Friday, 22 August 2014

POLE KAMA ULIPATA KAZI UHAMIAJI.... ISOME KWA MAKINI

POLE KAMA ULIPATA KAZI UHAMIAJI....
Week Kama tatu zilizopita Udaku Special tuliweka Habari kuhusu Majina ya Waliofauli Usaili wa Nafasi ya Ukonstebo na Koplo Pale Uhamiaji ambayo ilisemekana yalikuwa yamechakachuliwa kwani wengi waliopata kazi hiyo walikuwa na undugu na wafanyakazi wa Idara hiyo, Baada ya Habari hiyo Serekali ilisimamisha mchakato huo kupisha uchunguzi , Leo taarifa zimepatikana kuwa ni ukweli majibu ya usaili huo yalichakachuliwa na kuwaacha waliofaulu na wahusika kuweka ndugu ama jamaa zao hivyo basi matokeo ya usaili huo yamefutwa rasmi Mpaka hapo Utakapofanyika Usaili Mwingine 

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil alisema hatua hiyo imechukuliwa baada ya kamati maalumu ya kuchunguza ajira hizo kubaini wazi kwamba waliopewa nafasi hizo hawakukidhi vigezo.

Abdulwakil alisema wizara imesikitishwa na udhaifu huo baada ya kubainika wazi kwamba malalamiko yaliyotolewa na wananchi na kusababisha wizara kuingilia kati na kufuta usaili wa kuitwa kwenye ajira kwa watu 200 ulikuwa sahihi.


Alisema baada ya kubainika kwamba kweli kulikuwa na upendeleo wa dhahiri kwani watahiniwa wenye sifa na waliopata alama za juu wakati wa usaili hawakuitwa na kukiukwa kwa vigezo vya wazi, ajira hizo zitatangazwa upya na kusimamiwa moja kwa moja na wizara na siyo idara hiyo kama ilivyokuwa awali.

No comments:

Post a Comment