Thursday, 11 September 2014

WAZO LA LEO::Unawapa Somo Gani Wadada Waliobakiwa na Vitu Vya Kuhongwa na Kuyakosa Mapenzi?



Unawapa somo gani wadada waliobakiwa na magari ya kuhongwa, Simu za gharama za kuhongwa, majumba ya kuhongwa huku wakiyakosa Mapenzi na kusema Watapaki kuwa Single Ladies forever?

Hakuna kitu kinachoumiza moyo kama mapenzi hata kama unamiliki dunia.

Utajikaza tu lakini, maumivu yako pale pale; hata unywe hadi ulewe, uvute hadi uchizike.

Cha muhimu ni kumheshimu akupendae, hasa kama tayari mpo kwenye kiapo cha ndoa. 

Mwaka juzi ilitokea nchini Nigeria; Wanawake zaidi ya 8,000 waliandamana hadi kwa waziri kuitaka serikali iwatafutie wanaume wa kuwaoa, la sivyo watachukua wanaume wa wale wenye ndoa ili wawatumie kwa zamu.

Kunda Mwanamke Ndugu yangu Kabisa Wakati wa Ujana wake Alikuwa Moto wa Kuotea Mbali Uzuri Wake Ulimdatisha Kila Mtu Kiasi Akaapa Hata Olewa na Alikusanyia Mali nyingi sana kutoka kwa Wanaume Wakware..Sasa yupo na Miaka 42 anajuta kwa upweke alionao Japo Anakila Kitu plus Majumba Hakuna anaye mtaka nae zaidi ya vijana Kumchezea na Kusepa.

It is easy to say "i want to be single lady" but it is very difficult to maintain singlelism.

No comments:

Post a Comment