September 6, 2014
Moja
ya gari ambalo lilikuwa kwenye msafara wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Katibu Mkuu wa Cuf, Maalim Seif
Sharif Hamadi baada ya kupata ajali, Misungiwi, Mwanza leo.
Hili ni gari lingine ambalo lenye usajili namba T397ANU nalo lilihusika katika ajali hiyo leo.
Keria ya moja ya magari yaliyopata ajali ikiwa chini baada ya kufyatuka baada ya ajali.
Baadhi ya wananchi wakishuhudia msafara wa Maalim Seif, mara baada ya ajali.
Msafara wa Maalim Seif ukijiandaa kuondoka mara baada ya magari mawili kati ya saba yaliyokuwa kwenye msafara kupata ajali.
Katibu
wa CUF Wilaya ya Nyamagana, Rehema Mwenda amejeruhiwa na kupelekwa
Hospitali ya Rufaa Bugando (kulia) na muonekano wa gari (kushoto) baada
ya ajali katika wilaya ya Misungwi, jijini Mwanza.
Mkuu
wa kitengo cha habari Wilaya, Mh Shido ambae pia ni Mwenyekiti wa Mtaa
Utemini Kata ya Mirongo amejeruhiwa na kupelekwa Hospitali ya Rufaa
Bugando.
Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamadi.
Habari zinasema msafara wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na
Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamadi umepata ajali ukihusisha magari
mawili ya msafara wa kiongozi huyo ambayo jumla yake yalikuwa saba
yalipogongana na lori lenye tela.
Akizungumza na
mtandao huu, Mkurughenzi wa Habari wa CUf, Adam Kambaya alisema
Viongozi wawili wa CUF, katibu wa wilaya ya Nyamagana na mwenyekiti wa
mtaa wa Nyamagana ambao hakuwataja majina wamelazwa katika Hospitali ya
Bugando kwa matibabu zaidi.
No comments:
Post a Comment