Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Dkt.Yahaya
Msigwa akiongea na waandishi wa habari jana mjini Iringa kuhusu ziara
ya siku sita ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana aliyeifanya
mkoani hivi karibuni. (PICHA NA FRIDAY SIMBAYA)
NA FRIDAY SIMBAYA
Katibu Mwenezi wa Chama
cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Dkt. Yahaya Msigwa amesema kuwa ziara ya
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana aliyeifanya mkoani hapa imesaidia
kuponda mawe magumu na kutuachia mawe madogo madogo.
Akizungumza na waandishi
wa habari jana kuhusu mawe magumu hayo ndani ya chama katibu mwenezi huyo wa
mkoa alisema kuwa ziara ya siku sita ya kinana kutatua kero mbalimbali
zilizokuwa zinakikabili chama hicho.
Alisema kuwa kiongozi
huyo wa kitaifa aliwapa fursa wananchi kuuliza maswali ambayo yamesadia kuibua
changamoto mbalimbali na wao kama chama mkoa kero hizo wanaendelea kuzifanyia
kazi.
“Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana na Katibu wa Itikadi
na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye walikuwa katika ziara ya siku sita mkoani Iringa kuimarisha
uhai wa chama, kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010
pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi,” aliongeza
katibu mwenezi wa mkoa huyo.
Aidha, katibu mwenezi
huyo wa mkoa alisisitiza viongozi kuwa karibu na wananchi ili kuweza kusikiliza
matatizo yao kuliko kukaa ofisini kuhusu kuletewa kero hizo ofisini.
Alisema kuwa katibu mkuu
kinana alisisitiza umuhimu wa kuweka viongozi wanaokubalika na wananchi pamoja
kuheshimu moani ya wananchi ili kusimamisha viongozi wanaokubalika kwa kufuata katiba, kanuni na taratibu za
chama.
Wakati huohuo, Katibu
Mwenezi CCM Mkoa, Dkt. Msigwa aliwaasa wananchi kujiandikisha katika daftari ya
mpigakura ili wawezekushiriki kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa
na ule Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Alisema kuwa ni lazima
wananchi wa hakikishe wanachagua viongozi wazuri wanaotokana na chama cha CCM
ili kuweza kudumisha amani na utulivu wa nchi yetu kama tunu aliyetuachia Baba wa Taifa Hayati
Mwl. Julius Nyerere.
No comments:
Post a Comment