Saturday, 6 September 2014

HIVI HILI NI BASI AU BOKSI>>TASWIRA YA AJALI MUSOMA SIKU YA JANA

Posted September 6, 2014

Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS lenye nambari za usajili T 677 CYC lililokuwa likitoka Musoma kuelekea Kilari Mkoani Mara likiwa limeumia vibaya sana baada ya kugongana uso kwa uso na Basi lingine la Kampuni ya MWANZA COACH lenye nambari za usajili T 736 AWJ katika eneo la SabaSaba, Mjini Musoma mchana siku ya jana.

Basi la Kampuni ya MWANZA COACH lililokuwa likitokea Musoma kwenda Mwanza linavyoonekana baada ya kugongana uso kwa uso na basi la Kampuni ya J4 EXPRESS.
Hali Ilikuwa hivi katika eneo la tukio lililotokea ajali ya mabasi hayo kupata ajali baada ya kugongana.

Umati wa watu ukiwa umekusanyika kwenye eneo hilo lilikotokea ajali hiyo mbaya na kusababisha watu 39 kupoteza maisha papohapo.
Gari likiwa ndani ya mto baada ya kutokea ajali.

Guldoza likifanya kazi ya kuichomoa gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye namba ya usajili T 332 AKK lililosukumwa na basi hilo mpaka kuingia mtoni. Gari hili ilikuwa na watu watatu, ambapo wawili wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa.

Sehemu ya waokoaji waliofika kwenye tukio hilo.

Wanausalama wakijadiliana jambo kwenye eneo hilo la tukio.

Baadhi ya mizigo ya abiria wa mabasi hayo wakiwepo waliopoteza maisha.

Hivi ndivyo uokozi namna ulivyokuwa ukiendelea baada ya ajali kutokea.

  Polisi wakitoa miili ya watu wawili waliokuwemo kwenye gari hiyo.

MATUKIO YA AWALI YA AJALI HIYO ILIYOTOKEA MKOA WA MUSOMA NA ZAIDI YA ABIRIA 25 KUPOTEZA MAISHA.

Mabasi hayo yakiwa yamegongana
Baadhi ya miili iliyofariki katika ajali hiyo.




Basi la J4 Express lililokuwa linatoka Sirari kwenda Mwanza limegongana uso kwa uso na basi la Mwanza Coach lililokuwa linatoka Mwanza kwenda Musoma. Ajali imetokea katika eneo la daraja la sabasaba.

No comments:

Post a Comment