Picha yapamoja
BENKI ya NMB imefanya mkutano wake wa
mwaka na umoja wa wateja wao(NMB BUSINESS CLUB) na kuwafundisha ujasiliamali na
fursa za biashara.
Katika mkutano huo Wateja hao pia
walitoa maoni mbali mbali ya uboreshaji wa huduma za kibenki ikiwa ni pamoja na
maofisa wa benki hiyo kutambulisha bidhaa na huduma mpya kwa wateja.
Mwezeshaji katika Mkutano huo alikuwa ni
Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Rosemary Senyamule, ambaye pia ni Mtaalamu wa Biashara
na Ujasiliamali ambaye aliwafundisha wateja hao upatikanaji wa fursa na namna
ya kutafuta masoko kwa wakati huu.
Senyamule pia alitoa wito kwa
Wafanyabiashara na Wajasiliamali kutumia mitandao ya kijamii kutangaza
bidhaa zao ikiwa ni pamoja na kutafuta masoko ya kimataifa.
Alisema wafanyabiashara wa sasa
hawapaswi kubweteka kwenye maduka yao kusubiri wateja bali wanapaswa kuzunguka
kutafuta fursa zingine na kuzitumia ili kujiongezea vipato zaidi na sio
kulizika na aina moja ya shughuli anazofanya.
Alisema mitandao ya kijamii ikitumika
vizuri kwa wafanyabiashara itasaidia kumtafutia masoko kimataifa na kuitangaza
biashara yake kwa gharama ndogo na sio kuwaachia vijana kwamba ndio wanaostahili
kutumia mitandao hiyo.
Aliongeza kuwa Tanzania na Mkoa wa Mbeya
kuna fursa nyingi ambazo wafanyabiashara wanaweza kuzitumia na hatimaye
wakaongeza vipato vyao ikiwa ni pamoja na sekta ya Uwekezaji ambapo aliwataka
wafanyabiashara kutumia fursa hiyo na sio kuwaachia wawekezaji kutoka nje.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Wateja
wa Nmb, Jeremia Mahenge,alisema tangu umoja huo uanzishwe changamoto nyingi
zimetatuliwa kutokana na Benki hiyo kupokea maoni kutoka kwa wateja wao kupitia
umoja huo.
Alizitaja baadhi ya changamoto ambazo
zimeboreshwa kuwa ni pamoja na ongezeko la mikopo na kupungua kwa makato kwa
wafanyabiashara, kupungua kwa foleni wakati wa kupata huduma pamoja na
uboreshaji wa huduma ambapo hadi sasa Benki hiyo imeongeza siku za kufanya
kazi.
Naye Meneja Mahusiano wa NMB Makao
makuu, Dickson Pangamawe, alisema lengo la kuanzisha umoja huo ni baada ya
kuona Benki inashindwa kupata maoni kutoka kwa wateja wao kirahisi pamoja na
kutambulisha bidhaa zinazoanzishwa na benki hiyo kwa wateja.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment