuko.

Amesema mpaka sasa Serikali inadaiwa takribani shilingi Tilioni 7, Bilioni 134, Milioni 300 ilizokopa kwenye mifuko hiyo ambayo watumishi hukatwa mishahara yao kwa lengo la kuhifadhi kwa matumizi wakati wanapostaafu.

Akitaja mifuko na kiwango cha fedha zilizochukuliwa na serikali, amesema...
Mfuko wa PSPF inadai shilingi 4, 827, 800, 000, 000/=
Mfuko wa LAPF unadai shilingi 2017, 700, 000, 000/=
Mfuko wa NSSF unadai shilingi 1, 333, 600, 000, 000/=
Mfuko wa PPF unadai shilingi 288, 600, 000, 000/=
Mfuko wa GEPF unadai shilingi 18, 000, 000, 000/=
Mfuko wa NHIF (wa afya) unadai shilingi 458, 600, 000/=

Aidha amesema hali mbaya ya mifuko hiyo inatokana na fedha nyingi zilizochotwa na serikali pasipo kuzirejesha kwa wakati, na sasa imeanza kupunguza malipo ya Pensheni ya mkupuo kutoka asilimia 50 ya sasa hadi asilimia 33.3 ya mshahara kabla ya kustaafu.

Pia amedai kuwa serikali inatumia wastani wa mshahara wa miaka 3 badala ya mshahara wa mwisho kukokotoa Pensheni.

Na kuwa imekuwa ikipunguza makadirio ya umri wa kuishi – badala ya kustaafu kutoka miaka 15.5 hadi miaka 12.5.

Amesema pia iunafanya hira katika kurekebisha vikokotoo limbikizi (Accrual rates ) vya mifuko kutoka 540 kwenda 580 kwa mifuko ya PSPF na LAPF, na kuwa hali hiyo kamwe haikubaliki.

Hata hivyo amesema kama chama wanaisihi serikali iachane kabisa na mpango huo dharimu kwani unaua nguvukazi ya Taifa la leo, kesho nala miaka ijayo.

Naye katibu wa CWT Mkoa wa Iringa Mwalimu Mshamu Aly Mshamu amesema serikali inatakiwa ilipe madeni yake yote inayodaiwa na walimu, ifikapo septemba 14, na kama haitafanya ivyo Septemba 15 walimu wa Wilaya zote watakutana katika ofisi ya mwajiri wao kwa kila Wilaya.

Mshamu amesema lengo la kufanya hivyo ni kuishinikiza serikali iwalipe stahiki zao walimu, kwani madeni hayo yanachangia kudhorotesha utendaji kazi wa walimu, na kuwa sasa kila mwalimu amdai mwajiri wake mpaka anapomlipwa.

Mshamu amesema tamko hilo linaitaka serikali kuanzia Septemba 1 mwaka huu mpaka 15 iwe imekamirisha madeni yote, kwani bila kufanya hivyo walimu watakaa katika ofisi za waajiri wao mpaka kutimia kwa sharti hilo.

Amesema walimu wilayani Mufindi wanadai serikali zaidi ya shilingi Milioni 159, huku Manispaa ya Iringa ikidaiwa na walimu wake zaidi ya shilingi Milioni 279, na Walimu wa Wilaya ya Iringa wakiidai Halmashauri hiyo zaidi ya shilingi Milioni 160.

Mshamu amesema Wilaya ya Kilolo nayo inadaiwa deni la zaidi ya shilingi Milioni 270 na walimu wake, na hivyo walimu mkoani Iringa kuidai Serikali jumla ya shilingi Milioni 871, 639, 188 na senti 70.

MWISHO.
CHANZO:matukiodaima

MSHANGAO??ESHA BUHETI ANANGWA, KISA MAKALIO

Na Rhoda Josiah
MJINI kuna vituko! Kitendo cha kutojaaliwa makalio makubwa kwa staa wa filamu za Kibongo, Esha Buheti kimemsababishia anangwe na wasanii wenzake.
Staa wa filamu za Kibongo, Esha Buheti.
Akipiga stori na paparazi wetu, Esha alisema anafahamu na anawashangaa watu wanaoponda maeneo hayo ya mwili wake kwani kwa upande wake anaamini kuwa mwanamke sura, makalio majaaliwa kwani hata mwanaume aliyemuoa analijua hilo na anampenda jinsi alivyo.
“Kwa kuwa mume wangu ananikubali jinsi nilivyo hainiumizi kichwa kwani mimi naamini sifa ya mwanamke ni tabia na wala siyo shepu kama wengine wanavyofikiria,” alisema Esha.

HOJA::Kuvaa Shanga Miguu au Vikuku Kwa Mwanamke Kuna Maana Yoyote Mbaya?



Kumekuwa na tetesi nyingi kuhusu urembo huu wa kuvaa cheni za miguuni. Wengi wamekuwa wakisema kuwa cheni hizo zinamaanisha kwamba mvaaji anaonyesha kwamba yeye anaweza mapenzi ya kinyume na maumbile, au analika pande zote tetesi hizi zimeleta mchanganyiko kidogo kwenye urembo huu.

Watu wengine wamediriki hata kukataza kabisa wapenzi wao wasivae urembo huo, mimi binafsi siwezi kuongozana na mtu amevaa kitu kama hicho. Haya sasa kazi kwako mdau, wewe unaonaje ni sawa urembo huo kutumika, na je mwenza wako akivaa urembo huo, utaafiki?

USHAURI WA LEO::WASTARA AMPA SOMO LA NDOA LUCY KOMBA

Stori Na: Gladness Mallya
SIKU chache baada ya msanii mkongwe wa filamu Bongo, Lucy Komba kuolewa, msanii mwenzake, Wastara Juma ameibuka na kumpa somo la ndoa huku akimtaka kuwa mvumilivu na msiri katika maisha hayo mapya.
Staa wa filamu za Kibongo,Wastara Juma.
Akistorisha na paparazi wetu, Wastara alisema maisha ya ndoa yanahitaji uvumilivu na usiri mkubwa hivyo Lucy anatakiwa kuzingatia hayo kwani ndiyo siri ya kudumu kwenye ndoa lakini akiyakosa hayo atashindwa kuilinda ndoa yake kwani ndiyo sababu kubwa ya ndoa za mastaa kuvunjika.
“Nimefurahi sana Lucy kuolewa, namuombea Mungu amsaidie adumu kwenye ndoa mpaka kifo kitakapowatenganisha kama mimi nilivyotenganishwa na Sajuki lakini awe msiri, mvumilivu na mwenye hekima,” alisema Wastara.
Nyota wa filamu Bongo, Lucy Francis Komba na mzungu wake raia wa Denmark anayejulikana kwa jina moja la Janus wakiwa ni wenye furaha wakati wa harusi yao.
Lucy alifunga ndoa hivi karibuni na mchumba wake wa siku nyingi ambaye ni raia wa Denmark anayejulikana kwa jina la Janus ambapo baada ya hapo atakaa nchini kwa mwezi mmoja kwa ajili ya maandalizi kisha waelekee Denmark kwa mumewe.