Mrembo akataa kurejesha taji lake
2 Septemba, 2014
Mshindi wa taji la urembo nchini
Burma aliyenyang'anywa taji lake wiki iliopita ,amekataa kurudisha taji
hilo kwa waandalizi wa mashindano hayo Korea Kusini.
Katika kikao na wanahabari,Mya Myat Noe amesema
kwamba atarudisha tu taji hilo lenye thamani ya dola 100,000, ikiwa
ataombwa msamaha na waandalizi wa mashindano hayo.Wiki jana waandalizi walimshtumu kwa kukosa shukrani na kutokuwa mkweli.
Bi May ni mshindi wa kwanza wa shindano hilo nchini Burma , kulingana mwandishi wa BBC Jonah Fisher.
Bi May aliwaambia wanahabari kuwa alilazimishwa kudanganya kuhusu umri wake na waandalizi hao pia walimshurutisha kuwekwa matiti bandia.
Hata hivyo amekana madai ya kuwa alitoroka na taji hilo akisema kuwa aliabiri ndege kuelekea Myanmar bila kufahamu kuwa alikuwa ashavuliwa taji hilo.
Waandalizi walidai kuwa mwanadada huyo aliwadanganya na kuwadharau, ila hawakutoa maeleo zaidi.
Baadaye ilifahamika kwamba kulikuwa na mtafaruku kati ya mamake May na waandilizi hao kuhusiana na vipi Bi May anaweza kusimamiwa .
CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment