Saturday, 11 October 2014

HABARI NA PICHA::MKUTANO WA CCM IRINGA MJINI....CHADEMA MPO???

msafara  wa  Kiana  ukiwasili uwanja wa Mwembetogwa mjini Iringa
Wana CCm wakiwa na mabango katika  mkurtano wa  Kinana jimbo la Iringa mjini
Kamanda  wa UVCCM mkoa  wa Iringa  Salim Asas kushoto  akiwasilia na katibu mkuu Bw Kinana kulia
Kinana akiwasili uwanja  wa Mwembetogwa  leo
Umati  wa  wananchi  na  wanaccm waliofika kumsikiliza Kinana
wananchi jimbo la Iringa mjini wakimsikiliza  katibu mkuu wa CCM
Aliyekuwa  mmoja wa makada wa  Chadema Kalenga  akirejesha kadi ya  chadema
Kinana  kulia  akiwa katika  mkutano wake  leo mjini Iringa kulia kwake ni Mnec Iringa Bw Madenge
Umati wa wananchi   mjini Iringa
Kinana  akiwahutubia  wananchi wa Iringa mjini leo

UTALII RUAHA::HIFADHI YA TAIFA YA RUAHA IRINGA NI FAHARI YA KUSINI ,TEMBELEA LEO UONE WANYAMA

Twiga  wa  hifadhi  ya Ruaha  Iringa 
Watalii wa ndani wakiingia katika  nyumba za  kulala  wageni hifadhi ya Ruaha 
Moja kati ya  nyumba ya  kulala  wageni hifadhini hapo 
Tembo akiwa kando ya mto  Ruaha mkuu hifadhi ya Ruaha 
Clement Sanga  akitazama moja kati ya  gari la kitalii 
Hii ni ndege  ndogo ya  kulinda  hifadhi hiyo dhidi ya majangili 
Tembo na mwanae 
Twiga  akila  matawi ya miti huku akiwa amelala 
Ni maeneo yanayovutia  zaidi 
Swala  wa  hifadhi ya  Ruaha 
Kiboko  katika  mto  Ruaha 
Ndege wa  kuvutia 

TAFAKURI YA LEO::KAMANDA WA CHADEMA ALIYEJISALIMISHA CCM...

21Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi  pamoja na benderaalizokabidhiwa na wanachama wa CHADEMAbaada ya kurejea CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Nyololo Njiapanda. 

SIASA IRINGA::KATIBU MKUU WA CCM AIMALIZA CHADEMA NYOLOLO, LEO KUUNGURUMA IRINGA MJINI

Katika mkutano uliofanyika kijiji cha Nyololo  aliyekuwa Katibu wa CHADEMA  Kijiji cha Igowole Bw. Josephat Sibadi Soda amerejea CCM  baada ya uongozi wa chama hicho kutomlipa madeni ya vifaa mbalimbali alivyochukua madukani wakati wa ujenzi wa mnara wa marehemu Daud Mwangosi aliyeuwawa wakati wa mapambano ya jeshi la polisi na wafuasi wa CHADEMA mwaka jana uliojengwa katika kijiji cha Nyololo yeye akiwa mkandarasi na mbunfu wa mnara huo.2Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma mara baada ya kuwasili katika mashamba ya chai ya Ngwazi wilayani Mufindi kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Ndugu Jesca Msambatavangu.4Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana kulia  na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa ,Ittikadi na Uenezi wakishiriki kuchuma chai katika shamba la chai la Ngwazi wilayani Mufindi.1Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya kumwagilia maji katika bustani ya miche ya miti ya mbao katika vitalu vya kuotesha miti vya Umoja wa Vikundi vya Kijamii vya Kigamboni mjini Mafinga.13Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Nyololo Njiapanda kata ya Nyololo wilayani Mufindi.15Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Ndugu Jesca Msambatavangu akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ili aongee na wananchi wa kata ya Nyololo.14Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa ,Ittikadi na Uenezi  akiwahutubia wananchi wa kata ya Nyololo wilayani Mufindi katika mkutano uliofanyika uwanja wa Nyololo Njiapanda.
16Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Nyololo Njiapanda kata ya Nyololo wilayani Mufindi.18Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa ,Ittikadi na Uenezi  akimkaribisha aliyekuwa Katibu wa CHADEMA  Kijiji cha Igowole Bw. Josephat Sibadi Soda aliyerejea CCM leo baada ya uongozi wa chama hicho kutomlipa madeni ya vifaa mbalimbali alivyochukua madukani wakati wa ujenzi wa mnara wa marehemu  Daud Mwangosi aliyeuwawa wakati wa mapambano ya jeshi la polisi na wafuasi wa CHADEMA mwaka jana uliojengwa katika kijiji cha Nyololo19Aliyekuwa Katibu wa CHADEMA  Kijiji cha Igowole Bw. Josephat Sibadi Soda akikabidhi kadi yake pamoja na wanachama wa chama hicho 27 kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanabaada ya kurejea CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Nyololo Njiapanda. 20Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi alizokabidhiwa na wanachama wa CHADEMA  baada ya kurejea CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Nyololo Njiapanda. 21Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi  pamoja na benderaalizokabidhiwa na wanachama wa CHADEMAbaada ya kurejea CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Nyololo Njiapanda. 22Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongoza wana CCM waliojiunga na chama hicho kula kiapo mara baada ya kukabidhiwa kadi zao katika kiutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Nyololo Njiapanda wilayani Mufindi.23Waimbaji wa kwaya ya CCM Band wakiimba katikia mkutano huo.24Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiserebuka pamoja na wana CCM mbalimbali mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo.25Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa ,Ittikadi na Uenezi  wa tatu kutoka kulia na Katibu wa CCM wilayani Mufindi Ndugu Miraji Mtaturu wakipiga picha na waimbaji wa CCM Bandi waliotumbuiza katika mkutano huo.

UFISADI BARCELONA::FEDHA ZILIZOTUMIKA KUMLETA NEYMAR

Screen Shot 2014-10-10 at 9.16.37 AM 

Mwanzoni ilitangazwa kwamba ada ya €57m ililipwa kwa usajili wa Neymar, lakini katika matukio ya hivi karibuni yanaonyesha dili hilo la uhamisho limeiigharimu klabu zaidi ya €100k, Rosell bado chini ya uchunguzi kutokana na tuhuma hizi.
Gazeti la Cadenas Ser  limetoa taarifa kwamba Rosell amemwambia Jaji wa kesi yake wiki hii kwamba klabu yake ililipa kiasi cha €300,000 kuwasafirisha marafiki wa Neymar kutoka Brazil mpaka Barcelona kwa kutumia ndege binafsi katika utambulisho wa Neymar.
Kundi la marafiki wa Neymar maarufu kama ‘The ‘Toiss’ wamekuwa na Neymar tangu utotoni katika mitaa ya jiji la Sao Paulo, na wamekuwa wakimtembelea Neymar jijini Barcelona, lakini sasa ni mchezaji mwenyewe anayewalipia washkaji zake.

VITUKO MITAANI:: NANI ALAUMIWE KATI YA JIJI NA TANESCO MBEYA KWA KITUKO HIKI


Hii hatari kwa waendesha magari nyakati za usiku hii nguzo ipo barabara mpya jirani ya bustani ya jiji eneo la uwanja wa sokoine jijini Mbeya 
Je? ushirikiano wa Halmashauri ya jiji la Mbeya na Tanesco hakuna mmeshindwa kukaa chini mkajadili swala hili maana yote mnayofanya ni kwafaida ya wananchi 
Picha yenyewe inajieleza je mnasubiri ajali itokee ndiyo mchukue hatua?
Hii hatari sana ujumbe tunaimani umefika 


Picha na Mbeya yetu

MOSHI::Maofisa polisi 120 watimuliwa CCP

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu  

Moshi. Maofisa wa Polisi wapatao 120 wa Jeshi la Polisi, waliokuwa wakihudhuria mafunzo ya kupandishwa vyeo katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi (MPA), wametimuliwa chuoni hapo.
Habari za uhakika zilizopatikana jana kutoka ndani ya chuo hicho zamani kikijulikana kama CCP, zimedai uamuzi wa kuwaondoa chuoni ulitangazwa jana na mkuu wa chuo hicho, Matanga Mbushi.
Vyanzo mbalimbali vililidokeza gazeti hili kuwa, waliotimuliwa chuoni hapo ni maofisa ambao wana ulemavu wa aina mbalimbali walioupata wakiwa wanatekeleza majukumu yao ya kazi.
Habari hizo zilisema hadi jana saa 9:00 alasiri, maofisa hao walikuwa ofisi za mkuu wa chuo hicho wakisubiri kupatiwa maelekezo ya namna ya kurejea katika vituo vyao vya kazi mikoa mbalimbali.
“Wako 120 hivi walikuja hapa (MPA) kwa ajili ya kuchukua kozi za Koplo, Sajenti, Meja na ‘Assistant Inspector’ (wakaguzi wasaidizi), lakini ndiyo hivyo wametuambia tuondoke,” kilidokeza chanzo chetu.
Hata hivyo, ofisa mmoja alilidokeza gazeti hili kwamba mkuu wa zamani Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema, ambaye amestaafu, ndiye wa kulaumiwa kwa kutoheshimu mapendekezo ya wataalamu.
“Tulimwambia IGP Mwema kwamba ni vizuri kama maofisa wenye ulemavu kama baadhi ya vigezo wanavyo basi wapewe vyeo huko huko mikoani, lakini wasiende chuoni,” alidokeza na kuongeza;
“Tulipendekeza yafunguliwe madarasa ya kanda wakishafanya mtihani wa kawaida wapewe vyeo huko huko, lakini wakija chuoni ni lazima wahudhurie vipindi vyote ambavyo vinafanya chuo kiitwe chuo.
“Chuo chochote kile kina vigezo vyake na kwamba ili mtu apate cheo alichokwenda kukisomea ni lazima ahudhurie asimilia 95 ya vipindi ikiwamo kwata, medani za kivita na kuzuia vurugu,”alisema.
Chanzo kingine kililidokeza gazeti hili kuwa maofisa hao waliripoti chuoni hapo wiki mbili zilizopita na katika uchunguzi, walibainika wana ulemavu ambao hawawezi kumudu mafunzo ya ukakamavu.
Mmoja wa maofisa hao waliotimuliwa alilalamika kuwa kitendo hicho siyo cha kiungwana kwa kuwa ulemavu huo waliupata wakiwa kazini wakilitumikia Taifa na hawajashindwa kuingia darasani.
“Baadhi yetu tumefanya kazi miaka 20 wengine 25. Wamekatika miguu. Wako trafiki wamegongwa na polisi wengine wamepigwa risasi na majambazi wakapata ulemavu si sawa kutunyima vyeo,” alidai. (MWANANCHI)