Thursday, 16 October 2014

IRINGA::Akamatwa na bangi katika bakuri


Watu wawili wanashikiliwa na Jeshi la polisi mkoani Iringa kwa makosa
tofauti tofauti likiwemo la Rahedy Josephat (23) mkazi wa Ipogoro
kukutwa akiwa na bhangi kete 43.


Akizungumza ofisini kwake,
Kamanda wa polisi mkoani Iringa ACP Ramadhani Mungi alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 13 Oktoba majira ya
saa 12 za jioni maeneo ya kata ya Ruaha.

Kamanda alisema mtuhumiwa huyo alikutwa akiwa amezihifadhi kete hizo
katika bakuli la kuwekea chakula.

Tukio lingine, mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la John Bosco alikutwa
akiwa na silaha aina ya shotgun yenye namba za usajili 66721 na risasi
zake 10 akizimiliki bila kibali.

Kamanda alisema mtuhumiwa huyo ambaye alikamatiwa maeneo ya kijiji cha
Mmbweleli kilichopo kata ya Migoli wilaya ya Iringa Vijijini pamoja na
kukamatwa na hivyo vitu pia alikutwa akiwa na nyama ya swala kilo nne.

Mbali na matukio hayo, kamanda alisema watu wasiofahamika walimvamia
Happy Ingasi (36) ambaye ni mfanyabiashara na kumnyang’anya fedha
taslimu shilingi Milioni 2.5, simu aia ya tecno pamoja na vocha
mbalimbali zenye thamani ya shilingi milioni 3.5 baada ya kumshambulia
na panga.

Tukio hilo lilitokea tarehe 13 Oktoba majira ya saa 2 za usiku huko
maeneo ya Nduli wilaya ya Iringa Vijijini ambapo watuhumiwa bado
wanatafutwa na Jeshi la polisi.
NA DIANA BISANGAO WA MATUKIODAIMA.CO.TZ IRINGA

No comments:

Post a Comment