Thursday, 14 August 2014

MUVI inaendelea:WIZI WA KIHISTORIA WA CHILE


Wizi wa kihistoria waleta aibu Chile

 14 Agosti, 2014 

Moja ya magari yaliyokuwa yamebeba pesa hizo
Chile imemfuta kazi afisaa mkuu wa usalama katika uwanja rasmi wa ndege baada ya tukio la kuaibisha la wizi wa zaidi ya dola milioni kumi katika sehemu ya kupakia mizigo.
Waziri wa ulinzi George Burgos, amesema kuwa uchunguzi umeanzishwa kuhusu namna wanaume 8 waliokuwa wamejihami kuiba pesa kutoka kwa gari lenye ulinzi mkali katika uwanja wa ndege katika mji mkuu Santiago.
Alitaja tukio hilo la Jumanne kama la kutia aibu na la kushangaza sana na linalostahili hatua kali.
Picha za video, zilionyesha genge hilo lililofanya kitendo chao kwa kujidai kuwa wafanyakazi wa uwanja wa ndege.
''Wakati uchungizi unapoendelea, afisa mkuu wa usalama katika uwanja wa ndege, Arturo Merino Benitez Airport ameachishwa kazi,'' alisema bwana Burgos.
Pia aliahidi kwamba usalama utadhibitiwa katika uwanja huo na kufanyiwa mabadiliko makubwa.
Wezi waliingia katika sehemu ya kupakia mizigo ya uwanja wa ndege wakiwa wamevalia nguo za kazi,na kulisimamisha gari lililokuwa limebeba pesa hizo. Inaarifiwa gari hilo lilikuwa na ulinzi mkali sana.
Pesa hizo zilikuwa zinaelekea katika benki na kampuni za migodi Kaskazini mwa Chile.
Wanaume hao waliwaondoa walianzi kwenye gari hilo na kuchukua pesa kabla ya kutoroka bila hata ya kufyatua risasi yoyote.
Kitendo chenyewe cha wizi ambacho ni kikubwa sana katika historia ya Chile, hakikunaswa kwenye kamera za ulinzi,bali walionekana wakitoroka.