Boko Haram Wateka Chuo Cha Polisi
Kundi la wapiganaji la kiislam
la Boko Haram,wamevamia shule moja ya mafunzo ya kipolisi.kituo hicho
cha mafunzo kilichoko kwenye kitongoji cha Gwoza kiko karibu na mpaka wa
nchi ya Cameroon ambacho hufundisha maofisa wa Polisi nchini Nigeria.
Kikundi hicha Boko Haram pia kinasemekana kuudhibiti mji wa jirani na Gwoza uitwao Buni Yadi.Nalo shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch wametoa takwimu ya vifo vilivyosababishwa na kundi hilo kua watu zaidi ya elfu kumi mpaka sasa tangu walipoanzisha harakati za kutaka upande wa kaskazini mwa Nigeria uwe chini ya utawala wa Kiislam.
No comments:
Post a Comment