NA FRIDAY SIMBAYA, IRINGA
Jeshi
la polisi mkoani Iringa linamshikilia Gwerino Ngaga (70) mkazi wa Mbigili kwa
kosa la kumpiga risasi kifuani Thadei Mbugu(40) mkazi wa Mbigili na
kusababishia kifo chake papo hapo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi akielezea tukio hilo la kinyama kwa waandishi wa habari ofisini
kwakw leo alisema kuwa limetokea Oktoba 9 majira ya saa moja za jioni katika kijiji chaMbigili kata ya Lugalo tarafa
ya mazombe wilaya ya kilolo mkoani hapa.
Kamanda Mungi alisema kuwa awali kabla ya tukio marehemu pamoja na mtuhumiwa
wakiwa na wakezao walikuwa wakinywa pombe za kienyeji katika kilabu kinachoendeshwa na mke wa Gwerino.
Mungi alisema kuwa sababu kubwa ya mtuhimiwa kumpiga risasi marehemu Thadei
lilitokea mara baada ya mke wa mtuhumiwa kumuomba pesa marehemu mbele ya mkwewe na mumewe kitendo kile kilimuudhi mtushtakiwa na kuamua kuenda nyumbani kuchukua bunduki aina
ya shortgun na kumpiga kifuani hali
iliyopelekea kupoteza maisha.
‘’Hawa jamaa walikuwa wote na wake zao
wakipata kinywaji sasa wakati wanakunywa huyu mke wa mtuhumiwa alimuomba marehemu
ampe hela ya kutumia na mke wa wa marehemu aliposikia mumewe akiombwa hela
alifoka kwa nguvu kwa kulaani kitendo cha mumewe kumhonga mke wa mtu hela tena
kilabuni huku angali akiwa na mumewe’’
“Sasa mume wa yule mke aliposikia mkewe
anapewa hela na marehemu alimuuliza kisa cha kumdhalilisha kwa kumpa mkewe hela
mbele yake ndipo marehemu akamjibu kwa dharau kuwa amezeeka na hivyo hana hela
hivyo anamsaadia kumlea kitendo kilichomuudhi mstakiwa na kumlipua kwa bunduki
yake,” alisema Mungi.
Mtuhumiwa huyo anashikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi wa karibu ili kubaini
nini chanzo hasa kilichosababisha mtuhumiwa kuchukua bunduki na kumpiga mwenzie kwani hapo awali kulikuwa hakuna ugomvi wowote na wote walikuwa
ni majirani wanaokaa mtaa moja .
Mungi alieleza kuwa baada ya kufanya
uchunguzi wa awali walibaini kuwa bunduki hiyo aina ya shotgun iliyotumika katika mauaji hayo
inamilikiwa kihalali na Gwarino Ngaga mkazi
wa Mbigili.
No comments:
Post a Comment