WAJUE WAVUMBUZI WALIOIBADILISHA DUNIA KIMAENDELEO
Posted by GLOBAL on September 4, 2014
Maandishi kwa ajili ya wasioona yaliyogunduliwa na Braille.
BRAILLE: Kipofu huyu aligundua maandishi ya watu
wasioona. Huyu aliubadilisha ulimwengu ‘mweusi’ na kuupa shule ya
mwangaza. Waliopatwa na upofu baadaye hawakuwa na tatizo katika kupata
digrii (shahada) hata bila ya uwezo wa kuona. Hivi sasa teknolojia hiyo
inataka kuhamia kwenye simu za vipofu pia. Soma zaidi kwenye mtandao wa
Google ujionee. Hapa nakuwekea picha ya simu uelewe kitakachokuja kwenye
simu kuhusiana na Braille. Kwa kifupi, Braille alizaliwa Januari 4
mwaka 1809 na kufariki Januari 6 mwaka 1852.
Davy Humphry aliyevumbua balbu.
DAVY HUMPHRY: Huyu alivumbua balbu zote zinazotumika
duniani kutoa mwanga wa umeme katika karne ya 18 ambapo aliunganisha
waya mbili kutoka kwenye betrii mpaka kwenye ncha ya hewa ya kaboni.
Peter Durand aliyevumbua chombo cha kuuzia vyakula kwenye makopo.
PETER DURAND: Huyu alivumbua chombo cha kuuzia
vyakula kwenye makopo ambavyo hukaa kwa muda mrefu bila kuharibika.
Vyakula hivyo kwa Kiingereza huitwa ‘canned food’ yaani vyakula
vilivyowekwa kwenye makopo kama vile maharage, nyama, njegere, na
kadhalika. Uvumbuzi huu ulikuwa mwaka 1810 ambapo uliwapa shida
watumiaji kuzifungua bidhaa hizo kwenye makopo hayo hadi mwaka 1858
ambapo (can opener)yaani kifungulio cha makopo hayo kilipotengenezwa kwa
mara ya kwanza na Ezra Warner mwenyeji wa Connecticut, Marekani.
Josephine Garis mmoja wa waliovumbua mashine ya kuoshea vyombo (dish washer).
JOEL HOUGHTON NA JOSEPHINE GARIS: Hawa walivumbua mashine ya kuoshea vyombo (dish washer).COENRAAD JOHANNES VAN HOUTEN (1801-1887): Huyu ni Mdachi (raia wa Uholanzi) aliyetutengenezea mashine ya kukobolea cocoa na kuanzisha biashara ya chokoleti duniani.
Froebel ambaye ndiye mwasisi wa shule za watoto chini ya miaka mitano.
FROEBEL, WILHELM: Alikuwa mwasisi wa shule za watoto chini ya miaka mitano (chekechea a.k.a shule za vidudu) huko Ujerumani.Alifungua shule ya kwanza huko Bad Blankenburg (karibu na Keilhau) mwaka 1837. Hata hivyo, serikali ya Ujerumani ilizifunga shule zote za chekechea, kwa sababu zisizojuolikana, kwa miaka tisa tokea mwaka 1851 hadi 1860 ambapo ziliruhisiwa tena.
No comments:
Post a Comment