Sunday, 19 October 2014

HABARI::JK ahitimisha Mafunzo ya Wakongo...Atunuku kamisheni kwa watanzania 23

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametunuku kamisheni kwa maafisa wapya wa Kitanzania 23 miongoni mwa maafisa 437 wa kundi la 53/13 – Kongo. Kundi hilo liliwajumuisha maafisa wa kitanzania wapatao 23 na wahitimu 414 kutoka Kongo.

Jumla ya wanajeshi 414 kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo  leo (18/10/2014 wamehitimu mafunzo ya Uafisa katika chuo cha maafisa  (TMA) Monduli baada ya kufanya kozi kwa muda wa mwaka mmoja.
Maafisa hao wanafunzi kutoka Kongo walipata mafunzo hayo pamoja na maafisa watanzania 23 waliohitimu leo na kupata kamisheni ya cheo cha luteni usu baada ya kula kuapa mbele ya Mhe. Rais Dkt Jakaya Kikwete.
Tofauti na kamisheni zingine kwani pamoja na Mhe. Rais Kikwete aliweza kutoa Kamisheni kwa maafisa wapya wapatao 23 .
Aidha, leo hii kitu ambacho ni kigeni vijana kutoka kongo walihitimu pasi kutunukiwa kamisheni kwani kulingana na taratibu maafisa  wa kongo wanapaswa kupewa kamisheni na Rais na wakiwa katika ardhi yao, hivyo wahitimu hao watakapewa kamisheni nchini mwao.
Akitoa shukurani kwa Rais Kikwete wa Tanzania, Rais Joseph Kabila ambaye alishuhudia maafisa wake wakihitimu mafunzo hayo, alisema anawashukuru kwa kukubali kutoa mafunzo kwa maafisa hao.
Pia alisema anaamini atakuwa amepata makamanda wazuri watakaosaidia kuimarisha usalama nchini mwao na pia kuondoa maadui wanaohatarisha amani nchini Kongo.
Miongoni mwa viongozi waliohudhuria sherehe hizo Wazri wa Ulinzi na JKT, Mhe. Dkt Hussein Ali Mwimnyi, Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe, Katibu mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Waziri Mkuu Mstaafu na mbunge wa Monduli, Mhe. Edward Lowasa, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Magesa Mlongo, majenerali, majenerali wastaafu, na mabalozi wa kijeshi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.
kwa upande wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Naibu Waziri Mkuu na waziri wa Ulinzi, Alexander Luba Ntambo, na Waziri wa Mambo ya Nje, Raymond Tshibanda N’tungamulongo, Balozi wa Kongo nchini Jean Pierre Juma Alfani, Mkurugenzi wa Idara ya Usalama Kahimbi Delphin na Mkuu wa Mafunzo, ya Kijeshi,  brigedia Jenerali Aguru Mamba Maurice.

No comments:

Post a Comment