Thursday, 11 September 2014

PICHA ZA BUNGE MAALUM LA KATIBA


Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, ambaye pia ni mwanasiasa mkongwe, Mzee Kingunge  Ngombale  Mwiru akichangia leo katika mjadala wa Bunge  hio kuhusu masuala  ya uchumi mjini Dodoma.
 
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta akizungumza jambo leo  na  mjumbe mwenzake Mhe . Anne Makinda ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma leo.
Askofu  Amos  Muhagachi  akichangia katika mjadala wa Bunge Maalum la Katiba kuhusu sura zilizobakia  katika Rasimu ya Katiba Mpya mjini Dodoma leo.
 
Mjumbe  wa Bunge Maalum la Katiba,  Mhe . Anne Makinda ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  akizungumza jambo na  mjumbe mwenzake Mhe. Jenister Mhagama  mjini Dodoma leo.

No comments:

Post a Comment