Posted by GLOBAL on August 22, 2014
Mratibu wa Ziara ya
Wachezaji wa Zamani wa Timu ya Real Madrid,Ssebo (wa tatu kushoto)
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya mechi ya
kirafiki kati ya Tanzania Eleven na Timu ya Wachezaji wa Zamani wa Real
Madrid kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kesho.Mpaka sasa ni
wachezaji watatu tu ndio waliowasili nchini huku wengine kadhaa
wakitegemewa kuwasili mchana wa leo.Wachezahi hao ambao wapo nchini hivi
sasa ni Luis Figo (wa tatu kulia),Christian Karembeu (kulia) na Beki
Fernando Sanz Duran (wa pili kushoto).wengine pichani ni Mkurugenzi Mkuu
wa Kampuni ya TSN,Farough Baghoza na Kocha wa Timu ya Tanzania Eleven,
Jamhuri Kihwelo 'Julio'.…

Jamhuri Kihwelo 'Julio'.
Kocha wa Timu ya Tanzania
Eleven,Jamhuri Kihwelo "Julio" (katikati) akizungumzia namna Timu yake
ilivyojiandaa kuwakabili Wakali hao wa soka Duniani wakati wa Mkutano na
waandishi wa habari uliofanyika leo kwenye Hoteli ya SouthernSun jijini
Dar es Salaam.Kulia ni Luis Figo na kushoto ni Fernando Sanz Duran
ambao ni wachezaji wa zamani wa timu ya Real Madrid ya nchini Hispania.
Mchezaji Kiongozi wa Timu
ya Wachezaji wa Zamani wa Real Madrid,Luis Figo akizungumza na
Waandishi wa habari juu ya ujio wao hapa nchini.Figo amewaahidi wa
Tanzania kuwa yeye na Wenzake watatoa burudani kabambe katika Uwanja wa
Taifa jijini Dar hapo kesho.
Mchezaji Fernando Sanz Duran (kati) nae akitoa maneno yake kuhusu mchezo huo.
Mwanasoka Christian Karembeu akizungumza.
No comments:
Post a Comment