Wananchi wakishuhudia lori la saruji lililopinduka na kuua dereva wake leo eneo la Milima ya Sekenke mkoani Singida.
DEREVA wa lori lililokuwa limebeba saruji kutoka jijini Dar es Salaam
kuelekea Mwanza leo amefariki dunia baada ya lori hilo kupinduka eneo
la Sekenke mkoani Singida. Watu wengine wanne waliokuwa kwenye lori hilo
wamejeruhiwa.Mmoja wa mashuhuda wa ajai hiyo ameiambia tovuti hii kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kufeli breki kwa lori hilo lililokuwa likishuka Milima ya Sekenke na mpaka anaondoka eneo la ajali hiyo bado dereva (marehemu) na mmoja wa watu waliokuwemo aliyekuwa hai walikuwa bado wamenasa kwenye lori hilo.
No comments:
Post a Comment